Kama nilivyosema katika post iliyopita badges na certificates zote nitaziweka hapa hivyo zote zipo hapa. Kila mtu achukue ya kwake hapa hapa. Nimejaribu kuweka kwa original size kama mtu anashida ya kupunguza badge yake na hajui jinsi ya kupunguza aniandikie nitamsaidia kupunguza kwa size anayoitaka.
Sitatuma tena certificate au badge yeyote katika email accounts za watu hivyo kila mtu cha kufanya ni kila mtu kudownload ya kwake hapa kwa urahisi. Nimejitahidi sana kuhakikisha viko sahihi but always a fresh set of eyes helps. Kama unaona nimekosea jina au nafasi yako katika ushiriki naomba uniandikie nitarekebisaha hayo kabla hujadownload cheti chako.
1. Naomba usome huku kwenye blog kama jibu hujapata ndio uniandikie swali. Maswali mengi ninayoyapokea majibu yake yapo humu.
2. Kama nilivyosema kila mtu anachotakiwa kufanya ni kudownload cheti chako hapa havina tofauti yeyote na mimi kuvituma katika email account.
3. Vyeti nilivitengeneza na kuupload hapa vikiwa katika original size. Nilivitest katika A3, A4, A5, B5, letter, legal & executive size papers. Hivyo ukidownoad make sure unasave katika original size ili kama unataka kuprint uweze kuprint katika paper ya size hizo bia matatizo yeyote.
4. Kama unataka nikutengenezee badge katika size yako unayotaka tafadhali ukiandika katika heading andika "badges". Email account hii inapokea emails nyingi sana kwa siku na sina muda wa kufungua kila email inayoingia. Hivyo heading inayoonyesha kuwa unahitaji kuresize badge yako itakua rahisi kwa mimi kuiona. Na kwenye subject niambie ni kiasi gani au unipe blog yako na wapi unataka kuiweka ili niangali kuwa ni size gani. Ukiandika tu "nipunguzie kidogo" siwezi kujua kidogo kwako ni kidogo kiasi gani?
5. Mwisho wa kupokea emails za kutaka kupunguziwa badge au jambo lolote kuhusu shindano la mwaka huu ni Nov 30th.
6. Sorry, siwezi kuvituma hivi vyeti kwa mail kwa wale walionitumia anuani zao sitaweza kufanya hivyo.
7. Kwa wale wanaotaka kuja kuvichukua Dar pia hawataweza kufanya hivyo kwa sababu siishi Dar- Es-Salaam au Tanzania kwa sasa.
Shukrani sana kwa wote walioshiriki, wote wale waliopendekeza blogs mbalimbali na wale wote waliochukua muda wao wakati wa kupiga kura.
1 comment:
Twakushukuru sana mpendwa kwa juhudi zako hizo, ubarikiwe sana, hatuna cha kukulipa, ila mungu pakee ndiye mlipaji, na ni matumaini yetu kuwa mwakani unaweza kuja na jipya, hatujakata tamaa na wewe.
Post a Comment