Proud Tanzanian

Kutokana na kuona kuwa hii site inatraffic nyingi sana kwa siku na sisi hapa tupo kwa faida ya watanzania wote bila kujali wapi wanaishi, tumeamua kuwa kwa wale watanzania wote wanaotaka kujitagaza kwa kazi zao (arts, books etc) au biashara zao msisite kututumia. Tutakuwekea hapa bila malipo yeyote. 

Wow! Traffic iliyopo hapa kila siku na hakuna kinachoendelea kwa sasa ni jambo linalotushangaza na kutufurahisha sana. Jambo la busara ni kunyoosha mikono yetu na kuwasaidia watu wengine kujitangaza pia zaidi ya bloggers tu.  Itakua sio jambo la busara na ni uchoyo mkubwa tukiona traffic yote hii na kuachia bila kuwasaidia watu wale wenye kutafuta mahali pa kujitangaza lakini wanashindwa kufanya hivyo kutokana na gharama nyingi za matangazo.  

As usually kama wewe ni blogger usisite kututumia blog yako tukutangazie hapa. Kwa bloggers tumekua tukipokea kila siku bila masharti yeyote. 

Tutapokea matangazo kwa wafanya biashara wadogo na sio makampuni. Hatutapokea matangazo ya bar, night clubs au club nights parties.

1 comment:

emu-three said...

Nashukuru sana mpendwa, kwani wengine tuna blogs, tunaandika stories lakini jinsi gani ya kutengeneza kitabu inakuwa shida....