AIDS And Black Community

Oookay ...Nini tena nanaleta humu leo? Si mimi ninayehamasisha watu wakianza kublog na hili wasiende kuishia blog lile jamani. Yes naelewa tupo hapa kwa kuhamasisha watu ili wengi waweze kuingia katika hii fan ya kublog, wale wenye blogs tayari ni mambo gani ya kuzingatia kuongeza ubora wa blogs zao na jinsi ya kujitangaza kwenye social networks ili kupata watu wengi wakusoma blog yako ila leo nilipokua naangalia CNN news asubuhi kuna jambo walikua wanazungumzia likanigusa sana nikaona nisipoandika post kuhusu hili basi sitakua nafanya justice kwa Taifa langu.



Walioyoukua wanayazungumzia ni mambo mengi sana na kuna mengine wengi huwa tunayasikia kila siku, lakini walivyokua wanazungumzia sababu za tatizo hili kuwa kubwa katika jamii zetu ndio macho yakafunguka. Nikawa najiuliza kweli  kwa nini sisi mpaka leo tuwe tunatafuta formal places za kuzungumzia hili jambo? Je wangapi wana blogs za siasa, dini, mapishi, elimu, jamii, burudani, michezo burudani au hata habari wanazungumzia hili jambo mara kwa mara au tunasubiri tu siku ya ukimwi duniani ikifika ndio tanakumbushana tena? Nimegundua hakuna sehemu maalumu ya kukaa na kusema tuanze kupena habari kuhusu huu ugonjwa. Kila unapopata mahali au unapoweza kueleza hili jambo ni muhimu kuweka awareness sana tu.

Je ni wanagapi majumbani wanakaa na watoto wao, wadogo zao au hata rafiki zao kuwaelezea kuhusu haya au wanayoyaelewa kuhusu huu ugonjwa? Honesty mimi mwenyewe nikiongea na mama yangu mzazi mambo ya sexuality na ukimwi unamwona kabisa anakua uncomfortable. I am like what? Hizi culture zetu ndio zinatumaliza kila siku. Kwa nini tukae kimya na wakati ukweli upo? Si watu wanakufa kila siku kwa kutokana na ugonjwa huu sasa kwa nini tunyamaze tu? Unajuaje ukiongea kuna mtu atakayesikiliza na atakwenda pima na kujikuta status yake kama hana basi anaelewa jinsi ya kijikinga zaidi kama anavyo basi anawahi dawa, kuongeza maarifa katika jinsi ya kujikinga ili asipate maambukizo mengine ya virus hivi na pia asimwambukize mwingine? Tutakalia kuwa na culture yetu hivi, culture yetu vile ni lini tutaanza kubreak this cycle? Ndio bibi na mama zetu ilikua vigumu wao kuongelea haya mambo ya sexuality as if ukizungumza au ukitaka kujifunza basi wewe utafikiriwa vibaya au utaitwa muhuni kumbe knowledge inaweza kukuokoa sana tu. Kwanini generation ya leo tusianze kufungua midomo na kuelezea wadogo zetu ni nini kiko mbele yao? Why can't we break that code of silence? When are we going to break this cycle?

Katika maogezi yao wamesema kuwa ingawaje population ya wamerekani weusi (African-Americans) ni ndogo kuliko populations za wengine lakini inasikitisha kuwa African Americans ndio wanaongoza kwa kuwa na virusi vya ukimwi. Katika data zao wamesema ration ni 8 to1 kwa wanaume, 15 to 1 kwa wanawake, 36 to 1 kwa lesbian na 46 to 1 kwa gays. Wakiwa na maana katika kila mtu mmoja mwenye virusi vya AIDS katika hilo group lingine basi ni wanaume nane wa Africans Americans wanao. Katika kila mwanamke mmoja mwenye virusi hivi basi ni kumi na tano kwa watu weusi wanao etc. Ingawaje hawakusema hilo group lingine waliolinganisha ni Caucasians only, Hispanic Americans, au Asian Americans tu ndio au ni wote hao kwa pamoja wamechukua samples zao au la? Hata hivyo ukiangalia iwe wamewajumlisha wote hao kati ya blacks au wametumia Caucasians tu lakini bado ratio ni kubwa sana.

Sasa walivyokua wanaenda kwenye communities zilizo na watu weusi wengi na kwenye makanisa wakawa wanauliza leaders wao wanafikiri pamoja na education na knowledge hizi zote zinazotolewa kila siku ni kwanini rate ya maambukizo ni kubwa bado katika communities zao? Hao watu waliongea mengi lakini kubwa nililoona ni kuwa mengi yanarelate sana na sisi sana tu:-
a) Kukaa kimya, nyuma au chini kusubiri mahali maalumu pa kuanza kuelezana kuhusu huu ugonjwa. Kumbe hata kwenye comminities zao hawana tabia ya kuongelea huu ugonjwa kama wengine wanavyoongea  na watoto wao ama kwenye communities zao. Sisi tunasubiri tupate sehemu ya kuelezana au mtu aje atuelezee.  Kumbe kupata hiyo sehemu ya namna hilo lazima basi kuwe na sponsor wa kugharamikia “semina elekezi” ili tukaelezeane. Je tukisubiri hao sponsors wa kutuwekea formal places za kufundishana na kuelekezana au kupeana awareness ya huu ugonjwa si tutaisha wote? Hakuna formal places za kuzungumzia huu ugonjwa. Kama una blog, gazeti, wewe ni kiongozi wa dini, kiongozi wa kampuni, siasa au hata nchi. Kama unapenda watu wako basi usisahau kueleza watu kuhusu hili.. Tukumbuke pamoja na dawa zilizopo lakini maambukizo bado ni mengi sana ya ugonjwa huu na awareness yake ni  ndogo sana kwa watu wengi tu hawana ndio inachangia hata vifo.

Kuna siku nilikua nasoma blog moja nikakuta kuna mtu anaomba ushauri amegundua kuwa ana virus vya ukimwi. Watu walikua wanamfariji hivi na vile lakini comment moja ndio ilinifanya niogope kweli. na kusikitika sana. Kuna mwanamke mmoja alikua anamwambia huyo aliyeomba ushauri kuwa asijali kwa vile yeye aligundua kuwa ana virus hivyo miaka minne iliyopita ila mpaka siku hiyo anaandika anasema hajaanza kutumia dawa. Nilisikitika na kusema je awareness iko wapi hapa? 2011 bado mtu mwenye virus anasema hajanza kutumia dawa kwa vile bado hajaanza kuumwa na maisha yanaendelea vizuri? Je na yeye ni nani alimshauri hivyo kuwa unatakiwa usubiri kutumia dawa mpaka utakapoanza kuumwa?  Na ni wangapi wanafanya hivyo kama yeye? Ndio maana wengi wakiugua kidogo wanapoteza maisha kwa vile si ajabu alikua na virus muda mrefu lakini hakutumia dawa sasa ugonjwa kidogo basi mwili unashindwa kujikinga. Unajua watu wanasahau kuwa UKIMWI hauui ila complications za ukimwi ndio zinazoua. UKIMWI ni hali inayofanya mwili kushindwa kujikinga na magonjwa mengine. Immunes zimekua comporomise sasa unatakiwa utumie dawa ili kukeep hizo CD4 numbers (white blood cells) zako juu wakati wowote. Kwa vile mwili wako umepoteza ule uwezo wa kujikinga na magonjwa mbali mbali. Hivyo zikiwa chini gonjwa lolote likikuta kwa vile mwili wako hauwezi kujikinga basi ndio unaumwa sana au unaishia kufa kwa kitu kidogo tu. Sasa ukiangalia na nchi yetu haina canselors wengi wa kuwashauri watu utakuta huyo mtu anarely na information anazozikuta humu kwenye blog. Sasa akisoma ushauri wa mtu mwingine anayemwambia mimi nina 4 yrs na situmii  dawa na yeye si ataendelea hivyo hivyo kweli?

Kwenye kilele cha miaka 30 ya huu ugonjwa walikua wanaonyesha South Africa kuhusu ukimwi katika kuhoji kijana mmoja alikua so proud na kusem yeye toka ameelewa matumizi ya condoms basi anatumia condoms wakati wote. Lakini mara katika mahojiano hayo akajikuta anasema anare use those condoms..Mwandishi wa habari mwenyewew alishtuka na kusema vitu vidogo vidogo kama hivyo ndio vinachangia maambukizo mengi na ambayo ni unintentional kabisa. Awareness na personal responsibility ni muhimu sana. Ndio hivyo nikasema bila kuelezana ukweli basi tutaishia kuwa scapegoat kila siku. Watu weusi hivi, watu weusi vile, Africa hivi  Africa vile .....

b) Walisema lingine linaloongezea hii ni personal responsibility- wamesema kwa sisi weusi kwenda kutest status zetu bado kabisa. Ili mradi tuwazima na hatuumwi basi tunaamini tuwazima. Nikasema this is so true kwa kwetu pia Tanzania. Hatutaki kujua kabisa status zetu lakini kumbe ni bora kujua mapema kuliko kufahamu ikiwa ni too late. Siku hizi kuwa na virus sio death sentence tena, sasa kwa nini mtu usijaribu kujua tu status yako. Kwa nini utumie sijui uzito au mtu mwingine kuwa tester yako. Watu wengine wanafikiri ili mradi mimi ni mnene basi I am fine.Au kwa vile my significant other is fine basi na mimi ni mzima. No take personal responsibility kama mwenzako hataki kupima wewe nenda kapime ujue status yako mapema. Na ukweli ni kuwa hamna kitu kigumu kama kusubiri majibu ya vipimo vyovyote vile. Iwe ni routine check up au sio lakini inaogopesha tu kwa vile hujui utaambiwa una cancer, BP au diabetic chochote  kile unaweza suiwe nacho mwaka jana klakini mwaka huu unacho. Lakini ni wajibu wetu kufahamu na ukifahamu mapema ni bora zaidi.

c) Lingine akasema ni stigma tulio nayo ya kuzungumzia kuhusu huu ugonjwa na inafanya hata walio nao waogope kuongea kwa ajili ya kufikiri kuwa society itawafikiriaje au itawafikiria waliupatataje. Kila mtu anafikiri kua mwenye ukimwi kaupata kwa njia moja tu. Mpaka leo bado tuna mawazo hayo wakati hasa kwa nchi yetu ukiangalia kila siku mambo mengi yanafanyika bila safety procausions wala nini honesty from my opinion labda 50% ya watu wenye virusi hivi wanaput blames kwa wenzi wao wakifikiri huyu ndio kaniletea kumbe wameupata somewhere else. Kuna siku nilijiuliza mwenyewe mimi nimeshafanya kazi na mtu mwenye viruzi vya ukimwi na pia nimeshawahi kufahamu watu kama watatu wenye virusi vya ukimwi wote hao ni Caucasians. Na wako open na kukubali status zao lakini watu ambao unaambiwa kila siku ni wengi wenye hivi virusi (African Americans) sijawahi kuona hata mmoja. Sasa najiuliza je hao watu wanaishi wapi? Jibu ni kuwa tuko humu humu, tunaishi pamoja lakini hakuna hata mmoja anayetaka kukubali ukweli au kuongelea hili jamno labda ni intentionally au unintentionally. Kwa vile walisema watu weusi ni wengi wanaishi na virusi lakini hawajui kuwa wanavyo kwa vile hawataki kwenda kupima….Sasa hapo ndio hivyo maambukizo yanaongezeka kwa wengine bila hata kukusudia kuwa wanaambukiza wengine. 

Conclusion ya yote haya ni maswali yangu haya

1) Je ni lini tutaanza kuondoa hii stigma ya kujudge watu wenye kuishi na virus hivi?

2. Ni lini tutakua na tabia ya kuongea na kupeana awareness kuhusu huu ugonjwa kila tunapopata nafasi?

3) Na wazazi ni lini mtaanza kufungua communication kati yako na wanao na kuanza kuwaeleza kuhusu mambo mengi ambayo wengi wetu hatukupata chance ya kuelezewa na wazazi wetu kwa ajili ya culture yetu. Lakini sasa hivi we know better why don't we do better?Let's forget about the culture for a minute people are dying na maambukizo yanazidi sana tu jamani.

4) Je sisi wenyewe tunachukua jukumu gani la kupambana na huu ugonjwa kama jamii?

5). Kama mtu pekee binafsi unachukua jukumu gani la kujua status yako?

Tukumbuke taifa likiwa na watu wengi wagonjwa nalo linakua gonjwa. Tutamlaumu nani?

No comments: