Blog nyingi feed updates zao hazifanyi kazi ni kwa nini?

Nimeona kuwa kuna baadhi ya blogs feed zao haziwi update sasa sijui ni wamebadilisha link na google inashindwa kujua link mpya au  kuna jambo lingine wamefanya likasababaisha hii.


Feeds updated ni muhimu sana kwa blog yako kwa vile kuna watu wengine hawana muda wa kupitia kila blog kusoma unachopost kila siku. Lakini wanaofuatilia blog yako kwa makini sana na kila unachopost hawamiss kusoma  kwa vile wanatumia feed readers. Najua zipo feed readers nyingi lakini hii ya google ambayo ndio inatumiwa na watu wengi sana basi ni muhimu uhakikishe kuwa inalink na blog yako ili iwe update. Sasa kama blog yako haiupdate basi wasomaji wako watamiss blog yako na wengine watazania hujaupdate kwa muda kumbe sio kweli.. Hivyo jaribu hata kufollow blog yako mwenyewe ili uone je unapata updates za blog yako? Kama hupati ni nini tatizo? Unaweza kupoteza wasomaji wengi sana kwa kutokua kwa kitu kidogo kama hiki.
Wengine wakipitia blog na kuona wanachopenda basi wanaiadd kwenye feed readers zao lakini mambo yalivyo mengi mtu hukumbuki tena au unasahau kuwa kuna blog fulani ina mambo fulani au kuna blog fulani niliiadd jana lakini mbona sijaona feeds zake. Feed update ikimfikia msomaji wako ile post ndio inamfanya akumbuke blog yako na awe na hamu ya kujua kesho ama kesho kutwa utapost nini tena. Lakini asiposoma kutoka kwako hata kukusahau atakusahau labda iwe sijui ni rafiki, awe ameshakufuata kwa muda mwingi au blog yako iwe iko so interesting ndio utakumbukwa na wasomaji wengi....

Ukiangalia kwenye hii directory list yetu tuliyoiweka sasa hivi kuna blogs kadhaa zinaonyesha kuwa hazijawa update kwa hata zaidi ya miaka miwili lakini ukweli blog zao zipo live and active. sasa jiulize ni wasomaji wangapi wa blog yako wanamiss?.

Jaribu kuangalia hapo kwenye directory list uone kama blog yako na updates zako zinawiana. 

No comments: