Missing Pieces or Missing Links?

Je unajua ni mada gani za blogs zimepungua au hazipo kabisa katika jamii yetu? Kwa vile tunajitahidi kuhamasisha watu kufungua blog ni muhimu tukionyesha wale wanaotaka kuingia kwenye fan hii ya kublog na hawajajua wanapendelea kuandika mambo gani basi hapa ni mwanga kidogo tu wa vitu ambavyo unaweza ukaanzisha blog na kuzungumzia.

Hizi ni orodha ya mada ambazo mimi kwa upande wangu naona bado hazijazungumziwa kwa wingi sana au hazipo kabisa katika jamii yetu. Tafadhali kumbuka kuwa hii sio repoti ya kisayansi na ninafahamu kuwa kuna blog nyingi tu za kitanzania bado hatujafanikiwa kuzipata ili tuziorodheshe kwenye directory list yetu. Hapa kwenye list yetu kwa kuangalia kwa haraka haraka karibu tumeshaziorodhesha kama 50% tu ya blogs zinazoandikwa na watanzania mpaka sasa hivi.

Mimi kama mwandishi wa hili shindano nimeshapitia hizi blog zote kwa zaidi ya mara moja hivyo ninaweza kusema kwa uhakika kuwa mpaka sasa hivi hizi mada zimepungua au hazijazungumziwa na watu wengi. Hizi mada najua kuna wasomaji wengi sana tu wangependelea kusoma mabo kama haya. Kama mtu akiamua kufungua blog na kuzungumzia moja ya topic hizi hapa na kuwa mbunifu kidogo au kuzingatia uhalisi wa blog yake basi hatapata taabu ya kupata wasomaji wakudumu wa blog yake.

Mada hizo ni kama :-

1. Blog zinazozungumzia mambo ya sheria (Sheria za Tanzania)

2. Blog zinazozungumzia mambo ya uzazi (Parenting ya kiafrica au kitanzania)

3. Blog zinazozungumzia mambo ya afya za watoto na watu wazima (Dalili na kinga za magonjwa mbalimbali)

4. Blog zinazozungumzia mapishi (ya asilia)

5. Blog zinazozungumzia harusi/ndoa (jinsi ya kufanya matayarisho mbalimbali ya harusi/ndoa, ideas za kufanya sherehe za harusi au mbalimbali, idea za jinsi ya kupunguza gharama mbali mbali za harusi, list ya sehemu nzuri mbalimbali za kufanyia harusi tanzania etc)

6. Blog zinazozungumzia wanyama wa porini na nyumbani.

7. Blog zinazozungumzia bishara, jinsi ya kuanzisha biashara au kuwekeza katika biashara mbalimbali. (entrepreneur blogs)

8. Blog zinazozungumzia Lishe bora (Nutrition) & Fitness

9. Blog zinazozungumzia michezo mmoja moja kwa undani (tennis tu, wrestling tu, badminton tu, soccer tu, swimming tu, netball tu, basketball tu, riadha tu peke yake etc etc)

10. Blog zinazozungumzia au kufundisha hobby mbalimbali kama ( Useremala, kusuka nywele, mashairi, crocheting, knitting, book club, creative writing, michezo ya kuigiza, mapishi, etc)

11. Blog zinazozungumzia safari (traveling) {mfano blog za kuzungumzia sehemu unayoishi kwa undani na vivutio vilivyopo, au sehemu nzuri kwa watu kutembelea kama honeymooners, familia, wafanyakazi au magroup mbalimbali na mambo mengi yanayohusu Tanzania}

12. Blog za wanawake (apart from love, relationship, beauty, fashion and entertainments) {blog zinazozungumzia afya za wanawake kwa ujumla, kuwawezesha wanawake etc}

13. Blog zinazozungumzia uchumi ( uchumi wa Tanzania)

14. Blog zinazozungumzia jinsi ya kutunza hela (financing), jinsi ya kusave a deals mbalimbali zinazopatikana nchini na pia stock market.

15. Blog zinazozungumzia masoko Tanzania (branding, promoting local businesses, etc)

18. Blog za science na technology.

19. Blogs zinazozungumzia real estate na architecture.

16. Blog zinazotumia video (video blogging)

17. Podcast


Najua kuna mada nyingi tu lakini hizi natumaini kuna watu wengi tu wanavipaji au ujuzi wa mambo fulani hapo juu na wangependa kuwaelezea watu wengine.

No comments: