Umoja Wa Bloggers Wa Kitanzania

Asanteni sana wote kwa ushauri na majibu yenu . Sikujua nitapokea emails nyingi hivi kwa mara moja hivyo nimeona nijibu hapa kwa ujumla.

1. Idea ya fund raising sio kigezo cha kuwa na umoja huo. Hiyo niliweka kama idea mojawapo ya mafanikio ya umoja huo. Kwa vile kila mara nikiwa namsaidia blogger kufanya kitu fulani katika blog yake. Ukimwambia download kitu hiki ndio hapo anaanza kukwambia "computer" hivi "computer" vile. Ndio maana nikawa nikawaza hiyo idea ya jinsi ya kutafuta nyia ya kusaidia bloggers.


2. Kuhusu kuwa na semina elekezi kwa bloggers badala ya kuwapa baadhi ya bloggers tu laptops etc. Hilo ni jambo nzuri pia lakini semina hizo zitaandaliwa na nani? Bila kuwa na umoja hakuna mtu atakayeweza kujitolea kusema ngoja nifanye semina ya mafunzo kwa bloggers wa kitanzania.



3. Na pia wazo la kuwa na onsites semina ni jambo zuri ila nalo ni kuwa lazima kuwe na chombo kitakazhoweza kutekeleza hayo mambo. Na ukianzisha semina mfano Mwanza itabidi na nyingine ufanye sehemu nyingine na nyingine kwa vile sio bloggers wengi wataweza kwenda kuhudhuria ikiwa kwenye sehemu fulani tu.

4. Na kuhusu kuwa umoja huu utakua mkubwa sana na ni heri kila watanzania wanaoishi katika kila bara waamue kuanzisha umoja wao. Hilo pia linaweza kuwa jambo zuri lakini LINK kati yao itakua ipi? Link kati ya bloggers walioko Tanzania na bloggers walio nje ya Tanzania itakua ipi?

5. Na kwa wale wanaotaka niwaeleze jinsi ya kuraise fund. Well mimi nina ujuzi wa kuraise fund online au offline for a good cause. Sijawahi kuona mtu anaraise fund kwa ajili ya manufaa yake peke yake. Kwa wale wanaotaka kutafuta jinsi ya kusupport blogs zao labda wangeeka donation button kwenye blogs zao. Au kma unaona watu watakua na hamu ya kuisoma kwa kulipia basi kuna site zinafaya hiyo service. Watu wanalipia kusoma baadhi ya post kwenye blog yako.
Ila kuna site nyingi za kuraise money kwa ajili ya mambo mbalimbali ya jamii. Na watu wengi wanaoguswa huwa wanachangia. Na pia offline fundraising ni pale kutengeneza vitu mbali mbali na kuwapelekea watu unaowafahamu, kazini, kanisani. gym etc. Hata kama kitu kinatakiwa kuuzwa $1 lakini ukimwambia mtu nauza hizi kwa kuchangisha hela kwa ajili ya kitu fulani, watu wengi huwa wako tayari hata kukupa 50 times ya cost ya hicho kitu kama wanajua kinakwenda kwa ajili ya manufaa ya jamii, au awareness. Lakini sio kuwa namfahamu mtu mmoja ambaye atanipa hela. naomba hilo lieleweke.


Okay hayo ndio majibu ya maswali yote niliyoyaata mpaka sana ...Shukrani na pia bado wenye mawazo ya jinsi ya kufanya wasiache kuandika

4 comments:

nyahbingi worrior. said...

http://blogutanzania.blogspot.com/ hii ni link ya kurasa ya umoja au jumuiya ya wanablogu Tanzani(jumuwata).

emu-three said...

Wazo jema ndugu yangu maana huenda kwa kufanya hivyo tutapiga hatu nyingine.....oh, kumbe kuna umoja huo, mbona hatuujui!

jigambeads said...

kwa hilo natoa support kubwa by jigambeteam.

Ally shaaban mgido's said...

WAZO ZURI SANA HILI KWA KUAWA NA UMOJA
HUU NAIMANI UTASIDIA SANA ITAKUWA VYEMA KATIKA KUPIGA HATUA. CHA MSINGI UMOJA HUO UTAMBULISHE RASMI KATIKA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI ILI BLOGGERS WAFAHAMU NA KUJUA JINSI GANI YA KUJIUNGA.NAUNGA MKONO KWA NGUVU ZOTE.
KILA LA KHERI MUNGU AWABARIKI SANA.
ALLY S. MGIDO'S