Wow Wow Wow !!!

Okay tupo karibu na mwisho wa kupata wa wakilishi wote lakini mambo machache tuliyoyaona katika blog zetu  na naona labda tukiweka hewani tutawasaidia wale ambao hawaelewi kuwa ni tatizo au mapupungufu kidogo ambayo yanaweza kuwapunguzia wasomaji. Kwa sababu haya ndio yametudrug nyuma kidogo.Pamoja na kuwa blogs zilizopendekezwa wakati huu ni nyingi sana lakini haya yamechangia kwa kiasi fulani pia kuchukua muda kupitia blogs hizi.

1. Punguzeni gadgets..
Hizo gadgets ni nzuri ukizitama lakini zinachangia kwa wingi kupunguza wasomaji wa blog yako kila siku. 
a) Kuna gadgets ambazo zinatrack back au zinakuwa na matangazo. Sasa kwa watu wenye powerful spams and antivirus protector software kwenye computer zao hawawezi kufungua blog yako kwa ajili ya hizo gadgets.
b) Hizo gadgets nyingi zinachangia blog yako kuwa slow sana..Sasa kama blog itafanikiwa kufunguka inakua slow sana.


c) Gadgets zinaengeza kelele kwenye blog yako. Ukipunguza makele kwenye blog yako basi watu watakumbuka contents za blog yako. Mtu akiingia kwenye blog na kukuta vitu vingine vinavyomfanya aache kusoma yaliyo kwenye blog yako na kuanza kuangalia vitu vingine. Ndio inaweza kumfanya msomaji akae kwenye blog yako kwa muda mrefu lakini hasara ya kwako ni kuwa anaweza asisome kile kilochompeleka kwenye blog yako sasa badala ya kujiengezea msomaji unakuta unapoteza kwa vile kuna watu wanastumble kwenye blogs tofauti kila siku lakini wakisoma na kuona kitu cha maana watakumbuka hiyo blog lakini hizo gadgets haziwezi kumfanya mtu ambaye aliyepotea njia tu na kukuta blog yako na kurudi tena...

Kikubwa ni kukumbuka kuwa  hizo gadgets nyingi zimetengenezwa na watu walioko kwenye western countries au zinatumiwa na makampuni wyaliyoko nchi hizo kama sponsors. Wanakupa wewe bure lakini wanawapata wasomaji wako sasa wewe huko Tanzania blog yako inaweza ikifunguka hakuna pop ups yeyote lakini kwa watu wanaoishi kwenye targeted countries ni usumbufu sana na hizo zitawafanya watu watakimbia blog yako. Gadgets hizo ni za bure but remember there is no free lunch and if there is, you are a  product..Jitahidi kuweka chache au tafuta amabzo ni usniversal hizo zinakua hazina matangazo na spams nyingi.

2. Kwa wele wenye matangazo tafuta jinsi ya kuyapunguza size  Kama ni jpg punguza size kwa vile yanachangia kufanya blog yako iwe slow sana..Halafu jaribu kuyaweka upande ili mtu akiingia kwenye blog yako aone contents za blog yako. Blog unafungua unakutana na matangazo kibao hata hujui tangazo lipi ni lipi hata kama una contents nzuri zinaweza kuchangia watu wasirudi tena kwenye hivyo blog unless blog yako watu wanajua wanachokipata humo ni muhimu. Let us learn from waanzilishi wa hii tasnia. Mbona wao wanaweka matangazo lakini yameekwa vizuri na kwa utaratibu ambao unafanya msomaji asiwe turned off. Yapo lakini hayawai mlango wa kukukaribisha. Kama tunataka tufike kwenye anga za kimataifa blocking people na matangazo hivyo haitasaidia. 

b) Kwa mtazamo wangu watu wanaoingia kwenye hii site 80% kutoka Tanzania wanatumia simu sasa kama blog iko kwenye format ya simu ina maana hayo matangazo hayaonekani na mtu anayetakiwa kumfikia (mtu aliye Tanzania). Sasa ukiyaweka yakiwa madogo na kwa utaratibu haitakupungusia chochote bali kuengeza watu na hata walio nje ya nchi watafaidi blog yako pia..Kwa vile wakiingia kwa kutumia computer na kukuta vikwanzo hivyo vingiii...watakua hawana hamu ya kurudi tena kusoma hiyo blog.

3. Kuna watu blog zao font ni ndogo sana. Yaani ni font ndogo halafu ni italic....Hii ni turn off kwa msomaji .. jaribu kuangalia hili linaweza kukupunguzia sana wasomaji hata kama una contents za maana lakini kama watu hawawezi kusoma hamna faida..Usitumie fancy fonts kama uko serious. Hata kama unataka kupata younger readers fancy fonts zitakupunguzia wasomaji. Kwa vile fancy fonts ni kwa sentesi mbili tatu lakini palagraphs kadhaa na fancy fonts ni turn off

Okay hayo ni kwa leo ..Kesho majina yatakua tayari..

Good luck to all

3 comments:

emu-three said...

Nashukuru sana mpendwa,umenipa shule ambayo itanisaidia sana, ngoja niangali hizo gajeti...!

Gasper Sambweti said...

Nashukuru kwa elimu hii ya leo naamini nitafikia malengo yangu kwa kufuata hayo machache uliyoeleza ubarikiwe sana

Gasper Sambweti said...

asante sana kwa maelezo naamini kwa kufuata hayo nitafikia malengo yangu ubarikiwe sana