Mwanablogger wa week hii ni Ngwesa Paulo

Naitwa Ngwesa Paulo ni mhitimu wa chuo kikuu nina shahada ya utalii. Naishi Morogoro niliamua kuanzisha blog ambayo itakuwa inatoa habari mbalimbali kuhusiana na utalii Tanzania ili kuhamasisha utalii wa ndani na nje pia utupe faida mana tunavivutio vingi sana.

Kublog kwangu ni kama kazi wala sio kama hobby, kublog nilianza kama miezi sita iliyopita nilianza na blog inayokwenda kwa jina la Hapa hapa Tourism nikaona haileti maana niliyokusudia ndio nikanzisha hii ya NGWESA.

Kitu kilichonisukuma nianze kublog ni pale nilipoona hapa Tanzania tuna vivutio vingi sana lakini bado havijulikani waliopewa hiyo zamana hawaifanyi nikaona naweza fanya kazi hii kirahisi kwa kutumia blog.

Changamoto ninazozipata katika kazi hii ni ukosefu wa vitendea kazi vya uhakika kama kamera
zenye uwezo, ukosefu wa wazamini wa kudumu katika kazi hii kwa ujumla.

Wakati sighuliki na kazi za hii blog nafanya kazi zingine za kimaisha na mara nyingi nikiwa mbali na kompyuta huwa nafikilia sana blog yangu.

Wasomaji wa blog yangu ni watu wote tu Duniani kwa ujumla mana ni ya mambo ya kitalii hayana mkubwa wala mdogo.

Ili habari za blog hii ziwafikie watu wengi zaidi huwa natumia mitandao ya jamii kama facebook pamoja na twitter pia huwa nawaomba watu wenye blog zinazojulikana kuwatangazia wasomaji wao kama kuna blog nyingine ya mambo ya kitalii.

Changamoto kubwa wakati wa kutengeneza post ninayopata nazani network na pale ninapojiuliza je hii post itafaa , inapotokea sina la kuandika kwenye blog huwa naacha tu kwa siku hiyo ili niweze kutuliza akili nisije haribu mana kazi hii inatakiwa umakini mkubwa sio kucoppy na kupaste.

Mkakati wangu ni kuutangaza utalii wa Tanzania ujulikane zaidi mana bado upo chini pia blog yangu ijulikane na watu wengi kimataifa.

Katika kuweka habari ni bora kupata ukweli au uchunguzi wa jambo ambalo blogger anataka kuweka kwenye blog yake kupitia watu wengine au yeye mwenyewe. pia jambo mhimu ambalo blogger anaweza wapatia wasomaji wake ni habari zenye uhakika zaidi.

Style yangu ninayotumia kublog ni habari zinazoambatana na picha siunajua katika habari kama hizi za kitalii picha ni mhimu sana na maelezo yake kidogo.

Ili kujenga kujulikana mimi na blog yangu nimekuwa nikipost vitu vizuri ambavyo vinaweza kuwavutia watu wengi zaidi ili kuwafanya wapende kutembelea blog yangu kila mara pia huwa nawaomba watu wenye blog zinazojulikana zaidi kuwajulisha wasomaji wao kama kuna blog hii ya mambo ya kitalii pia.

Katika kupost ni kweli kila mtu anapest yake anayoipenda na nayoichukia kwa upande wangu post zangu zote nazipenda mana ni utalii tu kwa sana sijui kama zinachukiza.

Blogger ninaowangalia na kuwafata nyayo zao ni Issa Michuzi, Dj Choka , Bukopasport hawa nawapenda kwasababu waipenda kazi yao kublog kwao ni kazi pia ukiwa na shida kuhusiana na blog sio wagumu kukusaidia.

Nimekuwa nakutana na watu wa aina mbalimbali ambao hunikatisha moyo na wengine hunisupport wakati nasghulikia post zangu lakini sio mabya ndivyo ilivyo.

Mtu akiacha comment inayodai marekebisho ushauri nazani anahitaji kuona kitu alichokuambia ukikifanyia kazi na comment zingine huwa hazihitaji majibu mana huwa ni za kukupongeza tu.pia kuna dhamani kubwa kujibu comment iliyoachwa na msomaji hata kama hatarudi kusoma tena wengine ataiona kama ilijibiwa. Wasomaji wanaoacha comment kwa majina yao nazani kuwaacknowledge ni vizuri zaidi.

Pia sio makosa msomaji kucomment kwa kutumia jina linguine mana kinachohitajika comment na si jina la mhusika,

Mimi sio mtu wa kuakata tama kirahisi mana kukata tama nafanisha na kosa kubwa kama padre kumbaka muumini wake ni hatari sana, watu wanaokata tama wanahatari kubwa sana katika maisha yao.

Picha zangu ninazoweka katika post ni picha za uhalisia mana huu ni utalii uhitaji edit wala nini uhalisia ndo mpango.

Katika hii blog yangu nazani sina post post ambazo ziko very controversy kwa hiyo ni amani tu mimi na wasomaji wangu kitalii tu zaidi.

Huwa najisikia faraja sana ninapo weka post na kupata maoni ya watu wengi mana inaonesha kazi yangu imekubalika kwa watu wengi zaidi. Swala la wat mashuhuri wanaruhusiwa kutoa maoni pia kama watu wengine tu.

Katika kupost habari na kitu chochote kwenye blog yangu natumia jina langu harisi mana hii ni kazi kama kazi zingine uhuni uhini hautakiwi katika ofisi yoyote naheshimu ofisi yangu.

Baadhi ya malengo ya blog yangu kwa mwaka huu ni kuifanya ijulikane zaidi na watu wengi imataifa.baada ya mda natumaini itakuwa blog bora kwa mambo ya kitalii hapa Tanzania.

Ushauri wangu kwa wale watu wanaotaka kuanza kublog ni kutafuta wazo jipya katika kufanya kazi hii sio kucopy na kupaste sio vizuri ze comedy wanaweza waona na kuwatania.

Mi nazani lengo kubwa la wanablogger wengi ni kupata wasomaji wengi zaidi na kazi zao kujulikana zaidi ili iweze kuwa kazi ya kuwaingizia kipato.

2 comments:

emuthree said...

Hongeta sana mkuu, tumekupata na tunashukuru sana mpendwa kwa kuwajali wenzako!

Unknown said...

pamoja sana
karibu kijana