Njia mbalimbali za kutangaza blog yako

1. Taja jina la blog yako popote pale unapoweza kama kuwaambia marafiki zako, kujiunga kwenye social networks kama Twitter, Facebook n.k. Pia weka jina la blog yako kwenye signature ya email yako, na kama una kadi za biashara basi usiache kuitaja kwenye kadi yako kama hiyo kadi sio ya kikazi au kama unaruhusiwa kufanya hivyo na kazi yako basi usiache kuweka jina la blog yako.

2. Peleka blog yako mahali popote penye Blog Directory List au kama kuna mahali pa kuisajili basi iandike. Usisiste kufanya hivyo...kila unapoona mahali kuna list za blog peleka maombi yako na usisubiri wao ndio wakutafute.

3. Omba watu wenye blogs mbalimbali wakutangazie blog yako na kama unafuatilia blog zao ukiona hawajaiweka usikate tamaa kuwaandikia tena. Na ufanye hivi kwa utulivu sio kuwalalamikia watu au kuwalazimisha watu. Kumbuka wewe ndio unahitaji msaada na sio wao na pia ujue kuna bloggers wana ratiba za mambo ya kupost katika blogs zao. Wengine ni ijumaa tu ndio wanapost maaombi ya kila mtu na wengine hata mara moja kwa mwezi tu. Sasa kama hujui ratiba ya hiyo blog au huifuatilii ukituma maombi yako tulia na usubiri hata kwa week kama mbili ndio hapo ujaribu tena kupeleka maombi yako. Ukiwa uanalazimisha kila siku au ukituma maombi yako leo halafu kesho unategemea yawe yamewekwa na usipoona unatuma tena email , utawaudhi watu na mwishowe hawatakuwekea blog yako kabisa. Hivyo uwe na subira....

4. Pitia blog mbalimbali zenye mambo yanayofanana na blog yako na uache comments kwenye blog zao. Lakini uache comments za maana au zinazosaidia na zinazohusiana na topic zilizo kwenye blog yako. H ivyo watu wanaosoma hiyo blog kwa vile interest zao ni sawa na za wasomaji wa blog yako basi wachache wanaweza kuja kusoma blog yako na kama wakikuta mambo mengi wanayapenda basi umejipatia wasomaji wapya.

5. Kama kuna blog umeona mahali inatopic zinazoendana na blog yako na unaweza kuweka link ya blog yako basi fanya hivyo. Ila tricky hapa ni kuwa badala ya kuweka link ya blog yako weka link ya post unayoona inafanana na hiyo blog unayosoma au link ya topic unayoona ni nzuri au ina hits nyingi katika blog yako. Usiweke url ya blog yako yote kila mahali...ukiweka post tu mtu akisoma akavutiwa basi anaweza kupendelea kusoma zaidi blog yako lakini ukiweka Url ya blog na mtu akiingia anaweza akutane siku hiyo kwenye blog yako na vitu ambavyo sio anavyovipenda basi haitakua rahisi kwa yeye kuendelea kusoma blog yako au hata kuikumbuka tena.

6. Mwisho na muhimu ni kujitahidi kila siku kuandika post zako ambazo zina manufaa kwa wasomaji wako. Najua hii haihitaji a rocket scientist kuvumbua lakini ukweli ni kuwa kama post zako sio za muhimu kwa watu wengine hautakua popular na watu hawatajali kukumbuka blog yako. Utakua unapata watu wa kupita tu kila siku lakini watu wakuikumbuka kwa kichwa blog yako, kuibookmark au kumbuka kufungua blog yako kila mara wanapopata muda hautapata kabisa. Kama unacopy habari za watu wengine ambazo wameshazitangaza kwenye blog zao nani anajali? Kama wewe ni wakuelezea jinsi siku yako ilivyokua chuoni kwako, kazini kwako au jinsi ulovyospend weekend yako nani anajali? (Labda kama wewe ni mwandishi mzuri ) na ukielezea unaandika kwa lugha ya kuvutia watu bila hivyo utakua unapoeteza nguvu tu hata huko unakojitangaza itakua nihasara tu. . Jitahidi kuandika mambo ambayo ni muhimu lakini sana sana jitahidi kuandika mambo yako yawe unique na organic na watu wote watakukimbilia kila siku mara wakishaifahamu blog yako kutaka kujua kesho kutakua na nini??????

No comments: