Mwaka Huu Ndio Mwisho Wa Shindano Letu

Kama nilivyoandika katika post ya nyuma kuwa mwaka huu ndio mwisho wa shindano hili kusimamiwa na mimi. Kuna mtu (watu) waliniandikia na kuonyesha nia ya kutaka kuchukua shindano hili na kulifanya (For Profit) ili waweze kutoa zawadi kwa washindani na kufanya sherehe za kukabidhi vyeti hivyo katika sehemu maalumu watakayochagua wao ila sijajua kama watafanya hivyo au la. Ila hata kama hawatachukua mpaka mwakani still huu ndio utakua mwisho wa shindano hili. 

Nimeona iwe hivyo kwa vile shindano hili linaongezeka kuwa kubwa sana kila siku. Emails zinazoingia kutaka kujua mambo mbalimbali kwa siku wakati wa mashindano na baada ya mashindano ni nyingi sana sana na mimi nimejikuta nimebakia mwenyewe kusimamia kila kitu hapa. Hivyo kwa muda nilionao na ukizingatia majukumu ya maisha sitaweza kuendeleza kitu kiwe na good quality nikiwa peke yangu.  

Directory List ninafikiria kuiacha ilivyo lakini sikutaka kuwa niwe napokea emails za watu wakitaka kuregister blogs zao kwa vile kwa kufanya hivyo itakuwa ninatakiwa bado kucheck hii email ya blog kila mara. Hivyo nimefikira kutafuta sehemu ambayo watu wataweza kuregister blog zao wenyewe lakini pia blog isipokua active kwa muda fulani iwe inaondoka yenyewe ili kuhakikisha direction list hiyo ni kwa active blogs tu. 

Hivyo baada ya kutuma badges na certificates mwishowa kujibu swali lolote litakalojitokeza ni mwisho wa mwezi wa kumi na moja.

Napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa wote mlioshiriki na kusupport shindano hili toka lilipoanza na kufikia hapa lilipo.  

2 comments:

DarSlam said...

Na Blog ya kuregister ni http://bongoblogs.blogspot.com
Bongo Blogs -Blog ya Taifa

emu-three said...

Tunashukuru sana kwa kazi yako nzuri, lkn bado tulikuwa tunakuhitajia sana, kama `Tanzania Blog Awards' na pili mimi niliomba angalau mwaka huu ungejitahidi kupatikane hata kazawadi kadogo....kwa kumsumbua huyo ALIYEKUWA KAAHIDI, nasema hivi kwa sababu wengi watauwa wamevunjika moyo.
Japokuwa kiukweli zawadi haina maana sana ukilinganisha na huu udugu , wa blog mbali mbali kukutana sehemu moja,(ndani ya TBA) na pili imekuwa ni sehemu muhimu ya kujitangaza, kwani blog nyingi, zimafahamika kwa kupitia njia hii ..TWAKUSHUKURU SANA, na tunakuomba uzidi kuwa nasi mwakani.