Jamani ehee Watanzania Tupendane

Hapa tumejitahidi sana kuweka kila comments zinazoletwa na watu wote ili kuleta usawa na kuelimishana katika kila jambo. Toka tumeanzisha hii site hatujawahi kuacha kuweka comment yeyote zinazoletwa humu lakini zilizoingia leo zimenifanya nijiulize who are we and what have we become? Usitegemee utapitia kwenye hii site na kuacha comments zako zenye chuki kwa wanablog wengine ukitegemea tutazipost humu.  Hapa sio mahali pa mambo hayo. 
Hata hatujapost majina ya watu walioingia kwenye finalist basi wengine wameshaanza kujaza comments zao zisizo na malengo mazuri kwa majina yaliyopendekezwa humu. Kwa taarifa yako kama ni mtu mmoja au ni watu wengi tunakueleza ukweli kuwa  unapoteza muda wako wakuandika wala usitegemee kuwa tutaweka comments yeyote inayomdhalilihsa mwanablogger yeyote humu. Kama utatudhalilisha sisi tuliyoandaa hili shindano so be it lakini hatutatumia platform hii kuweka chuki baina ya watu binafsi na wanablog wengine au fulani. Kama wewe hupendi blog zilizopendekezwa hapa na haukuchukua muda kupendekeza hizo unazozipenda kaa kimya au tafuta platfom nyingine uweke mambo yako huko. 

Hapa hatutaendekeza watu wa siasa waje na siasa zao hapa, watu wa udini waje na dini zao hapa wala ukabila. Hapa wote sisi tunasimama kama WATANZANIA kama hupendi hilo tafadhali hapa sio mahali pako pa kupitia. 

Thanks na natumaini ujumbe utakua umekufikia au kuwafikia.

6 comments:

Anonymous said...

safi sana na kweli kabisa usiruhusu au msiruhusu hali hiyo kutokea kwa sababu itakua inaleta ubaguzi nimependa sana uamuzi mliofikia kama wapo wenye ujinga huo walioufanya washindwe

Evarist Chahali said...

Ndugu waandaaji wa tuzo,binafsi nina ombi moja tu kwenu nalo ni kutotilia maanani vikwazo mnavyokumbana katika wazo hili bora kabisa.Naamini bloogers wengi na wasomaji kwa ujumla wanasapoti wazo hili zuri lakini life always has its fair share of skeptics.Tumezowea sana mawazo imported kiasi kwamba mawazo ya Kitanzania na/au ya Watanzania wenzetu yanaangaliwa kwa jicho la wasiwasi.

Good news is,laiti wazo hili lingekuwa bovu kama baadhi ya skeptics wanavyojaribu ku-suggest,wala msingekumbana na hao wanaojaribu kuwavunja moyo.Mti wenye matunda bora ndio unaorushiwa mawe.

Anonymous said...

Really good post!

Admin said...

Asante kwa maneno yenu ya mazuri. Tulikua tunajua mengi yatasemwa kuhusu hili shindano na tulikua tayari kwa lolote lite lakini sikutegemea hata siku moja kuwa watu watakuja hapa kuanza kusema maneno ya dharau kwa wanablogger wengine waliopendekezwa kwenye hili shindano.

Hatupo hapa kwa hilo kabisa na wala hiyo sio nia yetu kukusanya wanablogger ili watu wengine wapate mahali pa kutoa depression zao. Kama hao walioandika hizo comments kama ana/wana blogs basi waende huko huko kwenye blog zao wakaandike hayo waliyoyaandika au kwenye blog ambazo zitaruhusu comments kama hizo. I think we are better than that and when you know better you do better..That is what I personal believe.

Mwanasosholojia said...

Hizi ni changamoto zisizo na mashiko, na binadamu ndivyo tulivyo. Msikatishwe tamaa. Binafsi niliona mnajali pale mlipokubaliana na maoni ya baadhi ya watu kwa kuongeza muda wa shindano. Hili kwangu nililichukulia kama busara kubwa na nia ya dhati ya kutaka kujenga. Keep it up, ukisikiliza kila mtu katika dunia ya sasa unaweza kushindwa kufanya mengine ya maana. Sisi hata kama tutatengwa, tupo tayari kushiriki, na waamuzi ni wasomaji wa blog zetu, wakiwemo hao ambao wanapinga. Tupo pamoja!

Anonymous said...

kwanza nawaapongeza sana kwa hii kitumlianzisha. hongereni saana. pili, hao wanaochonga bila kuwa na sababu kuntu watakuwa wamechakachuliwa kwani siku za kupendekeza zilikuwa za kutosha na tena zikaongezwa lakini hawakupendekeza blogu wazipendazo. mwisho, nawasihi timu nzima ya Tanzanian blog awards kuwa msivunjike moyo na watu wachache wenye roho mbaya na chuki zisizo na msingi, kazi mnayoifanya sisi wadau wenu tunaithamini saana tu. pamoja sana. Mungu Ibariki Tanzania.