Tafadhali Usitumie Form Ya Mwaka Jana

Ninaamini nimeshaiondoa form iliyotumika kupendekeza majina ya blog zilizoingia kwenye shindano letu la mwaka jana lakini kinachonishangaza ni kuwa bado kuna watu wanaoina na kuijaza. Hata sielewei kweli wanaipataje. Tafadhali form ya mwaka huu itapatikana hapa mwezi ujao tarehe moja..Itakua na mwaka 2012. Tafadhali kama unaujuzi wa kuipata hiyo ya zamani hata kama haipo humu usiitumie kwa sababu hata jinsi ya kujaza mwaka huu tumezibadilisha. Toka mwa huu nimeanza kupokea email kuwa form imejazwa na emails hizo zimeongezeka sana mwezi huu wa tatu...

Lingine tunalowaomba ni kuwa tafadhali jaribu kuzingatia sheria. Mwaka huu kama tunavyopokea emails za watu wengi tunajua ni wengi watashiriki kuliko mwaka jana lakini bado man power yetu ni ndogo. Pia kutokana na wingi wa email hizi tunahsi blog mwaka huu zitakazoshiriki ni nyingi zaidi hivyo muda wa kuweza kuhakikisha kuwa blog fulani inastahili kuingia kwenye kipengele hiki na sio hiki sitakua nao tena kama mwaka jana.  Hivyo sheria za mwaka huu tutaweka badge za wewe kuchagua kama mwandishi wa blog yako je ni categories gani blog yako inahusika zaidi uweke kwenye blog yako ili wanao kupendekza waweze kuelewa. Blog ikipendekezwa kwenye kipengele ambacho haihusiki itaondolewa na wala haita wekwa kwenye kipengele kingine. Hivyo hakikisha unapendekeza blog yako kwenye vipengele vile tu ambavyo blog yako inastrahili kweli. Kupendekeza blog yako kwenye vipengele vyote haitakuengezea chance ya kushinda..

Shukrani

No comments: