Tunapokea maoni

Tunafahamu kuwa watu wengi wanaingia kwenye hii site wakati wa mashindano. Hivyo tunaomba maoni yenu. Tumeshaongea na two different groups weekend hii ambao wote walikua wanaulizia kuhusu shindano hili kwa ujumla wakiwa na nia ya kudhamini.. Mwaka jana tulikataa wadhamini kabisa lakini kutokana na maoni ya watu tunafikiria mwakani tutaruhusu watu wadhamini shindano hili. Hivyo tunaomba maoni yenu ili kujua jinsi ya kuboresha shindano hili...

Maoni haya ni kwa ajili ya kuboresha shindano hili. Hatutaweka majina ya watu lakini tutapenda kuyapost ili watu waangalie na kujadili kama wana la kuengeza waengeze..

Maoni hayo tunaomba kutokakwa magroup haya
a) Bloggers - tafadhali kama hutaki jina lako liwekwe hewani tueleze. 
b). Kutoka kwa watu wasio na blogs. Pia hatutaweka jina lako kama hutaki..

Pia tunatafuta watu watakaopenda kuvolunteer kwa mwaka kesho..Hii ni strictly volunteering. Hatujajua wadhamini tutapata wanagapi na kama tutaweza kuwalipa watu hao temporary kwa muda wao. Kama tutaweza basi tutajua huko mbele tukishakamilisha kupata wadhamini hao lakini sasa hivi ukitutumia contact zako ujue ni pure volunteering. Na ukituma tunaomba utwambie wewe unapenda kusoma blogs zipi au una ujuzi kwenye mambo gani, ili tujue kuwa utatusaidia katika blogs za categories zipi. na watu hawa nadhani uwe na blog au usiwe nayo it is okay kwasababu kuna mambo yanahitajihata bloggers kufanya lakini ikifika wakati wa kuchagua nominees basi hao watu wasiwe na blog..email ni tanzanianblogawards@gmail.com

Shukrani..

3 comments:

emu-three said...

Maoni yangu yanaangukia kwenye vipengele vya blog ipi uiweke mahali gani,

Mimi nionavyo blog nyingi huandika mambo tofauti tofauti, licha ya kuwa imeandikwa labda blog ya urembo, au blog ya michezo,lakini kila mtu anajaribu kuweka kila kitu.

Labda hivi vipengele tungejaribu kuviweka vyema, ili angalau mtu akisema blogyangu ipo kwenye kipengele hiki iwe imekidhi haja.

Na utamaduni wetu unaotuwakilihsa sote kama Tanzania, ni lugha ya Kiswahili , ni vyema nyie mliopo huko nje mkakitangaza kwa kila hali, sijui labda ni kutokana na mitandao yenyewe kuwa imejengwa kitofauti na Kiswahili.

Kwa maoni yangu hata haya makundi yaandike tu kwa Kiswahili, mfano;

1.Blog za uandishi wa hadithi na visa

2Blog za michezo na burudani

3. Blog za habari na matukio

4. Blog za urembo na warembo
5 Blog za miziki na utamaduni.

6. Blog za dini na imani

7 Blog za vichekesh na katuni

Na vitu kama hivyo.

Ni hayo tu kwa leo

FESTUS KAHAYA said...

hivi mbona kuna blogu nyingine hamzijui. hamwoni kwamba imefikia wakati kuwahamasisha wenye blogu nao wajiandikishe kwnu ili mwafahamu

MfumuTzeNation said...

mimi kama mimi ,nilikua sifahamu kama kuna mashindano kama haya, hivyo basi nimejaribu kufatilia kwa umakini kila kipengele na washiriki nimeona wote wapo sahihi,na wadeserve kule walipo pangwa...hivyo basi kama mimi pia ni Upcoming blogger naejitegemea ,pia na mwenye umri mdogo napenda kutoa maoni yangu kua msitusahau na sisi tunaoanza katika industry hii ya Tanzania blog, mnaweza kuicheki kwa kuitafakari blog yangu kwani imeBase katika habari za entertainment zinazohusu hapa kwetu na pia nje ya nchi... me binafsi ni graphics designer,,,asante
BLOG YANGU ni www.mfumunation.blogspot.com na pia nimeDesign na kuipanga kimuonekano blog hii www.liberatus-apparels.blogspot.com ....
SHUKURANI NA NATUMAI HAMTATUSAHAU TULIOPO CHINI...