Kuwekwa Kwenye Award List

Mara kwa mara tunapokea emails kutoka kwa bloggers mbali mbali, baadhi yao ni wapya na wengine sio wapya lakini labda walikua hawaajui chochote kuhusu hili shindano. Wote wanaomba kuweka majina yao katika award list. Tunataka kuwaambia wote kuwa ili jina lako na la blog yako liwekwe kwenye award list ni lazima uwe umeshiriki kwenye shindano hili. Tafadhali soma About Us kama wewe ni mwanablogger mpya au sio mpya lakini ulikua hufahamu chochote kuhusu shindano hili na unataka kushiriki hapo mwakani.  Blog hizo hapo kwenye list zilishiriki katika shindano na kushinda. Kama blog yako itashinda basi itawekwa kwenye award list hapo kutakapofanyika shindano lingine.

Kuhusu blog directory list - blog zote tutaziweka kwenye directory list, hiyo haina kigezo chochote. Hivyo kama unaona blog yako ilishiriki katika shindano la mwaka huu au la lakini hatujaiweka kwenye directory list usiwe na shaka. Tutaziweka blog zote wakati tunaupdate directory list yetu. Kila miezi sita tunaondoa blog ambazo haziko active au zile ambazo zina broken links. Hivyo karibuni tutaupdate directory list yetu na tutaweka blog zote ambazo hazipo kwenye blog dorectory list.


Na pia kwa wale ambao wamebadilisha address za blog zao na wanataka bado blog zao ziwe kwenye directory list basi tuletee address mpya ya blog yako.  Sisi tukiwa tunaupdate na kuona blog inabroken link tunaiondoa na sio kila blog tunakua tunaelewa kuwa imebadilishwa address au imefungwa. Tunachojitahidi ni kuhakikisha ni kuwa blog zote zilizoorodheshwa hapo zipo active. 

Together we can!

Thanks

1 comment:

Delima said...

Thanks for sharing...thanks for Google Translate as well.

Cheers,
Delima