Shindano La Mwaka 2013

Tumekua tukipokea email nyingi kutoka kwa watu mbalimbali wakiulizia kuhusu shindano la mwaka huu. Okay kama unataka maelekezo zaidi ya jinsi ya shindano hili linavyokwenda soma FAQ hapa.

1. Kutokana na maoni ya watu wengi shindano la mwaka huu litakua kwa week moja tu. Nomination zitapokelewa kwa week mbili  za mwisho wa mwezi wa nne na shindano litafanyika week ya kwanza ya mwezi wa tano tu.

2. Kutakua na zawadi mwaka huu katika shindano letu. Waambie wasomaji wa blog yako kama wanataka ujishindie zawadi kushiriki kwao ndio kutakusaidia kushinda. Sponsor wa shindano letu (hataki jina lake litangazwe) atatoa zawadi kwa washindi watatu. Mshindi Wa Kwanza iPad 4.  Mshindi Wa Pili iPad mini Mshindi Wa Tatu iPhone 5. Kama kuna watu au mashirika mengine wangependa kusaidia kusponsor shindano hili usisite kutuandikia. Tutafurahi sana tukiwapa zawadi washindi wa kila kipengele...Hiyo itakua changamoto kubwa sana kwa bloggers wa Kitanzania kuendelea kudumisha ubora wa blog zao.

3. Jinsi ya kupata overall winners ni kuwa yule mtu atakayepokea kura nyingi kuliko wote total katika kipengele anachoshiriki ndio atakua mshindi na sio total ya kura zote katika vipengele vyote anavyoshirikishwa. Kwa mfano ukiwa umependekezwa katika vipengele viwili hatutajumlisha kura zote katika vipengele hivyo zilizopokelewa bali tutachukua kipengele kile tu ambacho umepokea kura nyingi. 

4. Mwaka huu tunafiria kutumia email au twitter handle kupiga kura..Hatujakamilisha uhakika huo lakini kama huna twitter account jitayarishe kuwa nayo. Fungua na follow official twitter handle ya Tanzanian Blog Awards ambayo ni BongoBloggers Muda wa kupiga kura ni mdogo sasa hivi na hatutaki malalamishi. Mara tukijua tutatumia njia ipi kupiga kura basi tutatangaza mara moja na muda ukifika tutapokea nomination kama mwanzo na kupiga kura kwa kutumia njia tutakayoiweka. 

5. Mwaka jana watu wengi walisikitishwa sana tulipoondoa kipengele cha Best Graphic Design Blog. Hivyo mwaka huu tutakirudisha na kukiita Best Design Blog lakini kitakuwapo tu iwapo tutaona kuna blog at least tatu zitakazopendekezwa zinaqualify kuingia katika kipengele hicho. Design means design and not any other way. 

Tafadhali tunaomba kama una swali soma FAQ kwanza kama hujapata jibu ndio utuandikie. 

4 comments:

Dr. Said Said said...

I would love to add my Marketing Blog http://saidsaid.net.

How do I do that?

It's a blog which helps business owners and individuals increase their profits using Cool Marketing Strategies.

emuthree said...

Twashukuru mpendwa na jopo lako, hili linatupa faraja hasa sie ambao blog zetu hazina namna yoyote ya kuiniza pesa, zaidi ya kujitolea tu!

Karen said...

Muda umefika first two weeks of April, nominaton zitaanza lini mh. admini

Panjila Poul said...

Tunangoja tuone kazi zetu kwa jamii wanapokeaje kama Watanzania.