Featured Blog - Suleyman Omary

Mimi naitwa Suleyman Omary lakini ni maarufu kwa jina kbornz au Sme ni mkazi wa Dar es Salaam, ni miliki wa blog ya Kbornz Blog

Nimekua blogger kwa muda wa mwaka 1 sasa ila niliifungua hii blog mwaka 2007, nikaachana nayo sababu nilikuwa sina muda na access ya internet kwa ajili ya kuupdate habari kila siku. Kiukweli nilivutiwa kuanza blogging baada ya kumuona Mjengwa kipinde kile anakuja ofisini kwetu pale kinondoni Cavalli internet so nikaamua na mimi nijaribu. Nilivyojaribu sikukaa muda nikaachana nayo, sasa nimerudi kwa nguvu mpya kabisa.
Ili kufanya blog yangu ijulikane zaidi, natumia mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter na mtandao wa Google plus. Mikakati niliyonayo kwa ajili ya blog ni kupata wasomaji wengi zaidi na blog yangu kuwa miongoni mwa blog maarufu hapa Tanzania na pia nje ya Tanzania.

Hata kama sina picha za matukio husika hua natafuta picha za wahusika kupitia mitandao mingine ili kufanya post ziwe na mvuto zaidi. Ninachoamini ni kwamba, picha zinahabarisha zaidi ya maneno, na zinaleta mvuto kwa msomaji pia kuendelea kusoma na kumfanya arudi tena kwa siku zingine.


Tanzanian Blog Awards inakutakia mfanikio mema katika blog yako. Tafadhali tembelea blog yake kwa support na maoni. www.kbornz.blogspot.com

No comments: