Featured Weekly Blogger - Abdallah Hamdun Ibrahim Sulayman

Karibuni katika mahojiano yeu ya kila week. Leo hii tumepata bahati ya kufanya mahojiano yetu na mwanablogger Abdallah Hamdun Ibrahim Sulayman ambaye ana miliki blog tatu....Ya kwanza ni Tanzania Football Event, Mashabiki wa Azam FC na Aboodmsuni Home. Karibu sana hapa na tunafurahi kufanya mahojiano nawe. Hebu tueleze kidogo kuhusu wewe na blogs zako?Jina langu la kwenye vyeti ni Abdallah Hamdun Ibrahim Sulayman, najulikana zaidi kwa majina ya Abood na Msuni. Ninaendesha blog 3, ambapo kila moja inashughuli zake, kuna ile inayozungumzia soka la Tanzania, nyingine inajumuisha mambo mbalimbali, huku ya tatu ikiwa ni ya mashabiki wa Azam FC. Mie ni mwanafunzi wa College, hivyo ni na blog kama kitu cha ziada.

Je ni mda ganiumekua ukiblog?
Nina miezi 7 toka nianze kublog.

Nini changamoto unazozipata kwa kuwa na blog?
Mara nyingi huwa katika harakati za masomo. Huwa najaribu kutoa mawazo hayo kwa kuwa ninakuwa katika harakati nyingine muhumu katika maisha.

Unafanya nini iwapo kuna wakati huna la kuandika kwenye blog yako?
Huwa nazunguka katika mitandao ya jamii.

Ni nani wasomaji wa blog zako?
Wasomaji wa blog zangu ni wapenzi wa mpira wa miguu, kwa kuwa sehemu kubwa ya blog hizo zinazungumzia soka.

Huwa unatumia social networking zingine kutangaza blog yako?
Na tumia twitter Id account aboodmsuni21., facebook, friendfeed, my opera na sasa naelekea kwenye my space.

Je ni bora kupata ukweli au uchunguzi wa jambo unalotaka kuliandika kwenye blog yako wewe mwenyewe au kupitia mtu mwingine?
Ni bora kupata ukweli na jambo ambalo sina uhakika nalo huwa naliweka katika Mitaani na Aboodmsuni. Ili msomaji wangu apate kwa ufupi hiyo taarifa kama atataka kuifuatilia aingie kwenye mtaa (chanzo) husika.

Kila mtu ana post anayoipenda au anayoichukia. Je wew ni post ipi unaipenda sana na kwanini?
Post ambayo ninaipenda ni ile ya vibangwa vya ligi kuu.

Je, unaamini comments kwenye blog yako zilizoandikwa kwa urefu sana zinahitaji
kuzawadiwa zaidi kuliko zile zilizoandikwa kwa ufupi tu?
Mie sio mtu kinganganizi, na huwa siingie kwenye mambo ambayo yanaonekana yako nnje ya uwezo wangu. Kama zinaukweli sihovii lolote.

Asante sana kwa kufanya mahojiano haya na sisi na tunakutakia mafanikio meama katika masomo yako na blogs zako

If you or someone you know would be great for our Weekly Blogger Interviews, please email us at Tanzanian Blog Awards and tell us!

2 comments:

Anonymous said...

big up msuni. I really enjoy reading your blogs. Goodluck wit ur studies

Anonymous said...

big up msuni! really like reading ur blogs. gudluck wit ur studies n blogging