Barua pepe kwa washiriki wa shindano hili - 2011

Tulikua tumepanga kuwa kila aliyependekezwa kwenye shindano hili na baada ya kuangalia kuwa blog yake inastahili kuwekwa katika kipengele hicho basi kabla ya kuweka list za washiriki wote watakao pigiwa kura hadharani ni vizuri kwanza kuwataarifu watu wote kipekee ili kama hawataki kushiriki basi tujue na kuondoa majina yao, lakini zoezi hili limekua gumu zaidi kuliko tulivyotegemea. Hivyo kuna watu wengine wameshapokea email lakini kuna wengine bado hawajapokea email kutokana na mambo kadhaa kama haya:-
1. Kuna watu kwenye blog zao hawana contact information yeyote. Nimejitahidi kadri ya uwezo wangu na sikupata kuziona .. Hivyo kuna nadhani mmoja au wawili nilikua nimeanza kupost kwenye comment boxes zao lakini kwa upande wangu niliona kuwa sio vizuri na huwa sipendelei nikitembelea blogs mbalimbali nikiona mtu anatoa comment ambayo haihusiani na post iliyowekwa hapo. Hivyo nikajiuliza kama mimi sipendi kuona hivyo kwanini nifanye hivyo?  Hivyo kwa wale ambao hawana contact info kwenye blog zao wajue labda wamechaguliwa lakini sikuweza kuwapata.

2. Kuna watu wanacontact info kwenye blog zao na nimewatumia taarifa lakini email zao zimerudi kwangu hazijawadeliver .Kuna wengine wameweka auto response na zimerudi, wengine email zao hazifanyi kazi na wengine sijui kwa sababu gani zinanirudia.

3. Na kuna wengine najua labda wana spam detectors/filters sasa kwa vile nimeshatuma email kadhaa week hii kutumia email hii labda filter zao zinaweza kuchukulia email yangu kuwa ni moja ya emails zinazotuma mass emails...Hivyo labda zimewekwa kwenye junk folder.

Hivyo baada ya hayo yote ni kuwa nimeamua nitaweka majina ya finalists wote katika kila kipengele hadharani...Please kama unamfahamu mwenye blog au unajua jinsi ya kuwasiliana naye muambie kuwa blog yake imependekezwa huku katika shindano hili kama hapendi kushirikishwa basi atuandikie tuondoe jina lake kabla ya tarehe 22. Watu wengi wameshapokea ujumbe na hakuna hata mmoja aliyesema jina lake liondolewe mpaka sasa hivi hivyo tunatumaini kila mmoja atachukulia shindano hili vizuri lakini huwezi jua. Na sisi hapa hatupendi kulazimisha mtu yeyote katika kitu chochote. 

Pia tulisema kama blog itapendekezwa kwenye kipengele isichostahili basi itaondolewa lakini kwa mwaka huu wa kwanza tumejitahidi sana majina yote yaliyopendekzwa kwenye vipengele ambavyo havikustahili hatukuyatupa kapuni. Tumejitahidi kuangalia hiyo blog inafit kipengele gani zaidi na huko inachance ya kuwin kuliko mahali ilipokua haistahili.  Kwa mfano kama blog ilipendekezwa kwenye best photography blog lakini haina hata picha sasa kuliko kuitupa kapuni tumejitahidi kuiweka kwenye kipengele tunachoona inastahili zaidi na mambo mengine kama hayo. 

Na kama sheria ya shindano ilivyosema blog iliyopendekezwa mara nyingi ndio zitachaguliwa lakini kuna watu wachache waliingia siku ya mwisho ya kupendekeza majina ya blog kwenye vipengele vingi back to back mara nyingi sana lakini ukiangalia walichagua vipengele vingi sana bila kujali kweli hizo blog zinastahili kuingia hapo au la? Hivyo pia hatukuzitupa kapuni blog hizo bali tumejitahidi kuziweka katika kipengele zinachostahili. 

Nadhani tumeelewa...


2 comments:

Anonymous said...

KUNA BLOG KAMA BONGO STAR LINK UNAIWEKA KATIKA NAFASI GANI

John aka J2

Anonymous said...

sio haki itendeke bali ionekane ikitendeka, michuzi anatisha kwa siasa na dj choka anafuatia kwa burudani, wengine ni kama 8020 kwa fashion, Othuman kwa mtaa kwa mtaa, kwa kweli kuna blog zingine hapo ndio kwa mara ya kwanza nazisikia ambazo sidhani kama zinafikisha hata watu 100 kwa siku kwa kutizamwa. kama mnataka mashindano haya yawe ya haki basi chagueni group lenu na mkague blog zinazotizamwa sana au zinazopata views kwa wingi ili hata wale wachanga wajifunze kitu. nihayo tu ndugu zangu