Mwisho wa Kupiga Kura ni 9/15/2013

Jamani mlikua wapi? Emails 127 leo tu! Really?

1. Hatupokei tena mapendekezo ya blog sasa hivi. Huu ni muda wa kupiga kura.

2. Wanaolalamika kuwa kuna blogs zimeingia kwenye vipengele visivyohusika sijui walikua wapi wakati wa kupendekeza hizo blogs wanazoona zinatakiwa kuwa katika hivyo vipengele?

3. Mwaka huu hii site niliyotumia kupiga hizi kura haiwezi kuweka hizi ballots kwenye blog kama kipindi kile hivyo nimeweka kila kipengele katika front page....Na pia zipo kwenye Facebook. Ni ballot hizo hizo....Hii front page itakaa hivi hivi kwa week hii ya kupiga kura. Hivyo ukiingia hapa ukifuata hiyo link utaona ballot ya kipengele unachohitaji.

4. Wanaotaka niweke hii link ya hizo blogs ili waziangalie na kuzicompare wakati wa kupiga kura cha kufanya ni kucopy and paste utaweza kuingia kwenye hizo blogs bila matatizo yeyote. 

5. Ili upige kura huhitajiki kusign up wala nini... Wewe fuata hiyo link upige kura yako....Sio pretty ballots but do the job just perfect.....Na uuri ni kuwa hatukublock IP hivyo katika office moja wote wanaotaka kupiga kura wanaweza kupiga kura....

5. Wanaotaka muda wa kupiga kura uongezwe jibu ni NO NO. NO Hatutaongeza muda wa kupiga kura kabisa....


1 comment:

emu-three said...

Na uuri ni kuwa hatukublock IP hivyo katika office moja wote wanaotaka kupiga kura wanaweza kupiga kura....

KWENYE OFISI YETU HII HAIKUBALI, MMOJA AKISHAPIGA KURA WENGINE HAWAWEZI KUPIGIA KURA COMPUTA HIYO, INASEMA `UMESHAPIGA KURA YAKO..'