Bloggers Association of Tanzania (BATA) coming soon!

Bloggers Association of Tanzania (BATA) inakuja hivi karibuni. Itakua kwenye website mpya na ndio itakua nyumba mpya ya Tanzania Blog Awards.  Madhumuni ya  BATA ni kusaidia kuwakutanisha wanablogger wote wakitanzania popote pale walipo, kuwasaidia katika mambo mbalimbali yanayouhusu kublog, kutangaza blogs zao, kuwapatia mafunzo mbalimbali online au onsite na pia kuongeza motisha ya quality za blogs zao.

BATA itakua na board members na pia kutaajiriwa mtu maalumu atakayeshugulikia site hiyo kila siku. Hivyo sheria nyingi ni mpya na watu watakaopenda kujiunga na umoja huu watatakiwa kujiunga upya. Blog zitakaguliwa na zitakazofikia kiwango cha kuingia kwenye umoja huu ndio zinatajiunga tu. Kwa miezi 6 kujiunga na umoja huo itakua ni bure baada ya hapo itakua kuna kiingilio. Kama blog yako haitakubaliwa kujiunga utarudishiwa hela zako. Kutakua na mtu atakayesimamia 24/7 site hii. Na pia tutaalika watu mbalimbali kutoa mafuzo kwa bloggers, consulting etc Hivyo bila kuwa na fee hatutaweza kufanya mambo yote hayo.

BATA inataka kuwa watu wakipitia directory list ya blogs za watanzania kwenye umoja huu wajue kuwa wanapata blogs zenye viwango vya juu tu, zenye information za maana na ambazo zipo active. Na pia hii itaongeza changamoto kwa bloggers wengi kujifunza umuhimu wa quality vs quantity.

Tumejitahidi sana kusaidia bloggers wengi wa kitanzania blogs zao nazo zijuilikane lakini tumegundua kuwa marketing less quality blogs sio aibu kwetu sisi tu bai kwa kwa Tanzania kwa ujumla. Watu wengi wanafungua blog tu kwa vile kila mtu ana blog. Wanazituma tuziweke kwenye directory list yetu lakini baada ya muda hawazishughulikii tena na hata kama wanazishughulikia wala hawazingatii ubora wa blog zao wala hawafikirii kuwa wabunifu au unique. Vitu vingi vinakuwa copy and pasted kutoka kwa blogs zingine tu. Kuna wakati ukisoma blog moja au mbili za Tanzania huna haja ya kupitia zingine kabisa kwa sababu vitu ni vile vile vinajirudia kwenye blog zingine. Na pia wengine wanaacha kushughulikia blog zao mpka tena karibu na shindano hii ndio wanaaza tena. Hivyo kwa watakao kubaliwa kujiunga ni wale tu weye blog zenye quality.

BATA wameamua kuwa mfano wa kuonyesha quality na wataanza na directory list yao. Sio kila blog itaingia kwenye directory list tena. Watu watakao taka kujiunga kwanye association hii watatakiwa kujaza form na blog zao zitapitiwa kwa ungalifu na kuhakikisha zimemudu quality ya kuingia. Ni heri kuwa na members watano tu wenye blog zenye quality kuliko kuwa na member 100 na blog zao hazina quality kabisa. Na pia blog ikiwa kwenye list na baadaye kutoshughulikiwa tena itaondolewa na itachukua hadi miezi 12 tena kwa wewe kuruhusiwa kuwa member.  Na pia sio kila blog ya Tanzania itaingia kwenye shindano hata kama ikipendekezwa na watu. Kama mwenye blog sio member wa BATA basi blog yake haitashirikishwa.

Hivyo kuanzia sasa hivi kama unataka kujiunga na umoja huu anza kuzingatia ubora wa blog yako kuliko idadi ya post unazopost kila siku. 

Mimi nitabakia kuwa member wa board lakini majukumu mengi baada ya muda hayatakua yagu tena peke yangu. 

Shukrani

Quality Quality Quality to promote Tanzania

3 comments:

utalii nyumbani said...

Nani amekuteua ua expert wa blog za Tanzania.

Admin said...

Hii ni umoja wa blog za watanzania na sio blog za Tanzania (big difference). Na kama katika kila umoja wowote ni option kujiunga...Quality za blog zitakazoomba na kukubaliwa ni kutokana na std ya board ya umoja huu watazoweka.

Brandbel Company-Tanzania said...

nataka kujiunga blog yangu ni www.kabatinionline.blogspot.com hebu angalia standard coz haijaanza kufanya kazi rasmi