Malalamishi Yaliyojitokeza na Maelekezo ya Tanzanian Blog Awards

Tunashindwa kuelewa malalamishi ni ya nini? Ni vitu gani vinavyowafanya watu waseme "wanayumbishwa?

Kilichobadilika ni vitu hivi vichache na tuliviongelea toka mwisho wa shindano la mwaka jana.
1. Kutumia email kupendekeza washiriki - Tuliamua kufanya hivyo kwa vile kwa kutumia form watu walikua wanaziabuse.Mtu anapendekeza blog moja mara zaidi ya 100 kwa dakika 10. Ilikua inatupotezea muda kuprocess data nyingi wakati 50% zilikua ni fake....

2. Blogger anayependekezwa amekubali kushiriki - Kuandika kuhusu shindano hili ni kwa vile tunataka kujua blogger anayependekezwa ni kweli amekubali kushiriki katika shindano letu...Sisi hapa tupo kwa ajili ya kuwasaidia bloggers wakitanzania kujitangaza sasa kama blogger anayeona hataki kushirikishwa hatutaki kumlazimisha. Sasa kwa kumake easy kwa blogger ambaye anataka kushiriki lakini blog yake post zake haziendani na post ya mambo ya awards basi atuandikie kuwa anataka kushirikkshwa. Blog tunazopokea ni nyingi sana lakini mwisho wa yote tutaweka wale bloggers waliokubali kushirikishwa tu. Tutaweka majina ya blogs zote zilizopendekezwa hapa tarehe 2 Sep 2013. Na Blogger anayetaka kushirikishwa lakini hakuweka post asipotuandikia kuwa anataka kushirikishwa basi tutaondoa blog yake na kuachia wale wanaotaka kushirikshwa waendelee....

3. Tarehe ya mwisho ya kupendekeza majina -  tumeisogeza kuwa tarehe 2 baada ya  watu kusema week mbili ni ndogo sana na ati tukizingatia siku za weekend wengi hawana uwezo wa kutumia simu "kuingia kupendekeza". Hivyo tumeongeza siku mbili ambazo zilikua haziharibu tarehe za kuanza kupiga kura...kura zitaanza zitapokelewa tarehe kama ilizopangwa. 

Na pia kwa wale waliouliza kuwa Jumamosi na jumapili hakuna kupendekea majina? Jibu ni kuwa kama una Internet access unaweza kupendekeza muda wowowte na siku yeyote mpaka tarehe 2 Sep. Sio kuwa ukipendekeza blog yako siku ya jumamosi na jumapili hatutahesabu kura zako. Nominations zitakusanywa tu ila huo muda tuliongeza kuondoa malalaishi ya baadhi ya watu waliosema muda ni mdogo na siku hio za weekend ni kama hazihesabiki.

Sasa watu wakiandika na kusema wanayumbishwa au masharti ni mengi sana ....hatuelewei ni kwa nini..

Mwisho wa yote msije mkaanza kualamika kama mwaka jana kuwa blog fulani zimeachwa au blog zilizopitishwa ni kwa kujuana...Trust me we don't know any blogger in person kiasi cha kumpendekeza na kumpitishia blog yake katika shindno kama hili...C'mon now we are not that low......Hatutaacha blog yeyote kwa makusudi wala nini kwa wale bloggers waliopendekezwa na kuwa wamekubali kushirikishwa ndio watakao shiriki tu...THAT IS ALLL


2 comments:

Anonymous said...

Blogger mwenyewe anaweza kupendekeza blog yake kushiriki au mpaka watu tofauti na yeye wapendekeze?

Admin said...

Yes blogger anaweza kupendekeza blog yake au za bloggers wengine anazozipenda au anazozisoma kila siku...Whatever good things we build end up building us. - Jim Rohn