Jinsi ya kupata wasomaji wa kudumu

Leo nilikua nasikiliza marketing radio moja hapa nikakuta kipindi chao kilikua kizuri sana hivyo niliyoyasikia huko naona sio vibaya kama nitashare na wengine humu labda moja au mawili yatakusaidia. 

Topic yao ilikua inazungumzia jinsi ya kupata wasomaji wa kudumu. Walikua wanasema watu wengi wenye websites au blogs ambazo haziuzi kitu chochote (information) hawafahamu kuwa wasomaji wa blogs au websites zao ndio wateja wao. Wengi wanajitahidi kupost kila siku lakini hawajui bila msomaji wa kusoma basi wanayoyaweka huko ni bure tu.

Sasa wakasema kama una blog au website na umeshaweka post kadhaa na wasomaji wachache wameshaanza kupitia blog yako kuna mambo mengi ya kuzingatia na kufanya ili wasomaji wako wawe wanahamu ya kusoma blog/website yako kila mara na hata kuwaambia watu wengine kuhusu blog yako..

1. Quality
Hili nadhani kila mtu anafahamu kama unaweka vitu visivyo na quality kwenye blog yako ni kama unawadharau wasomaji wako hivyo ni heri upost vitu vichache vyenye quality nzuri kwa week kuliko kupost vitu vingi visivyo na quality.

2. Unique
Na hili pia wengi tunaelewa kama blog au post zako sio unique basi ujue chance ya mtu kustumble kwenye blog yako halafu arudi tena au akubookmark ni next to none. Hivyo uniqueness ni muhimu...

3. Respect
Hata kama huwasiliani na wasomaji wako in a personal level ni muhimu sana kuonyesha kuwa unawaheshimu. Onyesha heshima kwa kusikiliza maoni yao, kujibu maswali yao kama wanafanya hivyo na pia kuweka vitu ambavyo hata wewe ungependa kusoma kama ungekua msomaji. Na kama wasomaji wako hawatoi maoni au kuuliza maswali yeyote basi tone ya post zako zionyeshe heshima na sio kiburi na kejeli. Kumbuka wasomaji wako ndio wanakuweka hapo sasa kama huwaheshimu utajikuta huna mtu wa kusoma blog yako. 

4. Write what they want to read
Kama watu wameishaijua blog yako na wanajua wewe blog yako inazungumzia mambo gani sana basi stick to that..eg sports, politics, beauty, fashion, family, women, children etc Sio leo uzungumzie michezo kesho urudi kwenye siasa, kesho kutwa upo kwenye fashion etc etc na kama blog yako sio ya breaking news basi jitahidi uweke news za aina moja tu..Sio kukopy na kupaste kila news unayoiona kwenye blog nyingine. 

5. Be professional
Kama una blog inazungumzia kitu fulani basi act like a pro in that topic. Kama hujui research. Ili ukiulizwa swali upate kulijibu. Na pia be professional katika blog template yako au website yako. Ukiweka vitu color au gadgets za kitoto basi watu watakuchukulia hivyo hivyo. Sasa punguza clutters, mavitu mengi na templates yenye rangi rangi nyingi itawakimbiza wasomaji wako. Wanasema jitahidi sana background yako iwe solid color (1st choice). Kumbuka kila unachopost kwenye blog yako kinakurepresent wewe. 

5. Multiple platforms
Wanasema kila mtu ni tofauti na kila mtu anaprocess information kwa njia tofauti sasa kwa vile siku hizi kuna platform nyingi za kupeleka habari basi usiache kuzitumia. Wamesema kwa mfano kwenye site unapopost kitu fulani basi kama hiyo post ina picha tumia Instagram kuweka picha ya hiyo topic huko halafu link hiyo picha kwenye hiyo post yako kwenye blog..Wanasema kuna watu wanaelewa habari zaidi kwa kuangalia picha. Hivyo wakiona picha kama inawavutia watataka kusoma zaidi basi wataenda kwenye blog au website yako. Lakini alisema hakikisha link unayopost kwenye hiyo picture ni ya hiyo post na sio ya blog yako yote in general. Wengi wanakosema na kulink blog yao as a whole na mtu akifuata ile link akakuta kitu kingine kinamkaribisha basi hatakua na hamu ya kusoma blog yako tena bali akikuta hiyo topic aliyoifuata kwa kutumia ile link basi akipendezwa nayo atajikuta anasoma post zingine ulizonazo katika blog au site yako. Hivyo akasema katika topic moja unayopost tumia Instagram, halafu kama una uwezo wa kurecord basi soma hivyo habari hata kwa ufupi uiweke kwenye podcast au blogradio na huko nako pia link your blog. 

6. Easy to navigate
Amesema kuna watu wengine wana website au blog lakini wanafanya iwe ngumu kwa wasomaji wao kuweza kuona post za nyuma au hata mambo mengine. Amesema ili watu wapende kuja kusoma kila siku hakikisha blog au website yako iko easy kunavigate around.

7. Give credit when it's due
Amesema ukitaka watu wakuheshimu na kukuamini basi toa heshima kwa watu unaotumia info au picha zao. Amesema watu wengine wanafikiri wasomaji ni wajinga kuwa kile wanachoweka basi kama wamekitoa mahali pengine hakuna mtu atakayejua. Sasa amesema kama umetoa picha mahai fulani usijifanye ni yako wewe original weka heshima. Kama umetoa habari mahali fulani basi link hiyo sehemu ulipoitoa. Na kama umeiandika hiyo habari in brief basi weka link ya mahali unayojua wakienda huko watapata habari yote kwa kirefu zaidi.  Hiyo itawaongezea wasomaji uaminifu kwako na pia kuwarahisishia kama kitu hawajaelewa wataenda kwenye hiyo link na kupata habari zaidi. Pia faida ya kuweka link na credit za mahali unapotoa habari zako ni kuwa kama watu wakigoogle ile blog au site uliotoa information pia na ya kwako itapop up kwenye list na the more blog yako inakuwa searchable mara nyingi the more inapanda juu katika search. Hivyo hata siku kama umepost habari ambayo watu wengi pia wamepost lakini watu wakigoogle blog yako itakua juu kwa habari hiyo. Na la muhimu wengi watakua wanatumia blog yako kwa kujua kuwa ni unapata mambo memgi ya muhimu na unawalink kwenye habari nyingine zaidi zamuhimu na utaonekana uko pro.

Watu wanachokosea
1. Alichochosema watu wanakosea na kujipunguzia wasomaji bila kufahamu ni kuwa mtu anaweza kuwa na blogspot, wordpress na tumblr sasa anapost habari hiyo hiyo kwenye sehemu zote hizo na kufikiria kuwa watu wengi wataona na kusoma. Amesema hiyo ni kupoteza nguvu kwa vile watu wanaopenda kusoma na kujua habari zako ni nzuri watakufuata tu hata ukiwa na mahali pamoja tu. Na kama unataka habari yaku iwe juu mapema kwenye search engine basi iweke mahali pamoja tu. Blog yako ikiwa watu wanaingia mara kwa mara katika kila wanachosearch basi itajikuta inakua juu tu lakini zikiwa tatu nne zenye habari hiyo hiyo basi zingine hazitaonekana bali ile moja yenye watu wanayoingia mara kwa mara. Hivyo kuweka kwenye platform nyingine zenye muundo mmoja ni kupotea muda tu na kupoteza wasomaji.

2. Kingine wamesema kama unatumia social network kama Twitter, Facebook au G+ set platform moja tu iwe inatweet kwa wakati mmoja. Au kama unataka ziwe zinatweet zote basi set kwa muda tofauti. Ukiwapata watu wa nchi mbalimbali kwa masaa yao. Mfano kama unataka watu walioko Marekani, Africa na Asia  wasome habari yako asubuhi basi set hizo ziwe zinapost kwa wakati tofauti lakini usije ukatumia mfano blogspot, instagram, facebook, podcast, tumblr kupost habari hiyo hiyo kwa mara moja kwenye twitter au kama unashare kwenye G+ ...Amesema ukifanya hivyo watu watakuchoka na hata hawatasoma habari zako tena. Kama ni habari hiyo hiyo share kwenye twitter kwa masaa tofauti na kama ni G+ share zile za maana tu zingine watakuja kuzifuata wenyewe huko. Sio kila kitu unashare. Share vichache vilivyo interesting halafu watu watajikuta wanaenda kuangalia nini tena unacho huko kwenye blog yako.

Okay I hope hii itawasaidia wengi kwa sababu niliona ni ujumbe mzuri sana hasa kwa watu wanaoanza kuingia katika hii fan hii ya kublog iwe as a hobby au profession..Kwa vile wengi wanaaznza na kujikuta hawana wasomaji wakudumu kila siku na kujikuta wanakata tamaa bila kujua blog zipo nyingi sana sasa ni nini kitawafanya watu wasome blog yako na kupenda kurudi kusoma kila siku ndio jibu la kuweza kupata wasomaji wa kudumu. 

Kama unafahamu lingine ambalo sijaliweka hapa feel free kuchangia kwenye comment hii yote ni kujaribu kutafuta njia ya kuboresha blog zetu za watanzania popote pale walipo..

5 comments:

emu-three said...

DARASA nzuri hili, tunashukuru mpendwa ubarikiwe sana!

Bennet said...

hii safi sana

Albert K(AK) said...

Point tupu,thumb up!from akclassic.blogspot.com

wamtaani said...

good lesson nimeongeza kitu kikubwa sana..

Fadhy Mtanga said...

Ahsante sana kwa hili darasa. nimejifunza mengi sana.