Badges

Hatukujua ni watu wengi hivi watataka hizi badges..

1. Itachukua kama week to week mbili kupokea badge na certificate yako.

2. Tunavyosema sisi hatutawasiliana na nyie ina maana kuwa, mwaka jana baada ya mashindano tulianza kuingia kwenye kila blog iliyoshinda nakutafuta contact info za washindi hao. Tulizopata ili tuwajulishe email hizo nyingi zilikua ni wrong, zingine zilikua ni zina auto responses hivyo ilikua usumbufu sana sana na mwisho wa yote sio wote tuliowatumia hizo badges waliziweka kwenye blogs zao. Ndio maana tuliamua mwaka huu kupunguza usumbufu na kwa vile ni watu wengi wameshafahamu hili shindano basi tunafahamu fika kama mtu anahitaji badge yake na certificate atuandikie. Hiyo inafungua communication kwetu ya sisi kuweza kuwasiliana na wewe kwa urahisi na kukutumia badge yako.

3. Sijui ni rangi red au blue zinaonekana wapi. Kuna mtu anasema kwenye hizi blog hapa kuna zingine ni red na zingine ni blue..Mimi sioni rangi tofauti kama  unaona hivyo haina maana yeyote labda na just a link problem..

1 comment:

emu-three said...

Hata mimi nahitaji hiyo badge usinisahau!