Majibu Ya Baadhi Ya Maswali Yaliyojitokeza

1. Ni jinsi gani tunachagua watu wa kuwafanyia mahojiano?
Ukweli ni kuwa mwanzoni tulituma maombi kwa baadhi ya blogs tulizokua tunazifahamu. Kuna wengine walijibu na kukubali kufanyiwa mahojiano hayo na wengine hawakujibu. Ila baada ya hii blog kujulikana kidogo tunafurahi kusema kuwa sasa hivi tunapata watu wanaotuma maombi ya kufanya mahojiano hayo na sisi. Na pia kuna baadhi ya wasomaji wa blogs kadhaa wanatuma maombi kama tunaweza kufanya mahojiano na mwenye blog fulani. Hivyo tunatuma email kwa mwenye blog hiyo akikubali basi sisi tunatuma maswali ya mahojiano yetu. Kila mwaswali tunayotuma na yakirudisha huwa tunasoma natukiona yamejazwa bila kupoteza maudhui ya blog hii tunayapost. Ni mtu mmoja tu mpaka sasa hivi ndio tuliondoa baadhi ya majibu yake na tulivyomrudishia ali ahakiki na kukubali kuwa hivyo ndio tutakavyopos basi hajatujibu mpaka leo. Lakini tunashukuru watu wote wanaoomba au kukubalia  kufanyiwa mahojiano haya wote madhumuni yao ni mazuri kama tunavyotegemea.

2. Ni vigezo gani tumetumia kuteua washiriki wa shindano hili?
Kama mnavyojua hawa washiriki hatukuteua sisi. Tuliweka form ya kupendekeza washiriki wa shindano hili hapa kwenye blog hii. Kwanza tuliweka kwa mwezi mmoja na nuse halafu kuna watu walitushauri ili tuengeze japo wiki moja kwa vile kua wengi walikua bado hawajapata taarifa. Basi sisi hatukuengeza wiki moja tu bali tuliengeza muda wa wiki mbili tena. Hivyo form hiyo yakupendekeza washiriki ilikua hapa kwa mtu yeyote kupendekeza blogs alizokua anataka zishiriki hapa kwa muda wa miezi miwili. Hivyo ukiona blog yako unayoipenda haipo hapa ni kuwa hukuchukua muda wa kutuma mapendekezo hayo kwetu. Kama hukuweza kupata taarifa hii kwa muda wa miezi miwili tuliotumia kutangaza na kuwaachia watu wajaze hii form basi ni bahati mbaya lakini kama uliiona na hukuchukua muda wako kujaza form hiyo ukitegemea watu wengine wataipendekeza hiyo blog basi nayo hiyo ni bahati mbaya pia. Ila hii pia iwe fundisho kwa wengi wetu ambao tunaona kitu badala ya kujituma na kufanya tunakaa kimya na kutegemea mwingine atafanya. Na kisipofanyika kitu au kikifanyika kwa kutofikia ubora wa malengo yetu basi tunakua wa kwanza au wepesi sana kulalamika.  Wanasema "If you don't vote, you can't complain". Kama ungetuma blog yako uliyotaka ishiriki ni lazima tungeiweka kwenye list zilizopendekezwa. Hakuna  hata blog moja ambayo ilitumwa kwetu kwa muda uliokua upepangwa au kujaza form zilizokua hapa tuliacha kiorodhesha. Tulisema watu wanaoacha mapendekezo yao kwenye comments hatutazipokea lakini tulizipokea ambazo zilikua zimewekwa kwa muda uliokua wa kupendekeza. Tuliingia kwenye spam folder na kuona kuna wengine wametuma emails zao na zilikua huko na pia tuliziorodhesha majina yao waliopendekeza kwa muda ule. Hii ni kusema wanaolalamika wana lao jambo au ni watu waliozoea kulalamika tu. 

3. Ni vigezo gani vilitumika kuwateua washiriki wa mwisho wa shindano hili?
Washiriki wa mwisho wa shindano hili kama tulivyoweka mwanzo ni kuwa blog ambayo ilikua imependekezwa zaidi katika hicho kipengele ndiyo ingeingia kwenye ushindani. Lakini matatizo tuliyoyapata ni kuwa baadhi ya watu walikua wanajaza form hizi bila kujali kuwa je hiyo blog inastahili kuingia katika hicho kipengele kweli au la? Na pia katika siku mbili za mwisho kuna mtu/watu waliamua kujaza hizo form kwa blog kadhaa tu katika kila kipengele kwa mara zaidi ya 15 hadi 20.  Hivyo kama tungekubali na kuweka hizo blogs tu basi kungekua hakuna ushindani mwingine katika kila kipengele na ingeharibu maana ya shindano hili. Hivyo tulichofanya ni kuchukua kila blog iliyopendekezwa katika kipengele fulani bila kujali imependekezwa mara ngapi. Nikatuma haya majina kwa wenzangu waanzilishi wa blog hii. Na kila mmoja alitakiwa kufungua blog iliyopendekezwa katika kila kipengele na alochotakiwa kufanya ni kwa kuangalia post zilizokua mbele ya ukurasa kwa siku hiyo tu. Blog zilikua nyingi na hatukuwa na muda wa kuangalia posts za nyuma zilikua zipi au zinazungumzia nini. Hivyo kwa kuangalia ukurasa wa mbele wajaze wanaipa hiyo blog number gani kwa kuhusiana na hicho kipengele iliyoshirikishwa. Na number ilikua 1 mpaka 10. Baada ya wao kujaza hivyo kwa kila kipengele walinirudishia. Walichuku wiki moja kuangalia na kunirudishia na mimi nilichofanya nikujumlisha tu hizo number kutoka kwa watu hawa 6. Baada ya kujumlisha iliyopata numba za juu katika kila kipengele ndiyo iliyoingia kwenye finalist. sasa mambo ya kuandika email na kuuliza kwa nini blog yangu haikushirikishwa katika vkipengele hiki na hiki ukweli ni kuwa siwezi jua ni nini hao wenzangu waliona au hawakuona kuwa blog yako inastahili kuingia katika hicho kipengele.  Sisi hatuishi mji mmoja hivyo hizo grade zilikua annonimous.


4. Mbona ni baadhi ya watu wachache tu ndio wamepokea barua pepe ya kupewa hongera za kuteuliwa kushiriki katika shindano hili?
Ni kweli tulikua tumeamua kila mtu aliyechaguliwa kushiriki katika shindano hili atapokea taarifa kutoka kwetu ili kama atapenda jina lake liondolewe basi aweze kufanya hivyo kabla ya uchaguzi kuanza. Wakati ninapitia blogs hizi nilikutana na matatizo kadhaa ambayo baadhi yake yalinifanya niachie hilo zoezi njiani. Kwanza ilikua shida sana kupta contact information za baadhi ya blogs. Kuna watu wengi sana wenye blog lakini contacts information zao sio rahisi kuziona au wengine hawajaziweka kabisa. Baada ya hapo kwa baadhi yao tuliofanikiwa kupata contact information zao tulianza kutuma lakini wengine email tulivyokua tunatuma basi zingine zilirudi kama undelivered, zingine zina auto response na zingine email zilikua hazifanyi kazi. Sasa wakati nafanya hivi na naona emal zinanirusia ndio nikaamua kuacha na kupost kueleza watu kwa ujumla kwa watu wote hapa. Hivyo sio kweli tulichagua baadhi tu ya watu kuwapongeza na kuacha wengine kama watu wengine wanavyofikiria. Kama hukupokea email kutoka kwenye labda sikuona email yako, email ilirudi au nilikua bado sijatuma kwa vile baada ya kutuma email kama 30 hivi na kuona hayo matatizo nayapata kutoka kwa watu wengine nikaamua kuacha.

Tanzanian Blog Awards Team






1 comment:

Anonymous said...

Thanks kwa majibu yako ...
Vote for www.bongoflavortz.blogspot.com