Umuhimu Wa Kuitangaza Blog Yako Kila Siku Upatapo Nafasi

Kutokana na maoni, maswali na malalamiko ya wengi nimeona ni muhimu kuweka hii post ili watakaoisoma labda watajifunza jambo moja au watafaidika kidogo. Haya ni mawazo yangu mimi kama msimamizi na mwandishi mkuu wa shindano hili na wala hayahusiani na watu wanaotangaza bidhaa zao humu au wanaoshiriki katika mashindano yetu kwa namna moja au nyingine. Haya ni kutokana na emails na comments ninazozipata kila siku toka tumeanzisha hili shindano.

Watu wengi wanafikiria kuwa kwa sababu wana blog na labda ina mambo mengi basi inajulikana sana. Ukiwa na blog up and running haimaanishi kuwa utapata wasomaji wa kusoma blog yako mara moja au kwa vile blog yako inapata 1000 hits kwa siku haimaanishi kuwa blog yako inajualikana na kila mtu. Watu wengi wananitumia email na kulalamika kwanini sijaiweka blog hii au ile kwenye Directory List yetu. Wengine wanafikia hata kusema blog zao ni mashuhuri sana kwa nini sijaziweka kwenye Directory List yetu mpaka sasa hivi. Sasa cha muhimu ni kuwaambia watu wote wanaoblog, hata siku moja usiache kuitangaza blog yako kwa vile unaona una hits 1000 au zaidi kwa siku. Kwanza hizo hits hazimaanishi kuwa ni number ya watu waliotembelea blog yako hiyo siku. Hiyo inamaanisha number za pages zilizofunguliwa katika blog yako kwa siku hiyo. Hivyo kama mtu mmoja ameangalia post mbalimbali ndani ya blog yako na pia kama amehit the refresh button hata kama ni kwenye ukurasa huo huo basi hit counter itakua inaongezeka tu. Anaweza kuondoka na kusoma vitu vingine na baadaye kurudi tena kwenye blog yako hit counter itaongezeka. Na mtu huyo huyo anaweza kurudi kusoma blog yako kila siku na hata mara zaidi ya moja kwa siku. Hivyo hizo 1000 counts zinaweza zimetokana na watu 100 tu au pungufu. Hivyo unatakiwa ujue hili hata siku moja hit counts 1000 sio kuwa watu 1000 wamesoma blog yako kwa siku hiyo.

Na pia watu wengine wanafikiria kuwa kwa vile blog zao zinajulikana sana na watu fulani au na kundi fulani basi wanafikiria kuwa kila mtu anaijua. Blog yako inaweza ikawa maarufu mahali fulani lakini bado kuna watu hawaijui mahali pengine. Inaweza ikajulikana sana nchi fulani lakini haijulikani nchi nyingine. Hivyo usiache kuitangaza blog yako kila unapopata nafasi. Tukichukua mfano wa makampuni makubwa na mashuhuri kama Pepsi au Nike ambayo wengi wetu tumezaliwa na kuzikuta hizi brands. Ingawaje zinajulikana sana lakini kila mwaka wanatenga fungu la kutumia katika matangazo ya bidhaa zao. Sasa kwa watu ambao hawajasomea biashara itabidi ujifunze kitu kimoja hapa. Kampuni kama hiyo ambayo wewe unafikiria kila mtu anaijua kwanini inatumia hela zake nyingi tena katika matangazo? Si wangeacha tu kwa vile watu wengi wanazijua? No!!!! Katika ulimwengu wa biashara na mfanya biashara wa kweli hata siku moja hatakiwi kufikiria kuwa kwa vile kitu chake anachouza ni maarufu basi hana shida ya kutangaza tena.....Lazima kuna mtu mmoja atakua hajui na hata kama akiwa anajua basi kuna ushindani wa bidhaa nyingine hivyo unatakiwa uwakumbushe wateja wako umuhimu wa biashara yao au kama umebadilisha vitu kadhaa katika biashara yako. Msomaji wa blog yako ni kama mteja wako unatakiwa umkumbushe mara kwa mara na uweshimu. Ingawaje labda blog yako ni kwa ajili ya kufundisha au kutangaza lakini bado ujue kuwa hao watu unaotaka kuwafundisha ni vizuri kuwaheshimu hata kama unajua kuwa unachokiandika kinawanufaisha.

Hivyo ili usikate tamaa ya kublog, mwanablog yeyote anayetaka kufanikiwa anatakiwa juhudi zake za kutafuta vitu vya kuweka katika blog yake viende sambamba na juhudi za kutafuta jinsi ya kutangaza blog yake kila siku. Bila hivyo utaishia kuwa unablog tu peke yako tu kila siku. Kila unapojitangaza hata ukiongeza mtu mmoja kuifahamu blog yako ni heri kuliko ungekaa tu kimya.

Baada ya hayo ninalotaka kukwambia ni GOOD LUCK kublog sio kazi rahisi lakini ni very rewarding thing to do. Na kila siku ukumbuke kublog iwe funny au topic unazo blog uwe unazipenda kama huenjoy au hupendi topic unazoziblog humo hutafika mbali bora uache.

No comments: