Meet Faith Hilary - Our Weekly Featured Blogger

Karibuni sana katika mahojiano yetu ya kila week. Leo tumepata bahati ya kufanya mahojiano  yetu na mwanablogger Faith Hilary wa Candy1's Little World Blog.  

Faith asante sana kwa kukubali kufanya mahojiano haya na sisi na karibu sana.  Je unaweza kutuambia kidogo kuhusu wewe na blog yako?

Naitwa Faith Hilary, jina la utani najulikana kama candy1 na kwa jina hilo ndio nilitunga jina la blog yangu candy1world. Candy1world blog inahusika na mambo makuu manne ambayo ni habari, burudani, fashion na fun ambayo sana ni vitu vya kuchekesha wanavyofanya watu wengine; pia naandika articles tofauti au huongea na kuuliza maswali kwenye video.


Je blog yako unatumia jina lako kamili au unablog kwa kutumia kivuli kingine na watu wanasoma na kuenjoy blog yako lakini hawajui wewe ni nani?
Jina la blog nimelipa nickname yangu kwahiyo mtu ambaye kaniona tu kwenye blog ataniita candy1 ila pia wapo wasomaji wanaonijua kwa jina langu halisi la Faith.

Ni miaka mingapi sasa umekua ukiblog?
Miaka miwili; nilianza tarehe 11/05/2009.

Ni nini kilikufanya uanzishe blog?
Kwanza kabisa ni kutokana na influence ya baba yangu, Charles Hilary ambaye ni mtangazaji. Wanasema mtoto wa nyoka ni nyoka lakini nilifanya uamuzi wa kutochukua journalism as a career, kwahiyo nikaamua kuanzisha blog ili niwe kwenye tasnia hii kwa njia moja au nyingine japo sio kwa malipo.

Nilikuwa nikitembelea blogs nyingi kabla sijafungua ya kwangu kwa muda mrefu na pia wakati natembelea blogs za watu wengine, sikufikiria kabisa kama ningepata wazo la kuanzisha yangu mwenyewe. Siku nikakaa nikafikiria kwamba unakuta habari moja, bloggers tofauti wameiweka. Mwingine ataripoti kama ilivyo au ku-copy na paste basi anapublish. Nilihisi kwamba kuna kitu hakitoshelezi nacho ni mtazamo wa blogger huyo kuhusu habari hiyo. Baada ya hapo nikaona nifungue blog yangu ambayo habari unaweza kuiona blog nyingine lakini ukisoma kwa undani zaidi, utakuta nilivyoandika mimi ni tofauti kwasababu napenda kuweka mtazamo na maoni yangu.

Je, wewe kazi yako ni kublog tu au hii ni kama kazi ya muda tu au hobby?
Ni hobby tu na nina enjoy ku-blog. Sijafikiria kama nataka iniletee kipato.

Ni nani wasomaji wa blog yako?
Watu tofauti sana na inategemea na post yenyewe kwamba nikiweka post kuhusu viatu vya Christian Louboutin basi ni wadada watachangia ama nikiweka post mara moja moja kuhusu siasa basi atakayechangia ni mtu tofauti.

Je unatumia mitandao mingine kama Twitter au Facebook kuitangza blog yako? Kama unazo unaweza kutuambia ili wasiofahamu waweze kufahamu na kukufuata?
Kwa sasa nina account ya twitter unaweza kunifollow kwa candy1world.

Ni jinsi gani (mtu) anaweza kuelezea style/theme ya yako unavyo blog?
Mtu anaweza kusema style yangu ya ku-blog iko informal na personal. Feedback ninazopata, watu wengine wanapenda vile ninavyoandika kwa kuchanganya Kiswahili na Kiingereza lakini pia nimekuwa nikikosolewa kwa style hiyo. Ninavyoona mimi ni kwamba nathamini lugha niliyozaliwa nayo na pia nataka ujumbe umfikie yeyote ambaye haelewi Kiswahili.

Je ni bloggers wapi ambao wewe unawaangalia na kufuata nyayo zao? Na kwanini?
Sifuatilii nyayo za bloggers wengine yeyote kwasababu muelekeo ni wa kwangu mwenyewe. Japo nasema hivyo lakini wapo bloggers ambao wanipa support na ushari. Siwezi kuwataja wote lakini yupo kaka Mubelwa wa Changamoto Yetu, Evarist Chahali wa Kulikoni Ughaibuni, Mtotosix kutoka Mtotosix., dada Sarah wa Angalia Bongo, Emu-Three wa Diary Yangu na wengine wengi. Ambaye sijamtaja utanisamehe lakini nathamini sana support yako.

Je kuna thamani kujibu comment iliyoachwa kwenye blog yako wakati ukijua kuwa huyo aliyeiandika labda hatarudi kusoma jibu lake tena?
Nikiona comment ya mtu, swali la kwanza najiuliza ni kwamba je atarudi kuangalia nilichojibu? So kwangu mimi, msomaji akirejea au asirejee kwenye kile alichochangia mwanzo, nitajibu kuonyesha ninajali mtazamo wake. Sio lazima msomaji yule yule ndiye atakayerudi kusoma comments, wapo wengine kwahiyo napenda kuonyesha kwamba ninawajali wasomaji wangu wote.

Ni nini baadhi ya malengo yako ya mwaka huu kwa ajili ya blogu yako au unaonaje mwenyewe kwa kipindi cha mwaka mmoja ua mitano toka sasa hivi blog ya itakuaje?
Natumai blogu yangu itaendelea vyema japo ninategemea kuzongwa na majukumu na masomo na vitu vingine lakini I hope nitaweza kuendelea kwa sababu toka nimeanza, roho hunisuta nikiiacha blog bila ku-update au hata kuandika kitu kwa zaidi ya masaa 24. Pia nina malengo ya kuipromote zaidi na pia kununua domain ya candy1world. Watch the space.

Je upi ujumbe wako kwa wale watu wanaotaka kuanza kublog?
Nawahamasisha vijana kuingia kwenye tasnia hii ya habari kwa mfumo wa blogging kwamba usiogope, kuwa huru lakini pia ujue unafanya nini ili usipoteze muelekeo kwa kile unachotaka kiwafikie watu.

Asante.

Asante sana Faith kwa kuchukua muda wako na kufanya mahojiano haya na sisi. Tunakutakia mafanikio tele katika blog yako na pia katika masomo yako.  

If you or someone you know would be great for our Weekly Blogger Interviews, please email us at Tanzanian Blog Awards and tell us!

3 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Cool.
Great job people. Natumai wengi wataweza kusoma na kusomwa na kuitangaza kazi njema ya blog.
PamoJAH

emuthree said...

Kwanza kabisa tunakushukuru mwenye blog kwa kuwajali wengine umekuwa kama muunganishi, na msaidizi wa kuzitangaza blogs.SHUKURANI SANA Candy tunakukubali sama maana unatupa vitu adimu toka majuu .Tupo pamojaKwanza kabisa tunakushukuru mwenye blog kwa kuwajali wengine umekuwa kama muunganishi, na msaidizi wa kuzitangaza blogs.SHUKURANI SANA Candy tunakukubali sama maana unatupa vitu adimu toka majuu .Tupo pamoja

Anonymous said...

Lovely blog! I am loving it!! Will be back later to read some more. I am taking your feeds also.