Kwa wale blog zao ambazo hazikuingia mwaka huu

Please tambua kuwa this is not the end of the world. Kumbuka kuna mwaka kesho. Kama blog yako haikuingia mwaka huu basi inawezashiriki mwakani Mungu akitujalia..Mambo ya kuandika email za hasira na matusi just because blog yako haikuingia that is just too low. Ina maana blog yako ingeingia usingefikiria hivyo unavyofikiria sasa hivi kuhusu shindano hili? People please!!!!

Kama unafikiria kuwa sijui tumeingiza blogs za watu tunaowajua PROVE that..Sio longolongo tu hapa na kuongea vitu bila kuwa na ukweli wowote. Kusema vitu bila fact is just too old. You know 2012 bado unafikiria mambo hayo? Well sisi wote tulioangalia hizi blog hatumjui mtu yeyote in person mwenye blog Tanzania au nje ya Tanzania. Sasa unavyosema hivyo ni kuwa hujui unalolisema.

Sisi hapa hatupo kwa ajili ya blog fulani au kumpromote mtu mmoja tu..Kwanza is just a big insult to us..badala ya kutumia muda wetu wa ziada kufanya mambo yetu  tunatumia kufanikisha hili shindano, kujibu maswali hata pia kusaida watu wenye shida  mbali mbali kuhusu blog zao halafu unasema tunawapromote sijui watu gani...We are here for all Tanzanians na tunajitahidi kadri ya uwezo wetu to do the right things na tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kusaidia blog za watanzania wote kuwa promoted na kuangalia jinsi gani tutasaidiana kuengeza quality...

Sasa kama mtu anayesema ametumia hela kutengeneza blog yake vizuri kwa ajili ya shindano hili halafu tumeondoa kipengele cha best designed/graphic designed blogs, kwanza labda hujasoma sheria za shindano hili. Tulisema vipengele vitakavyokosa blogs za kushiriki au kuwa na blogs chache tu zilizoqualify kushiriki tutakiondoa. Sasa sijui unacholalamika ni nini. Na pili kwa nini unatengeneza blog yako vizuri tu kwa ajili ya shindano tu? Quality is not an act, it is a habit..

Na pia kuna mtu ameandika kuwa anaomba blog yake tuihamishe kutoka kwenye kipengele kimoja na kuipeleka kwenye kipengele kingine. Hatuwezi kubadili blog yako kuweka kwenye kipengele unachotaka ishindaniwe. Kama unafikiria blog yako inahusu mambo fulani basi jitahidi kuzungumzia mambo hayo kwa wingi hivyo mwakani ukiipendekeza na ikapita kweli tukiangalia tuone kuwa inastahili kweli kuwekwa katika kipengele hicho..



1 comment:

Anonymous said...

mbona sehemu ya kupiga kura hatuioni?