Uteuzi wa Kupendekeza Blog za Kushiriki Kwenye Shindano Umefungwa

Kama tulivokua tumetangaza hapo awali leo ndio mwisho wa kupokea majina ya blog za kushiriki katika shindano hili.  Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wale wote walioshiriki katika kupendekza majina hayo. Leo kura zilizopendekezwa ni mara mbili ya kura zote zilizopendekezwa toka awali. Tunashukuru sana kwa watu wote walioitikia wito na kupendekeza majina ya blog zao au blog wanazozipenda.  Tutaweka kesho majina ya blog zote zilizopendekezwa hapa na watu mbalimbali.

Jambo tunalotaka kuwakumbusha watu ni kuwa majina hayo yamependekezwa lakini tafadhali  zingatia kuwa hayo majina sio kuwa ndio yameshapita. Tutapitia kila blog iliyopendekezwa na kuangalia kama blog hiyo imekidhi masharti ya shindano letu (soma hapa kuhusu sheria za shindano hili) na pia kama inastahili kushirikishwa katika kipengele hicho. Baada ya hapo tutawasiliana na wenye blog hizo kama watakubali kushirikishwa katika shindano letu basi majina yao yataingia kwenye ushindani wa kupigiwa kura kumtafuta mshindi katika kila kipengele. 

Mwanzo wa kupiga kura ni tarehe 25. 6.2011 

1 comment:

Sikuzani binti wa mzee Majaliwa said...

Mashallaaaah...Praise tha lord !!!

Kila la heri kwa kila mgombea