JUMUWATA

Asante kwa yule aliyetuma link ya huu umoja. Kumbe kuna umoja wa watanzania tayari. Hivyo ni vizuri nikiweka hii post na link ya huu umoja ili kila mtu mwenye swali kuhusu umoja wa watanzania basi apeleke huku.

Nadhani jibu tumelipata sasa ambalo kila siku nilikua naulizwa. Mimi binafsi nilikua sina habari kuwa kuna umoja wa bloggers wa Tanzania. Jibu ni kuwa KUNA UMOJA WA BLOGGERS WA TANZANIA. Na wote walionitumia email za kuwa interesting kujiunga na umoja  wa bloggers wa Tanzania tafadhali ingia kwenye hii link http://blogutanzania.blogspot.com/ .

Hivyo mjadala kuhusu umoja wa bloggers wa Tanzania umefungwa. Nashukuru sana kwa wote mliochangia mawazo yenu. Na pia kama nisingeamua kupost hii issue wengi wa wanaotafuta umoja na wanaotaka kujiunga wasingefahamu hili.

Shukrani

2 comments:

emu-three said...

Nashukuru sana P, Kwakweli tulikuwa hatujui kuwa huo umoja upo, na unafanya nini kutuunganisha, mimi napendekeza kuwa kwasababu ulikuwa na lengo jema kama hilo, basi wasiliana na huo umoja ujaribu kuwapa kile ambacho ulitarajaia kufanya kwa mfano kuwaunganisha wanablog wote kama ikiwezekana, kuwa na namna ya kuhamasishana kama ulivyofanya kwa kuweka blogs award, hili limehamasisha wengi na hata kujulikana na pia kuweka interview, kwa `undergraund blogs' ili wajulikane nk.
Kama chombo kama hicho kipo basi kijitangaze zaidi ili tukijue, ngoja niingie kwenye hiyo blog nione nini kimefanyika, tunashukuru sana kwanza kwa kutoa hoja hiyo na pili kutuwezesha kugundua huo umoja, ingawaje hatujajua ulivyo...
Tupo pamoja ndugu yangu, inagwae ni kwa shida shida, kama ulivyoanisha wengine inabidi tuwahi asubuhi sana ofisini kabla hawajaja wajamaa, uvizie komputa yenye internet, ufanye kwa haraka...

nyahbingi worrior. said...

Habari za siku.Nakuja kwenu na lengo moja tu.Tushirikiane kuifufua JUMUWATA.Naamini tukiunganisha nguvu zetu sote tutafika mbali sana.

Luihamu W.Ringo

nyahbingiworriors.blogspot.com