Kutana na Mwanablogger Umar Makoo


  1. Unaweza kutuambia kidogo kuhusu wewe na blog yako? Mimi naitwa Omari Abdallah Makoo na blog yangu inaitwa BUSTANI YA HABARI
  2. Je, wewe kazi yako ni kublog tu au hii ni kama kazi ya muda tu au hobby? Hapana mimi kazi yangu sio kublog tu bali ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika mwaka wa masomo utakao anza hivi karibuni pale MUSLIMUNIVERSITY OF MOROGORO
  3. Jinsi gani unaanza kublog na kwa nini? Mara ya kwanza nilipata hamasa ya kublog baada ya mhadhiri wa chuo kugusia swala la utengenezaji wa blog,faida na namna ya kutengeneza blog.Sababu iliyonisukuma kublog ni shauku ya kuhitaji kufukisha habari katika jamii mbali mbali nikiwa na chombo cha kujitemea mwenye kikiwa kama hazina ya habari.
  4. Nini changamoto unazozipata kwa kuwa na blog? Mwanzo nilikumbana na tatizo la uchache wa visitors ingawaje swala hilo halipo kwa sasa,Pia uchache wa vifaa vya kukusanyia habari pamoja na kukosa watumishi.
  5. Ni miaka mingapi sasa umekua ukiblog? Huu ni mwaka wa tatu nikiblog katika blog yangu inayoitwa MIRACLES OF ALLAH(omarimakoo.blogspot.com) ingawa kwa hii blog ya sasa ya BUSTANI YA HABARI inamiaka miwili tu.
  6. Unafanya nini wakati ukiwa hushughulikii hii blog yako? Mara nyingi hua na jisomea vitabu mbali mbali na muda mwwingine huwa najiunga na ndugu, jamaa na marafiki kubadilishana mawaz.
  7. Ni mara ngapi unafikiri juu ya blog yako wakati uko mbali na kompyuta? Kwa kweli huwa haiesabiki kwani kila ninapokuwa mbali na blog huwa najihisi kublog na utamani kuifikia kompyuta yangu.
  8. Ni nani wasomaji wa blog yako? Blog yangu imekuwa na wasomaji wa rika mbali mbali kutokana na contens zake kufaa kwa jamii ya rika lolote.Pia nimekuwa nikipokea wasomaji wa ndani ya nchi na nje ya nch. 
  9. Je ni mitandao gani mingine ambayo unatumi ili iweze kukusaidia kuitangaza blog yako ili iwafikie wasomaji walengwa wa blog yako? Mfano Twitter au Facebook.Mimi huwa natumia Facebook,Twitter,Stumble pamoja na +google kwa wasomaji wa mitandao ya kijamii
  10. Nini hasa ni changamoto kubwa wakati unatengeneza posy ya kuweka kwenye blog yako na kwanini? Changamoto kwenye kuweka post ni kutambua nini hitajio la wasomaji kwa sababu unapokuwa na wasomaji wengi pia wanakuwa ni wapenzi wa habari tofauti hivyo huwa naumiza kichwa sana kabla sijaweka post
  11. Unafanya nini iwapo kuna wakati huna la kuandika kwenye blog yako? Ninapokosa la kuandika kenye blog huwa natumia muda huo huo kuchat na wasomaji wa blog yangu waliopo kwenye mitandao ya kijamii
  12. Je ni nini mkakati wako na blog yako kwa ujumla? Ninampango wa  kuwa na kituo maalum cha habari kikiwa na title ya jina hili la BUSTANI YA HABARI
  13. Je ni bora kupata ukweli au uchunguzi wa jambo unalotaka kuliandika kwenye blog yako wewe mwenyewe au kupitia mtu mwingine? Ni vyema ukafanya uchunguzi juu ya jambo kabla haujaliandika na sio kusikia kwa mtu na kulipost kwenye blog kwani wanajamii wanatuamini na wametukabizi zamna ya kuwapatia habari sahihi kwa kutuamini na kutembea blog zetu mara kwa mara.
  14. Ni jambo gani bora blogger anaweza kutoa kwa wasomaji wake? Ni vyema blogger awe na makala za kuelimisha jamii ili kuifanya blog sio tu cha habari bali pia ni chanzo maarifa.
  15. Ni jinsi gani (mtu) anaweza kuelezea style ya yako unavyo blog? Anaweza kueleza kwamba ni blog ya kisasa yenye post zinazokwenda sambamba na mila na desturi za jamii mbali mbali na kukidhi mahitajio ya upatikanaji wa habari sahihi.
  16. Ni nini imekuwa mkakati wako kwa ajili ya kujenga kujulikana kwa mwenyewe na blog yako? Mikakati ambayo nimeifanya ni pamoja na kusabmit blog yangu kwenye searching engine zaidi ya mia tatu na pia kuwapa uhuru wasomaji wangu kuweza kuwasiliana nami.Pia kuisajili hapa ikiwa ni sehemu ambayo wasomaji wengi hufika pamoja na kutarajia kushiriki mashindano yaliyoandaliwa nanyi ili nitakaposhinda inipe nafasi zaidi ya kuwafikia wasomaji wangu.
  17. Kila mtu ana post anayoipenda au anayoichukia. Je wew ni post ipi unaipenda sana na kwanini? Na ni posy ipi unaichukia sana na kwanini?napenda sana post za kusisimua wasomaji wangu na nachukia sana post zenye picha za nusu uchi au uchi kabisa.
  18. Je ni bloggers wapi ambao wewe unawaangalia na kufuata nyayo zao? Na kwanini?Blog ambayo inanisisimua ni JICHO LA HABARI(www.ahmadamwariko.com) pamoja na SHAFFIH DAUDA.Watu hawa huwa wanaweka post mara kwa mara na pia hukidhi mahitajio ya wasomji wao.
  19. Hebu tuambie ni watu gani umewahi kukutana nao wakati ukisughulikia post za kuweka kwenye blog yako? Kwa kweli nimekutana na watu wa aina mbalimbali madiwani na hata wabunge
  20. Je unafikiria kuwa unadaiwa na mtu akiyeacha comment/s kwenye blog yako? Ndio tena ni deni lisilo na msamaha
  21. Je kunadhamani kujibu comment iliyoachwa kwenye blog yako wakati ukijua kuwa huyo aliyeiandika labda hatarudi kusoma jibu lake tena? Ni muhimu sana kwani comments huenda ikawa sababu ya kukidhu mahitajio ya wasomaji wengine ambao wationa comments hiyo.
  22. Je, umewahi kufikiria kuacha kupost comment ambayo iko negative kwako na ukijua hamna mtu atakayejua? Hapana cjawafikiria fanya hivyo kwani hata negative commnts hunijenga kiuandishi.
  23. Je unazitreat tofauti au unafikiri watu wanaoacha comment kwenye blog yako na kuacha majina yao yaonekane wazi wanastaili comments zao kujibiwa au hata kuacknowledge kuwa umeona maoni yao? Yes ni vyema kujibu comments zao na pia majina yao kuonekana ili kumfanya msomaji na wasomaji wengine kupata moyo wa kuendelea kucomments
  24. Je, unafikiria ni makosa kucomment kwenye blog yako kwa kutumia jina lingine? Yes sibusara kutumiajina la mtu mwingine ili ucomment kwani unapoweka post yenye jina lako unaifanya komment yako iwe na thamani zaidi.
  25. Je unazichukulia comments zote sawa unazotumiwa kwenye blog yako bila kujali maoni uliachwa? Huwa nazingatia ujumbe ulioachwa na asomaji wangu kwani kia aliecomments anacomment kwa maengo mahususi hivyo anastahili jibu stahiki.
  26. Je, unaamini comments kwenye blog yako zilizoandikwa kwa urefu sana zinahitaji kuzawadiwa zaidi kuliko zile zilizoandikwa kwa ufupi tu? Hapana kuna jumbe fupi ila zinaujumbe ulioshiba hivyo hutizama kiini cha ujumbe pasina kujali urefu au ufupi wa ujumbe.
  27. Je wewe ni mtu ambaye uko rahisi kukata tamaa? Hapana mimi si mwepesi kukata tamaa kwani,mtu halisi hakati tamaa
  28. Je unaedit picha zako ili ziwavutie sana wasomaji? Si mara zote huwa na fabya hivyo bali ni mara kadhaa tu
  29. Je unaepuka kuweka post ambazo ziko very controversy kwasababu ya kuogopa watu hawatakubaliana na wewe au huna hizo post? Zipo post za mtindo huo na huwa na weka paisna kuogopa changamoto itakayoibuka
  30. Je  unajisikia vizuri zaidi ukiweka post kwenye blog yako na ukapata maoni ya watu zaidi ya 20 au ukipata maoni ya mtu mmoja mashuhuri tu? Maoni ya watu wengi huvutia zaidi na kunipa moyo zaidi ya kazi yangu
  31. Je unasema blog yako kuwa inamafanikio iwapo unapata watu wengi wa kusoma  au unapata watu wengi wakuacha comment kwenye blog yako? Mafanikio ya blog kwangu hujengwa na vyote viwili kuwa na wasomaji wengi pamoja na kuwa na watu wenye kuacha maoni kwenye blog.
  32. Je blog yako unatumia jina lako kamili au unablog kwa kutumia kivuli kingine na watu wanasoma na kuenjoy blog yako lakini hawajui wewe ni nani? Natumia jina langu kamili ingawa limeanza na umar makoo baadala ya omari makoo lakini lina maana sawa.
  33. Ni nini baadhi ya malengo yako ya mwaka huu kwa ajili ya blogu yako au unaonaje mwenyeew kwa kipindi cha mwaka mmoja ua mitano toka sasa hivi blog ya itakuaje? Kwanza kondoa neno blogspot katika blog pili ni kuitanua zaidi kwa kuwa mawkala watkaonisaidia kukusanya habari sehemu mbali mbali.
  34. Je upi ujumbe wako kwa wale watu wanaotaka kuanza kublog? Wawe na malengo ya kuwafikishia jamii habari zilizo sahihi ili
  35. Je kwa maoni yako ni lengo gani kubwa kwa mwanablogger? KUFIKISHA TAARIFA KWA JAMII YENYE KUKIDHI MAHITAJIO YA HABARI
  36. Watu wengi wanafikiria kublog kwa ajili ya kupata hela. Je ni nini baadhi ya vidokezo kwa watu wanaofikiria kufanya hivyo? Je, ni ukweli upi wa baadhi ya matarajio yanayohusina na nini kinaweza kufanywa na nini hakiwezi kufanywa wakati wa kublog? Yes blog huleta pesa ila ukiitanguliza pesa kama lengo litaathiri hisia zako za uandishi na kufanya kuaribu utendaji wako kama blogger.

No comments: