Mwisho wa kupendekeza blogs za kushiriki umeongezwa

Kutokana na maombi ya wengi ambayo tumeyapokea. Tumeongeza muda wa kupendekeza majina yatakaoshiriki katika mashindano yetu. Hivyo tarehe ya kutuma majina ya blog hizo umebadilishwa kutoka tarehe 31 May 2011 kwenda tarehe 10 June 2011.

Tunataka kuwaambia watu ukipost habari za tangazo letu tafadhali usikose kutwambia ili turudishe fadhila.
Pia sasa hivi tumeamua logo ya shindano hili ni hii hapa...Kuna nyingine tulitengeneza mwanzoni lakini hii ndio tumeichagua kwa sasa. Sasa kama ukipost habari za shindano hili tafadhali tumia picha hii.

Pia kutokana na blog mbalimbali zimepost hili shindano letu na tumeona kuna maswali ambayo hayana majibu kwenye comments zao. Na sisi kwa vile hatutaweza kupitia kila blog iliyopost maelezo na kuwaelewesha watu. Hapa nitaweka majibu ya maswali baadhi nimeona yameandika najua kuna mengi lakini hatujaweza kuyaona. Ila kama una swali usisite kututumia.

1. Kuna mtu amesema kuwa shindano letu haliwashirikishi watanzania wanaoishi nje ya nchi. Hiyo siyo kweli kabisa.

2. Shindano letu ni kwa blog zilizoandikwa kwa kiswahili tu. Hilo sio kweli pia

3. Tunapendekeza wenyewe majina ya watu watakao shiriki katika shindano letu. Hio sio kweli kabisa.

4. Sio kila blog itakayowekwa kwenye Directory list yetu. Hilo sio kweli...Ukituletea blog yeyote iliyoandikwa na mtanzania mahali popote pale alipo ulimwenguni tutaiweka. Ili mradi hiyo blog inaweza kusomwa na mtu yeyote. Blogs ambazo hatuziweki huku ni zile ambazo waanzilishi wa blog hizo wamezifunga na wanahitaji msomaji wa blog hiyo awe mwanachama wa blog hiyo kabla hujaweza kusoma "members only blogs".

6 comments:

Anonymous said...

Nimefurahi kuona mmeongeza muda. Hii itasaidia watu wengi wataweza kuona na kushiriki. Mnatakiwa mtangaze matangazo yenu kwa wing zaidi pia.

Ally Shaaban Mgido's said...

Nimepost Tangazo Habari Njema Kwa Wanablog Mwisho Wa Kupendekeza Blogs Za Kushiriki Umeongezwa!!

LINK:http://allyshams.blogspot.com/2011/05/habari-njema-kwa-wanablog-mwisho-wa.html

Pauline said...

Kweli tumeona watu wengi wametuandikia kuwa walikua hawajalisikia hili tangazo ndio maana tumekaa tukaona sio vibaya kuongeza muda zaidi wa kupendekeza.

Asante @allysham...Ninatengeneza sehemu ya kutoa shukurani zetu kwa watu wote wanaotangaza shindano hili...

NAJUA WAJUA said...

Blog hii imetuma tangazo la kusogezwa mbele tarehe ya kupendekeza majina ya blog shiriki.

Pauline said...

Thanks so much!! Nitaweka blog yako kwenye supportive community..Asante sana kwa ushirikiano wako..

Anonymous said...

Nimeona nominated blogs kwenye kipengele cha Entertainment na sijaona blog ya Bongocelebrity.com.In my opinion it is the best in that category naomba kui-nominate.