Warning!!!!!!

Kuanzia juzi kumekua na watu wengi sana wakiingia kupiga kura huku kutokea blog moja.  My curiousity got the best of me nikaamua kuangalia ni nini kilichowekwa huko mpaka kiwavutie watu wengi hivi waingie kupiga kura direct kutokea hiyo blog? Well, nilivyoingia nikakuta kuna post imewekwa kuhusu hili contest. Haikuwa jambo la kunishangaza kwa vile ni blogs nyingi pia zimeshaandika sana kuuliza ni jinsi gani wao hawakuchaguliwa na watu wengi wameshapost comments au kkuandika emails kuulizia kwanini blog fulani haijawekwa huku anyway kilichonishangaza ni jinsi wasomaji wa hiyo blogs walivyoacha coments zao.

Tafadhali elewa kuwa hatuwezi kumzuia mtu yeyote aseme chochote kila anachokitaka kuhusu Tanzanian Blog Awards ila tunataka kuwaambia watu ni kuwa,  kama ukipitia blog yeyote ukakuta kuna  post imewekwa na watu wanaojibishana huko wanajifanya ni sisi tafadhali usifikirie hivyo. Sisi hatuna muda wa kupitia kila blog inayoweka post za awards hizi na kuzisoma achilia mbali kupitia huko na kuanza kutukana watu. Sisi hatuko hapa kwa hilo. Kama kuna watu wana ugomvi na watu wengine please tunaomba msijibizane huko kwa kutumia jina hili au kusema kuwa tumeacha blog fulani kwa ajili ya hili au lile. 

Sis hatuko hapa kwa ajili ya kugombanisha watu na hii contest iliwekwa kwa madhumuni mazuri tu lakini naona sasa hivi kuna watu wanaigeuza na kuanza kuifanya iwe platform ya kutafutana ubaya. Sisi hatujapendekeza blog yeyote au kuiweka kapuni blog yeyote kwa sababu fulani kama watu wanavyodai kwenye hizo comments. Hatujaanzisha hii awards ili sijui tumkomoe mtu fulani. We don't even know those bloggers and to be honesty one of these blogs ndio ilikua mara yangu ya kwanza kuiona. (Yes I live in the same planet)  but I was not aware of it. Na nimeangalia na kuiona ipo kwenye directory list yetu hivyo lazima nililetewa link na kuiweka lakini baada ya hapo sijapata nafasi kuingia tena humo. Mwenye blog hiyo simfahamu sasa watu wakiweka comments za kusema tumeiacha kwa sababu zetu binafsi au kulipiza kisasi hiyo sio kweli. We are not here for that...Kama blog ingependekezwa kwa kutumia form zetu au kwa email katika kile kipindi tulichokua tunapokea majina ya blogs hizi lazima ingewekwa huku.

Bloggers wengi sana wameandika emails huku kuuliza kwanini blogs zao hazijashirikishwa katika shindano hili kwa vile blog zao ni mashuhuri sana sehemu fulani, zina wafuasi na wasomaji wengi sana na wengine wameuliza kwa nini blog ya fulani haijashirikishwa? Lakini kama tulivyoandika kwenye post ya nyuma tulisema kama wasomaji wa blogs hizo au waandishi wenyewe hawakuona umuhimu wa kuchukua muda wao kupendekeza blogs hizo basi ndio maana majina yao hayapo, Sio kuanza kulalamika kuwa blog zao ziliachwa kwa makusudi fulani au kutafuta sababu yeyote ile. Majina yao yaliletwa na sisi tukayatupilia mbali kwa sababu zetu. Na kuna watu wengi tu wanaambiana uongo kuwa "sisi wandaaji wa shindano hili tumewaambia hao watu sababu za kuacha blog fulani"  Tafadhani hakuna msemaji mkuu mwingine wa awards hizi zaidi ya mimi hivyo yote yanayosemwa huko ni watu wanaamua tu kujisemea mambo yao kwa sababu zao.

Tuko hapa kwa bloggers wote wa kitanzania na kama kuna bloggers fulani wana ugomvi wao please msitutumie sisi kuwa platform yenu ya kukomeshana. Ndio maana hata watu wanaotuma message zao hapa za kutukana bloggers wengine hatujazipost kwa vile hatupo hapa kwa ajili ya mambo hayo.

3 comments:

Admin said...

Siku zote, sio watu wote wanaopenda akuona maendeleo au kusifia or kuridhika na ki2 flani. Watasema mwisho watanyamaza

Mwanasosholojia said...

Kwenye jamii ya watu wenye mawazo tofauti, haya hayakosekani, lakini yasiwavunje moyo. Wengine tunarecommend mawazo na jitihada zenu za kuendeleza fani hii ambayo bado haithaminiki katika jamii yetu

Unknown said...

NAIMANI HAWAJACHELEWA HATA MWAKANI SHINDANO LITAKUEPO SO WANGOJE MWAKANI WACHUKUE FORM KAMA HII IMEWAKOSA MWAKANI WASIJISAHAU..MIMI BLOGGER WA KINGKAPITA..NAOMBA KURA ZENU VILE VILE KWA KIPENGELE CHA BEST MUSIC NA BEST ADVERTISING BLOG..ASANTENI