Maswali yaliyojitokeza

Kuna watu wengi bado wanatuma maswali yao kwetu kuhusu directory list na shindano letu. Mengine naona nawajibu na kumalizana nao lakini maswali mengine naona yanajirudia rudia tu. Hivyo hapa ni kwa ufupi kwa wale wote wenye maswali.

1. Kama blog haiko kwenye directory list yetu inaruhusiwa kushiriki?
Jibu: Directory list yetu ni kwa kila mtanzania yeyote popote pale alipo ulimwenguni. Kutokuwapo kwa blog fulani katika directory list yetu ni kuwa bado hatujaifahamu au kutumiwa link. Ukituma link tutaiweka na kushiriki katika mashindano letu pia ni kwa kila blogger mtanzania nje au ndani ya nchi.

2. Kwa nini ni vipengele vitatu tu vinaruhusiwa kujazwa?
Jibu: Hii ni kuhakisha kuwa mtu anapendekeza blog kwenye vipengele ambavyo hiyo blog post zake inazungumzia kwa ujumla. Mwaka jana shindano letu theme yake ilikua kuhamasisha watanzania wengi kuona umuhimu wa kuwa na blog na umuhimu wa kutumia social networks mbalimbali kutangaza blog zao. Mwaka huu theme yetu ni umuhimu wa specialization katika hii blogging sphere ili kujipatia wasomaji wa kudumu (loyal readers).

3. Nini faida za kushiriki katika shindano letu?
Jibu. Shindano letu faida yake ni kukusaidia blog yako kujulikana kwa wingi  ili ujipatie wasomaji wengi kila pande ya ulimwengu. Sisi hatumlazimishi mtu yeyote kushiriki katika shindano letu. Tupo hapa kuhamasisha na kuweza kusaidia bloggers wa kitanzania mahali popote na ni wale tu watakaopenda. Na pia hapa ni mahali pa kuziona blogs nyingi za watanzania kwa urahisi. Kutokana na shindano letu la mwaka jana tunafurahishwa sana kila siku tunapopokea emails kutoka kawa bloggers mbalimbali ambao walishiriki katika shindano hili au walikua featured katika blog yetu wakitupa shukurani kuwa blog zao zimeweza kujiongezea wasomaji kwa wingi. Na pia wengine wanasema traffic ya blogs zao zinatoka kwa directory list yetu. Sasa sisi tupo hapa kwa ajili hii....kuwatambua, kuwapongeza bloggers na kuwasaidia bloggers hao kutangaza blogs zao bila kuingia gharama yeyote. 

4. Je mwandishi wa blog anaruhusiwa kujipendekeza katika shindano letu?
Jibu. Ndio mtu yeyote anaruhusiwa kujipendekeza. Kama uonaovyo form yetu haina njia ya kujua ni nani anapendekeza blog fulani. Hivyo kila mtu anaruhusiwa kupendekeza blog yake au ya watu anaotaka waingie katika blog hii. Unaweza kupendekeza mara nyingi upendavyo kwa vile watakao pata kura nyingi ndio watakaoshiriki lakini kama hiyo au hizo blogs zinahusika kweli katika kipengele zilizoshirikishwa. Sio kuwa hata kama blog haihusiki katika kipengele fulani lakini kwa vile imependekezwa mara nyingi basi itashiriki la hasha...eg..ukiangalia kwenye kipengele cha audio/vodeo blo/podcast kuna blogs nyingi zimependekezwa na zinaendelea kupengekezwa lakini ukiiingia kwenye blog hiyo hakuna hata kitu kimoja kinachohusiana na hicho kipengele. 2nd kama umeona sheria za shindano letu kuwa blog ambazo ni mpya (6 months or less) zitaruhusiwa kushiriki kipengele cha newcomer tu. Sasa kuna blogs zimependekezwa kama newcomer na vipengele vingine pia .Hilo litapitiwa kwa uangalifu na kujua haki inatendeka kwa wote wanaoshriki

5. Kwanini haturuhusu watu wasio watanzania lakini wanablog kuhusu Tanzania kushiriki?
Jibu: sisi shindano letu ni la watanzania na si la Tanzania. Hapa ni kwa wale watu ambao ni watanzania wawe wanaishi Tanzania ua katika nchi nyingine. Blog zao ziwe zinazungumzia mambo mengina na ya Tanzania pia. Kwa wale ambao sio watanzania lakini wanablog zao zinazungumzia mambo ya Tanzania hatukutaka kuwashirikisha kabisa kwa vile tunaamini wengi wao ni Tanzania expertise (TX). Wakiwa Tanzania wao wana uwezo wa kuweza kujitangaza wenyewe kupitia sehemu mbalimbali na wanakua na advernatage ya kujitangangaza kupitia nchi wanazotoka. Ndio maana tuliamua kuipa shindano letu jina la Tanzanian na sio Tanzania. Ila kwa wale ambao ni Tanzania citizens lakini ni wa asili ya nchi nyingine wanakaribishwa pia kushiriki ila cha muhimu ni kuwa blog zao ziwe zinazungumzia kwa wingi Tanzania na so nchi wanazotokea. Well, hatutadai mtu atuonyeshe passiport yake humu kama mtu mmoja alivyoniuliza "Nitajuaje mtu ni raia wa Tanzania au sio raia?" Sisi tutaangalia hiyo blog inazingumzia Tanzania kwa ujumla au la..Tuko hapa kwa malengo mazuri na sio kubagua watu...for the love of the country you are more than welcome to participate.

6. Je watu watajiunga vipi na umoja wa watanzania?
Jibu: Sisi jina letu tumelitumia kwa kuwa blog zetu ni za watanzania ila hatuhusiani na umoja wa bloggers wa Tanzania kama upo. Hivyo swala la uwanachama wa Tanzania hatulijui. Ila karibuni inakuja aggregator ya bloggers na news za Tanzania hivyo wote watakao penda blog zao ziwe linked na aggregator hiyo ni lazima wawe members ndio wataruhusiwa kuadd blog zao...

7. Mtu akitaka kusponsor shindano letu afanyaje?
Jibu,. Mwaka jana baada ya mafanikio mazuri ya shindano letu tulipata maombi na emails mbali mbali kuulizia jinsi ya kusponsor. Hatukutaka kukimbilia haraka haraka kuanza kushirikisha wadhamini ukizingatia shindano hili linashirikisha watu waliopo katika nchi mbalimbali. Na sheria za kutransfer hela zinatofautiana katika kila nchi. Hivyo tuliamua kuacha kwanza mpaka hapo tutakaporegister as a (LLC)  na pia kufahamu itakuaje  na ni jinsi gani tutawafikishia washindani wote zawadi zao. Hivyo kwa sasa hivi tunashukuru sana kwa moyo wenu lakini hatupokei mchango wowote kutoka kwa mtu binafsi au shirika lolote.
.

3 comments:

Unknown said...

Asante sana kwa maelekezo yenye maana sana kwa bloggers !!

emuthree said...

Hapo imekaa sawa

Unknown said...

Nimependa majibu yako,
ubarikiwe sana.