Zimebakia siku 9 za kupiga kura

Tunapenda kuwa kumbusha wale wote ambao hawajapata muda wa kupiga kura au hawajaamua nani wampigie kura kuwa zimebakia siku 9 tu za kupiga kura kuwachagua washindi katika kila kipengele. Piga kura yako leo kwa sababu kura ni nyingi sana zinazopigwa kila siku. Hivyo tusije anza kuuliza vipi huyu na yule ilikuaje?  Hapa wasomaji wa blogs mbalimbali ndio wanaochakua washindi "Reader's choice". Hivyo jitahidi sana kupigia kura blog/s unazozipenda. Usisubiri watu wenginewafanye hivyo. Onyesha mapenzi yako na uaminifu wako katika blogs unazozipenda..

Tuliamua kuwe majina ya blog  hizi kwa kutumia link zao badala ya titles za blogs hizi ili kama unahitaji kuzielewa zaidi iwe rahisi kucopy na kupaste link ya blog hizo.

No comments: