Nominations Form

Wow! Tunashukuru wale wote waliokwisha kuanza kujanza form. Mwaka huu inaelekea kutakua na blog nyingi sana zitakazoshiriki kuliko mwaka jana. Watu waliokwisha jaza form hii ni wengi sana. Tunafurahi kwa hilo. Ila kuna wanaoniandikia kuwa hawaioni form..Nitaiweka kwa jina la kiswahili hapo pia lakini form itakua ni hiyo hiyo.

Jambo lingine ukiwa kwenye site yetu tafadhali pitia directory list yetu uangalie blog za watanzania zilizopo huko kwa sababu kuna blog nyingi sana za kitanzania ambazo ni nzuri sana. Blog hizi zina mambo mengi mazuri ya kufundishana, kuhabarishana na kufurahisha. Huwezi jua nini utakiona na kukifurahia katika blog hizi. Na pia ukipitia blog ya wengine na kuacha message humo unajiengezea trafic kwa blog yako na unayemwachia message anafurahi umuhimu wa message yako. Ni win win situation...Ila juu ya yote utajifunza mengi sana kupitia bloggers wa kitanzania. Na pia kama ukiona blog yako haiko katika directory list yetu usisite kututumia link tutaiweka. Kama umechange link pia utumie tuweke link mpya. Huwa tunadelete site ambazo haziko active kila baada ya miezi sita ila ili usipoteze wasomaji wako ni bora unapotuma link mpya mara tu baada ya kubadilisha. 

Pia bado tunaweka kila week featured Blogger. Kama unataka blog yako ijulikane huu ndio wakati wa kuwa kwenye spot light kwa vile traffic ya blog hii kwa kipindi hiki imekwenda juu sana. Watu wengi sana wanaipitia hapa sasa hivi. Na sisi kazi yetu hapa ni tunajitahidi kadri tuwezavyo kuzitangaza blog zetu za kitanzania. Na tunapokea mtu yeyote anayetaka blog yake kuwekwa hapa.

One last thing ni kuwa jana nimetuma email kwa bloggers wote nilio na email addresses zao lakini kama emails 30 zimesharudi back mpaka sasa hivi..Non delivered, zingine email account hazifanyi kazi tena etc etc. Sasa kama hujapokea email usifikirie tumechagua baadhi ya bloggers tu kuwatangazia na wengine tumewaacha hapana. Wote nimewatumia kwenye address nilizokua nazo bali ni kuwa email addresses nilizonazo na kama iko active basi ndio wamepokea ujumbe. na kama unataka tuweze kukuupdate kila mara tutumie email yako tutaiweka kwenye database yetu.. 

Shukrani

1 comment:

Unknown said...

Ok, my email carternixl7@gmail.com