Check list kabla hujaweka hewani blog yako

Kuna vitu vichache vya kuhahikisha blog yako inavyo kabla ya kuiweka hewani. Vitu hivi ni muhimu kukusaidia ili watu watakaoiona blog yako kwa mara ya kwanza waweze kuikumbuka na kurudi tena. La sivyo wakiona hakuna kitu chochte ni rahisi sana kutotaka kurudi tena katika blog yako.

1. Hakikisha una post kama tano hivi za kuanzia

2. Hakikisha blog yako ni rahisi kusoma na kuona post zako zingine ulizonazo katika blog yako.

3. Hakikisha una RSS katika home page yako.

4. Hakikisha blog yako inaonekana vizuri kwenye browser mbalimbali. Blog inaweza kuonekana vizuri katika brower moja lakini nyingine ikawa haionekani vizuri. Hivyo jaribu kuifungua blog yako kwenye browswer kadhaa ili kuona inaonekana vipi.

5. Jitahidi uwe na social bookmarking kadhaa kwenye blog yako.

6. Andika kidogo kuhusu wewe hata kama unablog kwa jina lingine ni bora kuwaambia wasomaji wako ukweli.

7. Wape watu wasome tena post zako hizo kabla hujaziweka iwe unaandika kwa lugha ya kiswahili au kingereza. Ni rahisi sana kukosea neno au sentence na usiweze kuona mwenyewe. Na kila mara hisia za kwanza ndio zinawafanya watu warudi au wasirudi tena kwenye blog yako. Hivyo jitahidi sana kila kitu kionekane kuwa kimekamilika hata kama utafanya marekebisho, kuengezea vitu vingine au kubadilisha design ya blog yako baadaye hiyo haina tatizo.

1 comment:

Anonymous said...

You guys are doing such a great job.