Je Wafahamu Hili?


Wote tunaelewa kuwa na blog hii tu hapa haiwezi kusahihisha, kufundisha au kuelezea mengi kwenye jamii yetu ambayo ni muhimu sana. Na kama mnavyojua tuko hapa kuhamasisha watanzania wengi kuwa na blog, kujua umuhimu wake na pia kutangaza blogs za watanzania zilizopo tayari. Pamoja na haya yote kuna mambo mengi huwa nasikia tu lakini kutokana na kusimamia hili shindano ninajifunza mengi sana kila siku na pia ninaweza kuwa na ushahidi kamili kutokana na jinsi ninavyona nini kinaendelea hapa.

Watu wengi sana siku hizi wako kwenye social networks. Je ni watu wangapi Tanzania wenye biashara, wenye makampuni, viongozi wa vyama vya kijamii, siasa, dini, au viongozi katika mashirika mbali mbali wana accounts katika hizi social networks? Au hata kama wanazo je ni wangapi wanazitumia ipasavyo?

Jana jumapili nilipata kushangaa sana baada ya kuona kuwa watu zaidi ya 4000 ambao ndio mara yao ya kwanza kabisa kuingia humu wameingia kwenye hii blog. Pamoja na kuwa traffic nyingi imeletwa na watu wanaoshiriki katika shindano hili lakini pia traffic kubwa toka mwanzo ilikua inatokea kutoka Facebook na Twitter. Ukizingatia Facebook Page imefunguliwa si zaidi ya week mbili na Twitter account nayo pia haina muda mrefu na ukiangalia kwenye twitter account yetu mpaka sasa hivi hatuna zaidi ya watu 30 wanaotufuata. Hivyo ni kusema kama una kitu chochote unachoshughulikia unataka kufikisha ujumbe kwa watu mapema au unatafuta masoko ni muhimu sana kuwa na Twitter account na kujihusisha katika hizi social networks.

Ndio unaweza kuwa na account na kujiona kuwa huna wafuasi wengi lakini hilo lisikukatishe tamaa. Watu wengi wanaweza kupenda kujua unachofanya lakini hawataki kujulikana hadharani kuwa wanafuatilia mambo yako kwa sababu zao za kidini, siasa, wadhifa wao na mambo mengine mengi tu wanayoyajua wenyewe. Kumbuka kuwa kama una jambo muhimu, wadhifa ua hata kama wewe ni kiongozi wa chama chochote watu ambao hawakufuatili hadharani ndio wengi wao watakuja kila siku kuangalia unalilifanya kuliko hata wale wanaokufuatilia hadharani. Kama ni biashara wapinzani wako ndio watakua wafuasi wako wakubwa lakini hawatapenda kujionyesha hadharani wanakufuata wewe. Kama ni chama cha kijamii au siasa wapinzani wako ndio watakua wanakuja kuangalia kila siku umepost nini kwenye site yako au umetweet nini. Sasa kama una hizi accounts na unazitumia ipasavyo ujue ujumbe wako utafika mapema sana na kwa watu wengi kuliko hata njia za barua, simu au barua pepe. Kama ni biashara utatangaza biashara yako bila kutumia hela nyingi na kama ni chama cha kijamii au siasa mtakata gharama nyingi sana za kufikisha ujumbe kwa wanachama wenu na wanachama wenu watafikisha ujumbe kwenu kirahisi sana tu. 

Ila kwa kusema tu fungua account sio jibu la mambo yote hayo na  katika kila jambo ni lazima uwe na malengo. Sasa pamoja na kwamba utafungua hiyo page au twitter account jitahidi sana ufuate kilichokufanya kwanza kufungua hiyo account. Kama ni ya matumizi ya binafsi basi iwe hivyo lakini kama umeanzisha kwa ajili ya kutangaza biashara yako, kuuza, au kuwasiliana na wafuasi wako basi mambo ya binafsi usiweke au usitweet kabisa. Mfano umefungua tweet kwa malengo ya kufikisha ujumbe fulani kwa wafuasi wako halafu umekwenda mahali fulani na kufurahia sana na kuamua kutweet  “nipo mahali fulani nakula chakula fulani”. Fanya hivyo tu kama unalipwa kutangaza hiyo sehemu au kama wewe kuna watu wanajali na kufuatilia sana sana kila unalolifanya na kula katika maisha yako kila siku. Kama unafanya mara kwa mara utapoteza ujumbe wako maalumu siku unapoweka. Celebrities wa nchi zilizoendelea wengi huwa wanalipwa sana kwa kutangaza biashara sasa kama kuna baadhi unawafuatilia na kuona wanatweet hivyo sio kuwa wanatweet kwa bure na wewe uanze kuchanganya mambo hayo ya maana katika tweets zako ambapo malengo yako ya mwanzo hayakua hivyo. Kwa kufanya hivyo kama umefungua account na umepata wafuasi kadhaa ujue watu hao wanakufuata kwa yale malengo yako ya mwanzo ukianza kuchanganya hayo mambo yako ya binafsi na yale mambo muhimu ujue tweets zako nyingi zitakua zinapotea bure tu. Siku una jambo la maana la kuwatangazia watu wako basi linapotelea huko huko kwa vile wengine wataona aibu kujiondoa kukufuata kama unafahamiana nao lakini hawatazichukulia maanani tena  tweets zako. Jitahidi kila tweet unayotuma iwe inahusiana na malengo ya twitter account yako. Kwa vile wewe ndio umefungua hiyo account kwa malengo fulani hivyo fuata hilo ili malengo yako yafanikiwe. Na pia kumbuka kama kwenye twetter sio rahisi kujua  anayekufuata ana umri gani, elimu gani, kama wametumia alias account (hujui wadhifa wao n.k) Sasa jitahidi kuwaheshimu wafuasi wako kadri unavyoweza na heshima hiyo itarudhishwa kwako na matokeo yake kama unauza, unatangaza, unawasiliana na wafuasi wa chama chako au kampuni yako basi utajikuta hutumii hela au nguvu nyingi kufikisha ujumbe wako.

5 comments:

Rachel Siwa said...

Ujumbe mzuri!

Anonymous said...

Yeahhh sure

malkiory said...

Ili blogu yangu iweze kuwa kwenye orodha ya blogu za kitanzania inabidi nilipie?

Admin said...

Hapana hakuna chochote cha kulipia kama imekidhi masharti yetu hapo juu wewe tutulemie Link ya blog yako na sisi tutaiweka.

malkiory said...

www.malkiory.com