Vitu vya Kuzingatia Unapopendekeza Blog

1. Kuna walioomba kuwa jumamosi na jumapili zisihesabiwe katika siku za kupendekea blogs kwa vile wengi wanakua hawako kazini au shuleni, hivyo kwa siku hizo nne za weekend tumeadd siku mbili zaidi. Hivyo badala ya tarehe 30 mwisho wa kupokea mapendekezo utakua ni tarehe 2 September. Lakini kura zitaanza kupigwa tarehe iliyopangwa ambayo ni Sep 7th na katika kupiga kura hatutaengeza muda kuwa kupiga kura.

2. Tafadhali unapopendekeza blog weka link ya blog kwenye subject halafu kwenye body ndio unandike vipengele unavyotaka hiyo blog ishirikishwe. Subjects kama "salamu sana", "naomba kushirikishwa", "nawapa pongezi" halafu kwenye body unaweka blog  na kuipendekeza katika vipengele vyake itaishi kupotea. Hatutafungua email ambazo hazina jina la blog kwa kipindi hiki kama una swali wenka kwenye blog hii na tutaweza kuwajibu. Facebook hatuitumii sana hivyo ukiuliza swali huko itachukua muda kujibiwa. Na pia email ipo forwarded kwa watu wanaokusanya hizi nominations na pia wanaosaidia kukusanya hizi nomination hawaongei kiswahili. "We're so sorry about that" lakini ukweli ni kuwa tulijaribu kutafuta watanzania watakaopenda kujitolea kusaidia mambo mbali mbali huku na hakuna waliojitokeza. Hivyo tuliowapata vijana hawa ndio hivyo. Hivyo zingatia hilo emails zote sasa hivi katika kipindi hiki zinaenda kwa vijana hawa watatu na wao ndio wanarecord kila kitu. 

3. Tumeweka email mbili lakini tumia moja unapokua unapendekeza blog. 

4. Ukituma blog yako tuma mara moja kwa siku. Ukituma zaidi kwa wingi kwa kutumia email account hiyo hiyo mwisho wa yote zitaishia kwenda kwenye spam folder.  

5. Mwisho - Pamoja na kupendekea blog zako hakikisha unawaambia hao bloggers kuwa waweke post kuhusu hili shindano na walink kwetu ili tujue kuwa wamekubali kushirikishwa. Mwaka huu tutashirikisha bloggers wale tu wanaotaka kushirikishwa regardless ya blogs zao kuwa na wasomaji wengi au nzuri.
1 comment:

emu-three said...

Tunashukuru kwa haya yote, lkn wengi wetu, yaani wapenzi wa blog hasa waliopo Tanzania, sio wajuvi sana wa mitandao, kwahiyo tunaomba taratibu zisiwe na masharti mengi, kuwapo na njia rahisi ya kufanya. Tulitarajia kutakuwa na fomu, ambayo mtu angelijaza kuwa `mimi napendekeza blog hii iingiwe kwenye kipengele hiki.
Nimejaribu kuwasiliana na wapenzi wangu wa blog, wanasema maelezo ni mengi, na hawana muda wa kuyasoma yote, je wafanyeje..pili wengi wanaona ni kazi ndefu, kwanza wapendekeze pili waje tena kupiga kura..wengi wanasema mpendekezaji alitakiwa kuwa mwenye blog, kuwa kakubali kushiriki, na majaji wanazichuja hizo blog kutokana na masharti yanayohitajika, na kusema hizi zinafaa..ni ile hali ya Watanzania wengi kutokupenda kusoma au kuchukua muda kufahamu ni nini kinahitajika
Ni hayo tu mpendwa