Unaweza
kutuambia kidogo kuhusu wewe na blog yako?
Mimi naitwa Augustino Chengula niliyehitimu shahada ya kwanza ya Tiba
Mifugo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Morogoro mwaka 2007. Blog
yangu inaitwa “SEKTA YA MIFUGO TANZANIA” inayobeba jina linaloendana na kile
kinachowasilishwa katika blogu hiyo. Lengo kubwa la blog ni kuelimisha umma na
wafugaji juu ya ufugaji na namna ya kukabiliana na magonjwa ya mifugo.
Je,
wewe kazi yako ni kublog tu au hii ni kama kazi ya muda tu au hobby?
Kublog si kazi yangu ila ni hobby tu na lengo langu kubwa ni kuelimisha
umma na hasa wafugaji juu ya mifugo na ufugaji na mambo yanayoendana na hayo.
Hivyo naelimisha umma kwa kupitia fani yangu ya mifugo.
Jinsi
gani unaanza kublog na kwa nini?
Kabla hata ya kuanzisha blog nilikuwa najaribu
kutengeneza tovuti yangu kwa kupiatia zile za bure. Baadaye nikaona kwa
kuchelewa watu wanablog na mwanzo sikujua kama ni za bure. Nilipojua kuwa ni za
bure nikaanza kujifunza mwenyewe namna ya kufungua blog, nikafanikiwa. Nikawa
naendelea kuiboresha taratibu kwa kuangalia blog za watu wengine zipoje. Wakati
mwingine nilitumia Jamii forum kuuliza kama nataka kufanya kitu fulani kwenye
blogu inakuwaje. Sikuwa na elimu ya web designing lakini nilijua kutumia vitu
vya kawaida katika computer. Kupenda kujifunza vitu mwenyewe vilinisaidia.
Lengo kubwa la kuanzisha ni kutaka kuwagawia elimu ya ufugaji watu wengiene
kwani niliona wanahangaika kuitafuta hasa katika lugha ya kiswahili kwani mambo
mengi yapo kwa lugha ya Kiingereza.
Nini
changamoto unazozipata kwa kuwa na blog?
Changamoto ni muda kwani watu wengi wanahitaji
elimu hii ya ufugaji na wengine wanahitaji kujua vitu vingi sana. Kwa kuwa ni
kazi nyingine mara kadhaa nakosa muda wa kuweka elimu mpya kwenye blogu kila
siku. Nahitaji watu wa kunisaidia hasa kuchukua matukio huko mifugo iliko na
kuwajulisha watu wengine. Lakini pia kuandaa mafundisho ya ufugaji yanahitaji
muda na utulivu hivyo kushindwa kuweka kwenye blogu kila siku.
Nakuwa na majukumu mengine ya kikazi
Ni
mara ngapi unafikiri juu ya blog yako wakati uko mbali na kompyuta?
Mara nyingi sana kwani natamani watu waipate elimu
ya ufugaji kwa wingi iwezekanavyo
Ni
nani wasomaji wa blog yako?
Ni watu wote wanaofuga, wasiofuga na wanaopenda kuingia katika fani ya
ufugaji. Elimu hii inawasaidia pia wasiofuga kwani kuna magonjwa yanayoweza
wapata kutoka na kula nyama ya mifugo au mazao yake au wanaweza kuambukizwa
hata bila ya kuwa na mifugo.
Je
ni mitandao gani mingine ambayo unatumi ili iweze kukusaidia kuitangaza blog
yako ili iwafikie wasomaji walengwa wa blog yako?
Mitandao ninayotumia ni: Facebook (nina facebook
page inayoitwa Sekta ya Mifugo Tanzania), twitter, Jamii forum na google na
yahoo groups.
Nini
hasa ni changamoto kubwa wakati unatengeneza posy ya kuweka kwenye blog yako na
kwanini?
Uwekaji wa post kwangu hauna changamoto yeyote
Unafanya
nini iwapo kuna wakati huna la kuandika kwenye blog yako?
Siwezi kukosa la kuandika kulinga na sekta
ilivyopana na ina mambo mengi ambayo wafuatiaji wanataka kuyajua. Tatizo ni
muda tu.
Je
ni nini mkakati wako na blog yako kwa ujumla?
Mkakati wangu ni kuendelea kuiboresha na kuweka post za kuelimisha mara
nyingi iwezzekanavyo. Na nikipata watu wa kunisaidi hasa huko mifugo iliko
wenye nia ya kuelimisha watu bila kujali pesa itanisaidia sana kuifanya blog
yangu ikue na kupendwa na watu wengi zaidi.
Je
ni bora kupata ukweli au uchunguzi wa jambo unalotaka kuliandika kwenye blog
yako wewe mwenyewe au kupitia mtu mwingine?
Kupata ukweli ni muhimu sana si lazima utoke kwako
mwenyewe bali kwa mtu unayemuamini kuwa ni mkweli.
Ni
jambo gani bora blogger anaweza kutoa kwa wasomaji wake?
Japo
bora ni lile lenye msaada kwa msomaji na si uongo, uzushi au jambo lenye
kugombanisha. Linapaswa liwe na manufaa kwa musomaji na si hasara.
Ni
jinsi gani (mtu) anaweza kuelezea style ya yako unavyo blog?
Style
yangu ya kublog siku zote ni kutoa elimu kwa umma bure
Ni
nini imekuwa mkakati wako kwa ajili ya kujenga kujulikana kwa mwenyewe na blog
yako?
Kwa sasa ni kutumia mitandao ya kijamii
Je
ni bloggers wapi ambao wewe unawaangalia na kufuata nyayo zao? Na kwanini?
Issa Michuzi hasa namna anavyotafuta habari kwa wingi, anavyoboresha
blog yake na ulinzi aliouweka kwenye blog yake. Natamani name niiboreshe blog
yangu lakini najua inahitaji pesa ili utumie wataalamu waweze kuiweka katika
muonekano unaoutaka. Kwa sasa bado siajfikia pale ninapotaka angalau nifike.
Hebu
tuambie ni watu gani umewahi kukutana nao wakati ukisughulikia post za kuweka
kwenye blog yako?
Mara nyingi nakutana na wafugaji
Je
unafikiria kuwa unadaiwa na mtu akiyeacha comment/s kwenye blog yako?
Sidaiwi
Je
kunadhamani kujibu comment iliyoachwa kwenye blog yako wakati ukijua kuwa huyo
aliyeiandika labda hatarudi kusoma jibu lake tena?
Thamani ipo, hata kama hatarudi itawasaidia
wafuatiliaji wengine na huenda kuna wengine wanaweza kuwa na maswali kama yake.
Je,
umewahi kufikiria kuacha kupost comment ambayo iko negative kwako na ukijua
hamna mtu atakayejua?
Zijawahi
Je
unazitreat tofauti au unafikiri watu wanaoacha comment kwenye blog yako na
kuacha majina yao yaonekane wazi wanastaili comments zao kujibiwa au hata
kuacknowledge kuwa umeona maoni yao?
Comment zozote zina maana sana hivyo ni muhimu
kuzijibu kulingana na zinavyotaka ujibu. Hazipo kwa bahati mbaya, ila majibu
yawe na busara ndani yake. Pia comment iwe ya kimaadili isikiwuke maadili ya
Kitanzania
Je,
unafikiria ni makosa kucomment kwenye blog yako kwa kutumia jina lingine?
Si makosa, ilimradi tu comment iwe na maadili kama
si ya kimaadili au haiendani mambo yaliyo kwenye blog haifai.
Je
unazichukulia comments zote sawa unazotumiwa kwenye blog yako bila kujali maoni
uliachwa?
Kama zina
mlengo wa blogu yangu, zote nazipa uzito sawa
Je,
unaamini comments kwenye blog yako zilizoandikwa kwa urefu sana zinahitaji
kuzawadiwa zaidi kuliko zile zilizoandikwa kwa ufupi tu?
Hapana hapa swala si ufupi au urefu wa comment bali
ni uzito wa ujumbe ulioko kwenye comment
Je
wewe ni mtu ambaye uko rahisi kukata tamaa?
Si kati tamaa kirahisi kwani unapokaribia kukata
tamaa ndipo mafanikio huanzia. Hivyo naongeza bidii ninapokaribia kukata tamaa
Je
unaedit picha zako ili ziwavutie sana wasomaji?
Si kila picha kwani muda kwangu ni tatizo hivyo si
zote huwa naziedit
Je
unaepuka kuweka post ambazo ziko very controversy kwasababu ya kuogopa watu
hawatakubaliana na wewe au huna hizo post?
Sina hizo post
Je unajisikia
vizuri zaidi ukiweka post kwenye blog yako na ukapata maoni ya watu zaidi ya 20
au ukipata maoni ya mtu mmoja mashuhuri tu.
Maoni ya wengi ndiyo ninayo yapenda kwani
yananijenga na kunipa mwanga
Je
unasema blog yako kuwa inamafanikio iwapo unapata watu wengi wa
kusoma au unapata watu wengi wakuacha comment kwenye blog yako?
Mafanikio ya blog yangu ni pale watu wengi wanapo itembelea na kuisoma,
na wanapoacha comment wengi ni ishara kuwa wengi wameisoma na kupata ujumbe
husika.
Je
blog yako unatumia jina lako kamili au unablog kwa kutumia kivuli kingine na
watu wanasoma na kuenjoy blog yako lakini hawajui wewe ni nani?
Blogu inatumia jina la kile
ninachoelimisha, address ya blog imebeba jina langu na chini ya blog kuna jina
langu halisi na kazi yangu ninayofanya. Hivyo wasomaji wa blog wanajua ni blog
ya nani.
Ni
nini baadhi ya malengo yako ya mwaka huu kwa ajili ya blogu yako au unaonaje
mwenyeew kwa kipindi cha mwaka mmoja ua mitano toka sasa hivi blog ya itakuaje?
Malengo yangu ni kuitangaza
zaidi watu wengi waijue kwani naamini wapo wengi wanaopenda kupata elimu hii
kwa kiswahili, lakini bado hawajafanikiwa kuijua. Pia ndani ya miaka mitano
ijayo naamini nitakuwa na watu huko kwa wafugaji watakao nisaidia kukusanya
habari za mifugo na ufugaji ili tuwasambazie watu wengine.
Lazima waanze na malengo ya kwa nini wanataka
kublog, na wasilenge pesa walenge kutoa habari au kuelimisha na wawe na nia
hiyo ya dhati. Wakilenga pesa wasipopata wataishia kukata tamaa.
Je
kwa maoni yako ni lengo gani kubwa kwa mwanablogger?
Lengo kubwa ni kutoa habari na kuelimisha
Watu
wengi wanafikiria kublog kwa ajili ya kupata hela. Je ni nini baadhi ya
vidokezo kwa watu wanaofikiria kufanya hivyo? Je, ni ukweli upi wa baadhi ya
matarajio yanayohusina na nini kinaweza kufanywa na nini hakiwezi kufanywa
wakati wa kublog?
Akiwa na malengo ya kupata hela inabidi awe
amejipanga sana, kwa maana hiyo itakuwa kazi ya kujiajiri na itategemea sana
jitihada zako. Vinginevyo utaishia kukata tamaa, huwezi kuanza leo kublog
halafu kesho utegemee kupata pesa. Kazi si kuanzisha blog, kazi ni kuitangaza
na kuwavutia watu wengi kuitembelea.
No comments:
Post a Comment