Kura 1591 zimepokelewa kwa siku ya kwanza

Kura 1591 zimepokelewa leo katika ballot zote zilizo hapa. Tunashukuru kuwa siku ya kwanza imekwenda bila tatizo lolote na tunashurukuru watu wale wote walioshiriki kupiga kura hizi.

Kuna watu wametuandikia na wameomba tuwe tunaweka dondoo ya nani anaongoza kila siku katika kila kipengele lakini hata sisi tutaka iwe surprise for both of us. Hatutaangalia ni nini kinaendelea mpaka mwisho wa kupiga kura.

Kinachosikitisha ni kuwa kuna mtu/watu wachahce bado wanaandika comments za kutukana sana baadhi ya washiriki wa hili shindano na kinachosikitisha ni kuwa kwa vile tuliona matusi hayo mengi yanaachwa na huyo mtu/watu kwa kutumia anonymous basi tukablock hiyo feature. Lakini sasa hivi amefikia kufungua email accounts nyingi au labda anachange jina lake kila baada ya kuacha msg hizo. Najiuliza kwanini?  Sijui na sioni sababu kwa nini mtu mzima akae chini na kutukana watu wengine bila sababu ya msingi matusi ya nguoni hivyo ati kwa vile wao wamekubali kuingia katika hili shindano. Kama kuna mtu anayeweza kunieleza hili basi atuambie na sasa hivi ameona hatupost hizo msg zake za kutukana basi ameanza kutugeukia na sisi..

Sisi hapa hatuna la kumwambia bali tunamtakia/kuwatakia roho njema pamoja na kuwa wanatumia muda mwingi kutukana lakini labda kuna siku watakaa na kuuchunguza mioyo yao na kujua wanalolifanya sio jambo jema. Tuaamini aliye juu yetu ataweza kumsaidia na kumpa roho ya upendo na amani. Roho kama hiyo sio nzuri hata kwa afya yake mwenyewe. Ndio mwanzo wa kujipatia magonjwa yasiyo na sababu. Kuwa na hasira hivyo bila sababu ndio mwanzo wa kuwa na high blood pressure au psychiatry episode bila sababu. It is just sad.  

Enjoy your week end all

2 comments:

Biche said...

It's sad to see the "hating" that's taking place against this competition and its organizers. Although I do not know who is behind this competition nor their intentions in organizing it, I'd like to commend them for doing something positive to create awareness of the Tanzanian blogosphere. Through this competition, I have learned that the Tanzanian blogosphere offers a lot more quality and variety than I had thought previously.

May this be the first edition of many for this competition, and may each edition get successively bigger and better.

Kudos to the organizers for putting a good idea into practice. I take my hat off to you!:-)

Mzee wa Changamoto said...

Hii ni habari ya kusikitisha. KUTUKANA si suluhisho la lile unalopingana nalo. Ni KUJITENGA NA SULUHISHO kwani ukianza kutukana, hata unayetaka kum'badili hatasoma usemayo, na pengine akisoma hatatilia maanani.
Binafsi sikukubaliana na utaratibu mzima wa kupendekeza washiriki, lakini naamini nilikuwa wa kwanza kueleza hilo na kujaribu kutetea hoja zangu hapa kwenye "tab" ya contact (ambayo nadhani mmeitoa) na piua kwenye blogu yangu. LAKINI HAKUKUWA NA MATUSI
Naamini tunastahili kujua kuwa njia pekee ni kujenga hoja ili hoja hizo zijibiwe na kwa kufanya hivyo baadhi ya mambo yatambulike. Kama kuna ambaye anakosea atajirekebisha.
Kwa hiyo kwa wale watukanao nadhani wanalofanya si sahihi. Ni wakati wa kuJENGA HOJA kisha tusonge mbele. Na inapotokea hoja zetu hazituleti pamoja, basi TUKUBALI KUTOKUKUBALIANA. Ndio uungwana huo. Na hata kama hukubali kitu kimoja, haimaanishi kuwa huwezi kupongeza kingine.
BARAKA KWENU NYOTE