Unaweza
kutuambia kidogo kuhusu wewe na blog yako?
Mimi naitwa Augustino Chengula niliyehitimu shahada ya kwanza ya Tiba
Mifugo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Morogoro mwaka 2007. Blog
yangu inaitwa “SEKTA YA MIFUGO TANZANIA” inayobeba jina linaloendana na kile
kinachowasilishwa katika blogu hiyo. Lengo kubwa la blog ni kuelimisha umma na
wafugaji juu ya ufugaji na namna ya kukabiliana na magonjwa ya mifugo.
Je,
wewe kazi yako ni kublog tu au hii ni kama kazi ya muda tu au hobby?
Kublog si kazi yangu ila ni hobby tu na lengo langu kubwa ni kuelimisha
umma na hasa wafugaji juu ya mifugo na ufugaji na mambo yanayoendana na hayo.
Hivyo naelimisha umma kwa kupitia fani yangu ya mifugo.
Jinsi
gani unaanza kublog na kwa nini?
Kabla hata ya kuanzisha blog nilikuwa najaribu
kutengeneza tovuti yangu kwa kupiatia zile za bure. Baadaye nikaona kwa
kuchelewa watu wanablog na mwanzo sikujua kama ni za bure. Nilipojua kuwa ni za
bure nikaanza kujifunza mwenyewe namna ya kufungua blog, nikafanikiwa. Nikawa
naendelea kuiboresha taratibu kwa kuangalia blog za watu wengine zipoje. Wakati
mwingine nilitumia Jamii forum kuuliza kama nataka kufanya kitu fulani kwenye
blogu inakuwaje. Sikuwa na elimu ya web designing lakini nilijua kutumia vitu
vya kawaida katika computer. Kupenda kujifunza vitu mwenyewe vilinisaidia.
Lengo kubwa la kuanzisha ni kutaka kuwagawia elimu ya ufugaji watu wengiene
kwani niliona wanahangaika kuitafuta hasa katika lugha ya kiswahili kwani mambo
mengi yapo kwa lugha ya Kiingereza.