Jinsi ya kuanzisha blog

Hii ni kutokana na emails nyingi tunazozipokea hivyo tumeamua kuweka hii post hapa. Kama mtu unayesona hii topic una blog na ungependa kwasaidia watu wengine basi tafadhali copy na uweke kwenye blog yako.

Nimejaribu kuandika kwa Kiswahili kama watu walivyoniomba sasa kama kuna kitu nitakosea au nimeacha basi naomba usiache kuniandikie ili nisahihishe.

Kuwa na blog ni bure na hamna kitu ambacho unatakiwa kulipia zaidi ya muda wako utakao tumia kwenye internet. Kama unataka kuwa na jina lako binafsi mfano www.Tanzania.com na kuhost wewe mwenyewe basi hapo ndio utatakiwa ulipie lakini kama blog yako itakua kama http://tanzania.blogspot.com basi hutalipia chochote. Na kama wewe ndio unaanza tu kublog na hujajua unataka kublog nini basi ni vizuri kutumia blog host za bure mpaka hapo utakapoelewa zaidi na kama ni kutaka kuipeleka blog yako mbali zaidi basi utajua mwenyewe hapo baadaye. Na faida ya hizi blog za bure ni kuwa unaweza kubadilisha jina la blog yako wakati wowote kama hilo jina unalotaka kulitumia bado halijatumiwa na mtu mwingine.

Blog zinaweza kuwa katika platform kadhaa kama:-

Blogger - www.blogger.com

Wordpress - www.wordpress.com

Typepad - www.typepad.com

Posterous - www.Posterous.com

Letterdash - www.letterdash.com

Tumblr - www.tumblr.com

Sasa mimi hapa nitaandika maelekezo ya jinsi ya kuanzisha blog kwa kutumia platform ya blogger.com ambayo naiona ndio rahisi sana kwa mtu yeyote kutumia na ambaye hana ujuzi mwingi lakini hii ni kwa mawazo yangu tu. Unaweza ukaenda kuangalia hizo zingine zinaweza zikawa kwako ni rahisi kuliko hii hapa.

Nenda hapa www.blogger.com

Utaona mahali panasema “Create Your Blog Now"


Kama huna google account basi jaza maelekezo hayo hapo juu. (Gmail account)






Kama una account bas
i pita haya maelekezo na kutumia “sign in with existing account”


Ipe jina blog yako..Kama hutumii jina lako basi jitahidi jina hilo liwe fupi na liwe linaendana na vitu utakavyoweka kwenye blog yako.


Tafuta design unayotaka iwe katika blog yako.



Umemaliza sasa na wewe unablog yako


Andika post yako ya kwanza na kama unataka kuweka picha basi kuna hiyo button ya tatu kutoka kulia ndio inayotumika kuweka picha. Na hizo picha lazima uwe nazo kwenye hard drive yako au kama unataka kulink zilizopo kwenye internet tayari basi hiyo ndio itakuwezesha kufanya hivyo.




Natumaini haya maelekezo yatawasaidia wale waliokua wanataka kufahamu jinsi ya kuanzisha blog.

2 comments:

Feel At Home said...

Sisi 2meshaanzisha y kwetu bt 2nataka kulisajili jina letu isije m2 akali2mia hapo badae je 2fanyeje.

Pauline said...

Hey kuhusu hilo hapo yapo mambo kadhaa ya kufanya.
1. Nchi unayoishi sheria za copyright au trademark zinasemaje? Hivyo unatakiwa kusajili kwenye vyombo vinavyotumika kushughulikia hayo mambo.

2.Kama ni jina lako kwenye internet mimi kwa experience niliyonayo ni kuwa kila muda wa kurenew unatakiwa ufanye hivyo mapema sana au uwe na hela za kuajiri malawyer wakupigania hilo jina kama limechukuliwa na mtu wa nchi nyingine ndio hivyo tena. Naona sheria nyingi za mitandao haziruki mipaka kabisa au bado kabisa kwenye mambo haya. Hata kama umeTM logo na jina la biashara yako nchi fulani na unaiweka kwenye internet mfano www.watoto.com lakini likiisha muda wake kwenye hiyo kampuni ulioregister nao kama huta renew mapema nakwambia mtu mwingine wa nchi nyingine anaweza kulichukua just like that..Kama ni biashara ndogo tu ni vigumu kufuatilia au kuajiri lawyer wa kukupigania...

Ila kwa watu kuiga mambo yako unayoyaandika kwenye inernet kuna hii site http://creativecommons.org wao wanaweka lincense lakin sijui kama inazijumlisha nchi zote au inahusu vipi kwa international laws.