Mahojiano na mwana blogger wa wiki - Amani Masue

Wiki hii tumepata bahati ya kufanya mahojiano yetu ya kila wiki na mwana blogger kutoka blog ya Amani Masue. Asante sana kwa kufanya mahojiano haya na sisi. Hebu tueleze kuhusu wewe na blog yako. Kwa jina natambulika kama Amani Masue pia ndo jina la blog yangu ni blog yenye aina nyingi za habari zikiwemo za kitaifa na kimataifa katika nyanja mbalimbali michezo,siasa,burudani n.k.
Je, wewe kazi yako ni kublog tu au hii ni kama kazi ya muda tu au hobby?
Kazi yangu sio kublog hii ni hobby tuu kuwa blog na naipenda sana kwani ninakua face to face na kila aina ya habari kila siku.
Nini changamoto unazozipata kwa kuwa na blog?
Nimepata changamoto ya kutafuta habari za kila siku,kujua leo kuna nini na kesho kutakua na nini pia japo muda wa kuhabarisha uko limited basi muda unaopatikana unatumika ipasavyo katika kupost habari.
Ni miaka mingapi sasa umekua ukiblog?
Huu ni mwaka wa nne sasa.
Ni nani wasomaji wa blog yako?
Wasomaji wa blog hii ni watu wote wanaopenda kutafuta habari za nyumbani na nyinginezo.
Ni nini imekuwa mkakati wako kwa ajili ya kujenga kujulikana kwa mwenyewe na blog yako?
Ni kuleta mapinduzi makubwa kupitia tasnia hii ya blog, pia kuhakikisha inajulikana na kupata wasomaji wengi ndani na nje ya nchi kama blog nyingine zinavyojulikana nchini.
Je unazitreat tofauti au unafikiri watu wanaoacha comment kwenye blog yako na kuacha majina yao yaonekane wazi wanastaili comments zao kujibiwa au hata kuacknowledge kuwa umeona maoni yao?
Sio lazima kama mtu anahitaji mwangaza zaidi wa jambo flani atajibiwa.
Je blog yako unatumia jina lako kamili au unablog kwa kutumia kivuli kingine na watu wanasoma na kuenjoy blog yako lakini hawajui wewe ni nani?
Natumia jina kamili.
Ni nini baadhi ya malengo yako ya mwaka huu kwa ajili ya blogu yako au unaonaje mwenyewe kwa kipindi cha mwaka mmoja ua mitano toka sasa hivi blog ya itakuaje?
Itakuna na habari zaidi mwonekano mpya na itakua na wasomaji wengi zaidi.
Asante sana kwa mahojano haya na sisi na tunakutakia mafanikio mema katika blog yako.
If you or someone you know would be great for our Weekly Blogger Interview, please tanzanianblogawards@gmail.com and tell us!

1 comment:

Anonymous said...

http://kilinyepesi.blogspot.com/