Malalamiko Yaliyojitokeza Na Kuhusu Kukata Rufaa

Tunataka tueleze baadhi ya malalamiko yaliyojitokeza katika shindano hili. Watu wengi wameuliza uhalali wa blog kadhaa iweje zimeibuka washindi? Na baada ya hizo blogs kuibuka washindi ndio watu wengi wameanza kwenda kuzipitia hizo blogs na kusoma.  Wameona kuwa baadhi ya hizo blogs  "hazizungumzii kabisa hayo mambo kwenye hiyo kipengele iliyoshirikishwa na kujipatia ushindi", "nyingine ni mpya kabisa na hazina post nyingi." au "hazina hadhi ya kushinda".  Sasa sisi hapa tunaweka wazi kuwa kosa sio la hizo blog  kuibuka washindi bali mapungufu hayo ni yetu kuachia blogs kadhaa kuwekwa katika baadhi ya vipengele ambavyo hazikustahili kushirikishwa.



Ushindi wao waliojipatia ni kutokana na marafiki zao kuwapigia kura kwa vile kama ni wasomaji kuna baadhi ya blogs ambazo zilikua ni mpya kabisa na zilikua hazijulikani kabisa. Hivyo ushindi walioupata ni kutokana na marafiki waliokua nao kutoka Facebook kuja kupiga kura kwa wingi.Lakini ukweli ni kuwa zimeshinda kwa kupata kura nyingi.No question about that.Mnakumbuka mwanzoni niliandika post kuhusu Facebook. Watu waliopiga kuna humu  33% wametokea kwenye Facebook.

Lakini pia wote tunatakiwa kukumbuka kuwa sheria za hili shindano hapo mwanzoni ilikua watu wanapendekeza blog wanazotaka zishirikishwe katika kipengele fulani. Na tulitegemea watu watakaa na kuangalia hiyo blog kuwa inastahili kweli kuingia katika hicho kipengele au la lakini baada ya kupokea mapendekezo ya blog hizo, nyingi zilikua hazistahili kuingia katika baadhi ya vipengele hivyo. Kama mnakumbuka tulikua na kipengele cha Best audio blogs ambacho kilihitaji blogs zilizokua kwenye platform ya podcast tu lakini cha kushangaza kuna blogs zilipendekezwa humo bila kujali kuwa blog hiyo sio podcast.

Tulijitahidi kadri ya uwezo wetu kuziondoa katika baadhi ya vipengele na kuziweka katika kipengele tulichofikiria zinastahili zaidi. Na hata baada ya kufanya hivyo tulipokea emails kutoka baadhi ya bloggers wakilalamika kwanini blog zao zilipendekezwa katika kipengele fulani iweje tumeziondoa? Kwa vile kuna baadhi ya bloggers walikua wanapendelea vipengele fulani zaidi na walitaka wawekwe humo bila kujali blog zao zinazungumzia mambo yanayohusu hicho kipengele au hapana.  Ila tulijitahidi sana kuangalia blogs zilizoingia zinahusika katika kipengele hicho ila tuliangalia post zilizopostiwa mbele ya ukurasa tu kwa sku hiyo tulivyokua tunafanya uwakilishi wa mwisho. Tumeona hili na tunaelewa malalamiko yenu kuwa kuna baadhi ya blogs zilislip through the crack na hazikustahili kushirikishwa katika baadhi ya vipengele.

Ila tutapost guideline mpya ya blogs zitakazoshirikishwa katika shindano hili kwa vile hapo mwakani tunategemea kutakua na wadhamini. Hivyo badala ya kupokea badges na vyeti tu vya kushiriki basi kutakua na zawadi. Hivyo tutaweka guidelines ili kila blog inayopendekezwa kama haifikii hiyo guideline basi itaondolewa na haitawekwa kwenye hicho kipengele. Hivyo kama utapendelea blog yako ishirikishwe mwakani basi itabidi upitie guidelines yetu ambayo tutaipost angalau uone ni mambo gani yatakayoangaliwa na ikiondolewa utaelewa ni mambo gani yaliifanya iondolewe. Natumaini lawama zitapungua na washindi wataelewa ushiriki wao na ushindani wao utaongeza imani ya shindano letu. Pia ushindani utakua mkubwa zaidi kwa vile watu watakua na hamu ya kupiga kura kwa wingi ili walioshirikishwa washinde. Kuna baadhi ya vipengele vilivyoshirikishwa kutokana na blogs zilizoingia nyingi hazikustahili kuingia humo nadhani hata watu hawakua na hamu ya kuchagua nani ashinde hivyo pamoja na kuwa kuna washindi lakini kura zilizopigwa zilikua ni chache sana uilinganisha na vipengele vilivyokua na upinzani mkubwa. Hivyo hapo mwakani kila blog itakayoshirikishwa humu pamoja na kupendekezwa na watu itabidi tuangalie kwa makini kama imefuata masharti ya shindano hili. .

Kila kitu kina mwanzo wake ila sio excuse ya kutetea mapungufu yaliyojitokeza na sio kuwa kila blog iliyoshinda hapa haikustahili kushinda ila kuna baadhi ya blogs zilizoshinda zilitokana na mapenzi ya rafiki zao kuwapigia kura.  Mapungufu yaliyotokea ni baadhi ya blogs kuwekwa kwenye vipengele visivyostahili blog hizo kuwekwa.

Vitu ambavyo tumeshaelewa vitabadilika ni kuwa badala ya kushirikishwa blog 10 basi zitakua blog 5 tu.  Hivyo ushindani utakua mkubwa zaidi na itakua rahisi kw sisi kuhakikisha hizo blogs zimefikia kiwango hicho. Hata kama blog yako itapendekezwa mara nyingi lakini kama haikufuata guildlines za shindano hili haitaingia.

Yes, tumeona kuna forum ilipita humu na kupigiwa kura.  Tunakubali makosa hayo and we  apologize for that. Haikuwa nia yetu kushirikisha forum kabisa na zile zilizopendekezwa tuliziondoa lakini ndio hivyo moja iliingia kwenye shindano hili. Tumeona mapungufu hayo na tunakubali hilo ni kosa letu. 

Tunajua kila blog lengo lake pamoja na kutaarafisha, kufurahisha ila juu ya yote hayo ni kufundisha. Hivyo mwakani blog zitakazoingia kwenye kipengele cha elimu ni zile tu zinafundisha kikweli.  Yaani kufundisha watu  kama mwalimu darasani mfano jinsi ya kufanya au  kutengeneza kitu fulani...Blog zinazofundisha jinsi ya kusolve matatizo fulani..Kama unafundisha watu kupika, useremala, kupaint, kuchora,  kufundisha watu jinsi ya kupata kitu fulani, jinsi ya kusolve tatizo fulani, kutengeneza au kurepair gari, Tv, computer etc etc . Sijui inaeleweka yaani kufundisha kweli watu  ndio blogs zitaingia kwenye education. Tulipokea blogs nyingi sana katika kipengele hiki ndio maana blogs zote tuliamua kuzigawanya katika kipengele cha informative lakini mwakani hiki hakitakuwapo sasa kama unataka blog yako iwe iwekwe kwenye hiki kipengele basi itatakiwa iwe hivyo. Education zitakua ni blogs zinazofundisha tu. Kama hakuna blogs zinazofundisha watu basi kitaondolewa.

Na changamoto nyingine tuliyokumbana nayo kama mnavyojua 85% ya blogs za Tanzania ni za habari na burudani. Ila kuna blogs zinajulikana maarufu  kwa breaking news na zingine zinacopy hizo habari kutoka kwenye hizo blogs na kuweka katika blogs zao. Sasa kama mtu anataka blog yake ihusishwe kwenye kipengele cha habari basi habari zako hata kama unacopy na kupaste kutoka kwa blogs au magazeti mengine basi ziwe za theme moja au mbili tu. Yaani ndio kuna blogs zinajulikana kwa breaking news  sasa kama na wewe blog yako ni ya original breaking news basi iwe hivyo lakini wewe kama habari hizo sio zako mwenyewe bali unazicopy na kupaste kutoka kwenye blog nyingine basi kama  wewe unazungumzia habari za uchumi basi iwe hivyo, habari za siasa, habari za wanawake, habari za watoto, habari za michezo, habari za technologa, habari za biashara, habari za kidini, habari za mazingira basi iwe hivyo kwa 90% ya post zako kama unataka ushirikishwe humu. Wale wanao copy na kupaste kila habari inayotokea kutoka kwa blog fulani au magazeti fulani kwa vile itawaengezea traffic hatutazishirikisha kabisa. Ni heri blog iwe na post chache lakini iwe na theme kuliko kuwa na post nyingi zisizo na theme. 

Halafu katika kushirikishwa katika vipengele hivi basi blog hizo ni lazima ziwe zinazungumzia mambo ya kwenye hicho kipengele kwa 90% ya post zao. ...Kama blog yako inagusia kila kitu kidogo kidogo kama tulivyosema hapo juu haitaweza kushirikishwa kabisa. Jitahidi blog yako iwe na theme. Watu wametuandikis kutuomba tuweke directory list yetu katika category lakini tunashindwa kufanya hivyo kwa vile ni blog chache sana za kitanzania zina theme. Yaani ni chache unajua ukiingia  kwenye blog fulani mambo mengi nitakayoyasoma ni ya kuhusu kitu fulani. Lakini nyingine zote zinakusa kila kitu kidogo kidogo sasa inakua vigumu kuelewa hiyo blog uiweke kwenye category gani. Na ndio maana wengine wanashangaa kwa nini pamoja na kublog sana lakini trafic ni ndogio kwa vile blogs nyingi hazina specialization.  Ili uwe na wasomaji wa kudumu unatakiwa uwe unaspecialize kwenye mambo kama mawili au matatu. Kama ni mapishi basi 90% ya post zako ziwe mapishi, kama ni siasa basi 90% ya post zako ziwe siasa, kama ni burudani basi 90% ya post zako ziwe burudani etc etc. 

Na katika kipengele cha photography nacho itakua picha hizo zimepigwa na mwenye blog hiyo au wasomaji wa blog hiyo wamemtumia. Ziwe original na blogs ambayo zinacopy na kupaste picha za kwenye magazeti ya watu wengine hazitahusishwa kwenye kipengele hiki kabisa kata kama hizo picha unazoweka humo ni nzuri sana.

Kutakua na kipengele cha Best Newcomer Blog...Hii ni kuwa blog yeyote itakayokua na chini ya miezi sita itaruhusiwa tu kushiriki katika kipenngele hiki na sio kingine kabisa. Tumepokea malalamiko mengi kuhusu hili na tumeona ni kweli watu walivyosema sio halali blog ambayo ina miezi mitatu na bado haina theme kutokana na post chache zilizomo humo ishirikishwe na blogs ambazo zimeshajulikana zinazungumzia nini na ni za muda mrefu. 

Pamoja na yote hayo cha muhimu tutazingatia sana ni originality. Ndio kubog wengi wanatoa idea kutoka katika blogs zingine na vyombo vingine vya habari lakini tutakua makini sana katika hili. Blog zinazocopy na kupaste habari na mambo yao kutoka kwenye blogs au magazeti mengine hazitashirikishwa. Hata kama unatoa habari mahali pengine ni lazima uwe unaiandika habari hiyo kwa maneno yako mwenyewe. Na kwa post ambayo haiwezi kuelezewa kwa maneno yako mwenyewe basi kama unacopy na kupaste habari hiyo basi ni lazima uweke shukurani (credit)  au link kuonyesha habari hiyo ulikoitoa. Na copy and paste itaruhusiwa iwe sio zaidi ya 10% ya post zako. 

Kuna mambo mengi tutaweka kwenye guidline yetu lakini hayo ndio baadhi na tunatumaini pamoja na kutangaza blogs za watanzania basi tutaweza kusaidia kuongeza ubora wa blogs zetu za kitanzania. Watu wanasema ziweze kuvuka  bahari. Ikiwa na maana zipate wasomaji hata wa nje ya nchi. Kwanini blogs za watu kutoka nchi nyingine na wanablog kutoka nchi zao huku huko waliko ziweze kuwa na wasomaji wengi sana ndani na nje ya nchi yao na za kwetu zisiweze? Tunajua kwa kuelezana ukweli na kuona wapi tunamapungufu basi blogs zetu zitavuka bahari sana tu  bila kujali ni lugha gani hiyo blog zinatumia.

Kama issue ya google adsense. Kuna watu waliniandikia na kuniuliza ni jinsi gani matangazo hayo yanawekwa na kuna wengine wanasema waliapply kwa muda mrefu na hawajajibiwa. Ukweli nilikua sijui jinsi haya matangazo yanavyofanya kazi au ni vipi mtu anapewa hiyo publishing account au yanawekwaje. Hivyo kabla ya kuwajibu ilibidi nianze kutafuta kwenye google na kupata ufahamu wa hili zaidi. Na katika kuchunguza huko nikaona ni blogs nyingi sana za watu wako Kenya, India na Phillipines  wamekubaliwa kuweka. Na nimeona watu wengine wametumiwa check za US $4500 kwa muda wa miezi sita. Sasa nikajiuliza ni kwanini hao walioomba wa Tanzania hawajakubaliwa? Ila tuelezane ukweli hizo blogs nilizoziona na kuna baadhi nimewasiliana nao ambazo wana hayo matangazo zinapata wasomaji wengi wa ndani na nje ya nchi ambao sio raia wa nchi zao tu. Na nyingi ni kutokana na originality ya blogs zao na nyingine wanafundisha watu mambo wanayoyafahamu.. Hivyo kama tukielezana ukweli na kuhamasishana natumaini ni wengi sana watakubaliwa kuweka hayo matangazo. Na ukiangalia ajira zilivyo ngumu kupata sasa hivi kuna vijana wengi wana degree na hata 2nd dgrees lakini kazi zinakua ngumu kupatikana kama unaweza kublog na kutumiwa $4500 kwa miezi sita si itasaidia hata hela ya matanuzi kidogo kuliko yule asiye na blog? Sio kuwa kila mwenye blog basi uanzishe ukiwa na mawazo ya kupata hiyo hela kwa vile ukianzisha blog kwa malengo ya hela hutaweza kuiendeleza hiyo blog kabisa,  lakini kama utakua na blog na kuweza kupata hela ni nini kitapungua zaidi ya kuongeza kukuhamasisha kubog vizuri zaidi?

Hivyo kama baadhi ya watu walivyotuandikia na kusema ni heri kipengele fulani kisiwepo kuliko kiwepo na blog zilizowekwa humo hazistahili kabisa kuingia. Tunakubaliana 100% kuwa vipengele vitawekwa mwanzoni hapa na watu waone lakini kukiwa hakuna hata blog zinayostahili basi kitaondolewa. Ni heri kuwa na vipengele vichache na viwe na blogs zenye kustahili kuingia humo kuliko kuwa na vipengele vingi. 

Hivyo malalamiko yenu tumeyasikia tutahakikisha kila kitu kilichoelezwa tunakifuatilia na kukishughulikia ila walioshinda hili shindano walishinda kwa kupigiwa kura na rafiki au wasomaji wao. Kama ni kukata rufaa basi hilo lingeletwa mwanzoni wakati ule tulipotangaza tu blogs zilizoingia katika ushindani. Ili zisizostahili kuingizwa humo ziondolewe...kumbuka hizi blogs zilipendekezwa na watu mbalimbali.  Mtu akisema anataka kukata rufaa sasa hivi kwa vile blog fulani imeshinda haitakua halali kwa vile kama isingeshinda sidhani kama wangewaza kuwaza kuwa hata hiyo blog ilikuwapo.  Ushindi wao ni kutokana na kura walizopata na kama mtu unakata rufaa ni ili uwaulize watu waliopiga kura ni kwanini wamempigia kura nyingi hivyo huyo blogger wakati blog yake ni mpya na mambo yake mengi hayahusiani na hiyo kipengele iliyowekwa au unataka kutata rufaa kuuliza kwanini hiyo blog ilishirikishwa katika hicho kipengele?

No comments: