Mwana Blogger Wa Week Hii Ni Sarah Crystal

Week hii tumepata bahati ya kufanya mahojiano yetu ya kila week na mwanablogger Sarah Cristal wa Agalia Bongo. Sarah ana blog yake inayokuja juu na tulifurahi sana kufanya mahojiano haya na sisi.Sarah karibu sana na tunashukuru sana kwa kukubali kufanya mahojiano na sisi. Unaweza kutuambia kidogo kuhusu wewe na blog yako?


Well Jina langu kamili ni Sarah Crystal, nimezaliwa miaka ya themanini, sipendi kuweka umri wangu wazi as Marlyn Monroe anakwambia "A True lady never tell her age"so ningependa kuweka umri wangu siri...Nimezaliwa jijini Dar-Es-Salaam,familia ya watoto wawili and I’m the last born. Spiritual, sijaolewa ila nipo kwenye mahusiano...Nimesoma elimu yangu ya Primary Mjini Dar na baadaye sekondari mkoani Kilimanjaro na baada ya kufaulu nikachaguliwa mkoani Dodoma kwa kidato cha tano na sita ambapo nilihitimu mwaka 2007..

Baada ya hapo nilijiunga na DSJ at the same time nikaweza kupata kazi gazeti la Mwananchi as entertainment writer. Hiyo ilikuwa mwaka 2007..so nilianza kazi Mwananchi na it was a success as nilikuwa napenda kuandika tokea nipo mdogo so kazi niliiweza vizuri..

Nilipata bosi mzuri ambaye to me alikuwa kama dada, rafiki,ndugu Asmah Makau ambaye naweza kusema ni mojawapo ya mafanikio yangu mpaka hapa nilipo kwasababu through her niliweza kujuana na watu mbalimbali ambao walinipa deals and Yes amenisaidia kwa mambo mengi ...The same year nilianza kublog and I started with angaliabongo.blogspot.com na rafiki yangu mkubwa Suka (naye ni mtu muhimu sana kwangu) ndiye aliye-come up with the name AngaliaBongo na iliendelea hivyo mpaka mmoja wa rafiki yangu ambaye ni mmiliki wa mtandao mkubwa nchini Tanzania aliamua kunipa ofa ya kunipa server na mimi niweze kumiliki website so ever since blog name ilichange na kuitwa angaliabongo.co.tz...ambapo mwaka 2010 niliamua kubadilisha server kwa msaada mkubwa wa binamu yangu Henry alinibadilishia kwa mara ya pili from co.tz to www.angalia-bongo.com na I can tell hapa ndipo nilipokuwa nataka kufika siku zote...special thanks to him.

Ni miaka mingapi sasa umekua ukiblog?
Miaka mitano sasa tokea nimeanza kublog, watu waelewe kuwa angalia-bongo.com sio team ya watu, ni kazi ya mtu mmoja..Nafanya kila kitu mwenyewe ila kwenye mambo ya ufundi ndio my cousin ananisaidia sana and so proud to have him..

Je, wewe kazi yako ni kublog tu au hii ni kama kazi ya muda tu au hobby?
Kuna mambo mengine nafanya ukiachana na kublog, naweza kusema huwezi kuepuka kula lunch so blogging to me ni moja kati ya maisha yangu, siwezi kuacha in any way, kuna kipindi nakuwa bussy sana mpaka nashindwa kuweka kitu hapo unakuta kabisa roho inaniuma as sijaweza kuweka chochote kwenye blog,, mind you I’m a writer and I love wriiting..

Ni nani wasomaji wa blog yako?
Mhh nafikiri mtu yeyote anaweza kuwa msomaji wangu but nagusa hasa vijana..Sina mikakati rasmi zaidi ya kuwa na my own style of writing na pia kujua nini wasomaji wangu wanataka...Like huwezi kuta naandika kuhusu politics unless kitu kimetokea kimekuwa talk of town na kind of intresting then hapo naweza sema lemi write something but siku zote nasimama na kile ambacho nimezoea kuwapa wasomaji wa Angalia-bongo.

Je unatumia mitandao mingine kama Twitter au Facebook kuitangza blog yako? Kama unazo unaweza kutuambia ili wasiofahamu waweze kufahamu na kukufuata?
I’m a twitterholic, mafans wa blog yangu wanaweza kupata updates kupitia @angaliabongo, that's my twitter username na facebook wataipata kupitia www.facebook.com/angalia.bongo

Je ni bloggers wapi ambao wewe unawaangalia na kufuata nyayo zao? Na kwanini?
Kuhusu kufuata nyayo za blogger yeyote nchini Tanzania nitakujbu NO, kwasababu sifuati nyayo ya blogger yeyote cause I do write what I feel like. Hey, I wanna write about this, nafikiri naweza sema napenda na nakuwa inspired by kazi zangu mwenyewe. Don't get me wrong, I'm not selfish..

Je, umewahi kufikiria kuacha kupost comment ambayo iko negative kwako na ukijua hamna mtu atakayejua?
Yah sijisikii vizuri ku-trash comments zilizonitusi unless ziwe kwenye harsh words hapo nazitrash ila Angalia-Bongo ni uwanja huru so huwa sibani comments kwamfano Nakuta comments nyingi ambazo unakuta baadhi zinanitusi,watu tu na chuki zao so comments kama hizo huwa naziachia ili waweze kujua kuwa Im strong enough na matusi yao siyaweki kichwani kwenye maisha yangu ya kawaida.

Je wewe ni mtu ambaye uko rahisi kukata tamaa?
Well kwakweli mimi ni mmoja ya wale Die-Hard people cause sipendi sana kuzungumzia kuhusu maisha yangu but I can tell have been through a lot kwenye maisha yangu na kama sio ubishi wa kusema NO,I Can reach pale ambapo nataka kufika basi leo nisingekuwa hapa..Binadamu unahitaji kutokata tamaa.


Je upi ujumbe wako kwa wale watu wanaotaka kuanza kublog?
Ujumbe wangu mkubwa kwa yule anayetaka kuanza kublog ni kuwa awe na nia thubuti na ajue analenga kwenye kitu gani,ili wasomaji wake wajue tunaingia blog ya fulani tunajua tutakuta nini na sio leo upo kwenye siasa, kesho kwenye udaku, blah blah so ujue na uweke nia thubuti ya blog yako. Mfano mkubwani huyu mwenye blog ya mtotosix, kijana huyu anapenda kukosolewa na kusikiliza mablogers wengine wanaongelea nini blog yake...Na anafanyia kazi maoni na nafikiri akiendelea hivi atafika mbali...

Ujumbe kwa wote ni kumpenda Mungu na kuamini hakuna jambo ambalo Mungu hawezi kufanya,jisaidie nawe utasaidiwa and remember motivation and inspiration is the key to success so live your dreams and get money! GODs Love-Sarah!

Tunashukuru sana Sara kwa kufanya mahojiano haya na sisi. Pia sis hapa tunakutakia baraka tele katika blog yako. 

If you or someone you know would be great for our Weekly Blogger Interviews, please email us at Tanzanian Blog Awards and tell us!

3 comments:

Abdallah Majid Nassor said...

majibu mazuri

meems said...

safiii umejibu vizuri sana

jigambe said...

mwendelezo mzuri!