Zoezi la kutuma badges na certificates limeanza

Tunapenda kuwaambia wote kuwa tumeanza kutuma badges na vyeti kwa washiriki, washindani na kila mtu aliyeshiriki katika shindano hili kwa njia moja au nyingine. Zoezi hili limeanza jana na tunategemea litamalizika Jumapili. Hivyo kama hutapokea email kutoka kwetu mpaka Jumatatu basi ndio utuandikie. Kama hujawahi kuwasiliana na sisi basi email tunayotumia ni hiyo iliyopo kwenye blog yako.Kama huna email kwenye blog yako basi wasiliana na sisi utupe email yako au kama ukiangalia kwenye Junk folder yako hapo Jumatatu na kutoona email kutoka kwetu basi utuandikie. 


Inachukua muda kidogo kutuma kwa vile hizi zimetengenezwa kwa kila mtu pekee kwa hiyo ni lazima kutuma kila email peke yake. Na tumeanza na walioshinda na tunaendelea mpaka mwisho.

Tumeshamaliza kutuma emails kwa washindi wa kwanza. Ila kuna baadhi ya bloggers hawana email kwenye blogs zao. Contact information zao ni za kutumia form au hakuna. Hivyo siwezi kutuma hizi maelezo kwa kutumia contact form iliyopo kwenye blog. Sasa kama blog yako ilishinda nafasi ya kwanza katika kipengele chochote na hujapata email kutoka kwetu mpaka sasa basi wasiliana na sisi.
Kwa wale walioandika na kutaka kujua kama kuna uwezekano wa kupata hard copies za vyeti hivi, ni kuwa tumemeviweka kwa  JPEG format ili mwenye kutaka kuprint basi afanye hivyo. Mwakani tutaangalia uwezekano wa kumtumia kila mtu cheti chake kama anataka kwa njia ya posta.
Na kuna mwingine ametaka kwa format ya PDF...Well, tutaangalia uwezekano wa kufanya hivyo lakini kwa wanaotaka hivyo itabidi wasubiri mpaka tuhakikishe kila mtu ameshapata badge yake ndio tutafuatilia hilo.

Pia tunapenda kuwashukuru watu wote wanaochukua muda wao na kutuandikia. Tunataka kuwaambia asanteni sana kwa maneno yenu mazuri na emails zenu zinatupa moyo na kujua tulilolifanya limefundisha, waonyesha na kuwafurahisha wengi. Tunashukuru sana na tunafurahia sana kusikia kutoka kwenu na kuona jinsi manavyotushauri ili kuboresha shindano la mwakani. Tunajua itachukua muda kujibu email ya kila mtu lakini elewa kuwa tunashukuru sana na haya yote yasingeweza kufanikiwa kama sio ushirikiano tulioupata kutoka kwenu.

Na kwa wale wanaotaka kufanyiwa mahojiano nasi basi usisite kututumia email au kama unataka tufanye mahojiano na mwanablogger fulani basi tuandikie. Tutakua kila mara tunaposti mambo mengi yanayohusu blogs na wanablogger wakitanzania. Hivyo mahojiano yako na sisi yatazidi kuengeza exposure ya blog yako.

1 comment:

ally M said...

1st runers up nao watapata hivyo vyeti? sababu mie blog yangu ilikuwa 1st runners up.