Badges Na Certificates Zitatumwa Baada ya Siku ya Mwisho wa Kupokea Maombi

Asante kwa pongezi zenu. Tunawashukuru wote pia walioshiriki katika shindano hili, bila nyie hili shindano lisingeweza kukamilika. Ushirikiano wenu mliotoa ndio maana waliingia watu wengi sana sana kuiga kura. 

Okay, kwa vile ni watu wengi tayari wameandika kuwa wanahitaji badges zao  hata za kushiriki basi tutaamua kusubiri mpaka mwisho wa kukupokea maombi halafu ndio tutatengeneza. Hivyo ukishatuma email yako kuwa unahitaji badge hiyo basi usiandike tena kuhusu badge yako tutakutumia. Tutaanza kuzituma baada ya tarehe 21 October. Kama utakua hujapokea badge yako by November 20 ndio utuandikie.

Unapoandika kuomba badge yako tafadhali tueleze blog yako ni ipi na ilishiriki katika kipengele gani au imeshinda katika kipengele gani ili iwe rahisi kwetu. 

Na wale wanaoemail kuuliza maswali mengine tafadhali pitia kipengele cha maswali na majibu katika blog hii. Maswali yote unayoyauliza yanapatikana hapo. Kilichokua hakipo ni katika post niliyosema kutakua na zawadi za washiriki mwaka huu. Well, baada ya mashindano ya mwaka jana kuna mtu aliwasiliana na mimi na kusema atasaidia hilo lakini hataki jina lake litangazwe. Nilivyowasiliana na yeye mwaka huu sikuweza kupata jibu la YES, nitatoa, Yes, subiri kidogo au NO, sitatoa. Sasa kwa vile muda ulikua umefika niliotangaza kuwa shindano hilo litafayika ikabidi niendelee hivyo hivyo bila kuahirisha na bila kujua kuwa nikiahirisha kweli atatoa zawadi hizo kama alivyoahidi.


Hivyo kama miaka iliyopita vyeti na badge zenu zitatumwa kwa kutumia email.

2 comments:

umar makoo said...

NILIKUWA NASHAURI VYETI VITUMWE KUPITIA SANDUKU LA POSTA KWA WALE AMBAO WANA SANDUKU LA POSTA NA KWA WALE AMABAO HAWANA NDIO UWATUMIE KWA KUTUMIA EMAIL...NA BADGE NDIO VYEMA KUTUMWA KUPITIA NJIA YA BADGE KWA MATUMIZI YAKE NI YA ONLINE LAKINI KWA CHETI VYEMA KIKAWA KWENYE HARD COPY

umar makoo said...

NA KINGINE NLIKUWA NATAKA KUJUA MUAFAKA NA HUYO MDHAMINI AMBAE ALISEMA ATATOA ZAWADI..NDO KUSEMA AMEINGIA MITINI AU UMECHOKA TU KUMFATILIA?