Mahojiano Na Blogger Dina Ismail

Leo nafurahi kuwaletea mahojiano yetu na mwanablogger Dina Ismail wa Mama Papiro Blog ambaye pia ni mwandishi wa habari za michezo na burudani katika kampuni ya Free Media. Asante Dina kwa ajili ya kuchukua muda wa kufanya haya mahojiano. Kwa kuanza unaweza kutuambia kidogo kuhusu wewe na blog yako?

Jina langu halisi ni hilohilo Dina Ismail, blogu yangu ndiyo hiyo mamapipiro. Pamoja na habari za michezo huwa kuna habari za kijamii ingawa si kwa kiasi kikubwa kama zile za michezo na burudani


Je, wewe kazi yako ni kublog tu au hii ni kama kazi ya ziada au unafanya kama kitu ukipendacho cha kupitisha muda?

Hapana mimi kitaaluma ni mwandishi wa habari za michezo na burudani nikifanya kazi katika kampuni ya Free Media inayochapisha magazeti ya Tanzania Daima na lile la michezo la sayari. Naweza kusema pia blogu pia ni sehemu ya kazi kwani kupita blogu hii ama za wengine inaweza ikawa chanzo cha habari zetu.

Jinsi gani ulianza kublog na kwa nini?

Nilianzisha blogu yangu nikiwa na lengo la kuwapa habari mbalimbali na hasa zile za kimichezo zinazotokea ndani na nje ya nchi. Pia ni kama maktaba yangu na wengine kwani kuna kipindi unahitaji kumbukumbu ya kitu fulani unaweza kupata kupitia blogu yangu.

Na ni kwa miaka mingapi sasa umekua ukiblog?

Mitatu

Nini changamoto unazozipata kwa kuwa na blog?

Changamoto nyingi nakumbana nazo mfano kutoweza kupata ama kuweka taarifa muhimu. Pia kuna wakati ninakuwa natingwa sana na majukumu ya kikazi kiasi cha kushindwa kuweka habari ndani ya blog. Aidha, wakati naanza kazi hii nilikuwa napata shida ya vitendea kazi kama kamera, kompyuya na hasa jinsi ya kuweka habari, lakini nashukuru mungu nimeweza kupambana na hali hiyo na sasa mambo yapo sawa. Pia kutokana na uelewa mdogo wa baadhi ya watu kuhusu blog, wamekuwa wakizilichukulia blog zote kama mitandayo inayodhalilisha utu wa binadamu mfano ule wa ze utamu.

Unafanya nini wakati ukiwa hushughulikii hii blog yako?

Kama nilivyoeleza hapo juu mimi ni mwandishi wa habari hivyo muda mwingi nakua kazini na pia na mimi mama hivyo nikiwa nyumbani nina majukumu ya kifamialia.

Ni mara ngapi unafikiri juu ya blog yako wakati uko mbali na kompyuta?

Mara nyingi tu, lakini nakuwa sina jinsi kwa sababu najua hata nilipo ni sehemu ya majukumu yangu ya kila siku ambayo najua ni lazima kuyafanyia kazi , lakini kwa blogu najua naweza kuifanyia kazi wakati wowote nitakapopata nafasi hata usiku wa manane.

Ni nani wasomaji wa blog yako?

Wasomaji wangu ni watu wote wanaoongea lugha ya Kiswahili walio ndani na nje ya Tanzania wanaopendelea kufuatilia habari za michezo mbalimbali nchini. Kwa vile mimi ni mwandishi wa habari za michezo na burudani hivyo asilimia kubwa ya mambo ninayoposti kwenye blog yangu ni hayo. Ila walengwa wangu wengi ni wale wanaopenda habari hizi za burudani na michezo lakini hawataki kusoma kwenye blog ambayo ina flash nyingi.

Je ni mitandao gani mingine ambayo unatumi ili iweze kukusaidia kuitangaza blog yako ili iwafikie wasomaji walengwa wa blog yako? Mfano Twitter au Facebook.

Du, zipo tofauti kama kuna zile unawapa taarifa watu unaokutana nao, udhamini wa maonyesho ya muziki ama urembo, ku-linkiwa katika baadhi ya blog za ndani na nje.

Nini hasa ni changamoto kubwa wakati unatengeneza post ya kuweka kwenye blog yako na kwanini?

Kwa vile blog yangu inahusu habari za michezo na burdani zinazotokea kila siku, changamoto yangu ni muda tu. Kutokana na mjakumu ya kikazi na kifamilia sasa muda wa kuweka habari kwenye blog ndio mchache.

Unafanya nini iwapo kuna wakati huna la kuandika kwenye blog yako?

Aisee haiwezekani ukakosa cha kuandika, kwa bahati nzuri kazi yangu inaniwezesha kutokaukiwa na cha kuweka katika blogu yangu.

Je ni nini mkakati wako na blog yako kwa ujumla?

Ni kuleta mapinduzi makubwa kupitia tasnia hii ya blog, pia kuhakikisha inajulikana na kupata wasomaji wengi ndani na nje ya nchi kama ilivyo ya Michuzi, namaanisha ukiwauliza watu kuhusu blogs basi yangu iwe ndani ya top ten.

Je ni bora kupata ukweli au uchunguzi wa jambo unalotaka kuliandika kwenye blog yako wewe mwenyewe au kupitia mtu mwingine?

Ndio, kama ilivyo taaluma yetu huwezi kuandika taarifa bila kuwa na uhakika nayo, pia kuna wengine hawapendi taarifa zao kutolewa katika blog hivyo inabidi kufuata miongozo. Kwa kifupi blog ni kama chombo cha habari kama ukiweka vitu vya kupotosha ni lazima kitaleta matatizo.

Ni jambo gani bora blogger anaweza kutoa kwa wasomaji wake?

Kubwa ni taarifa bora ambazo zitaisaidia jamii kwa ujumla.

Ni jinsi gani (mtu) anaweza kuelezea style ya yako unavyo blog?

Kwa wapenda taarifa za habari za michezo na hasa zile ambazo hazijatoka katika magazeti basi kupitia blog hii watazipata mapema.

Ni nini imekuwa mkakati wako kwa ajili ya kujenga kujulikana kwa mwenyewe na blog yako?

Kama nilivyoeleza awali njia nyingi nazitumia kuhakikisha blog yangu inajulikana, nashukuru kwa hilo matunda yameanza kujulikana.

Je ni bloggers wapi ambao wewe unawaangalia na kufuata nyayo zao? Na kwanini?

Issa Michuzi, John Bukuku, Mzee wa Changamoto, DJ Choka, Bongo Celebrity, na nyingine kwa kiasi chake. Hawa wameweza kujipatia umaarufu na hasa wasomaji wengi hivyo kuwa na mitandao mingi ya kutumiwa habari, natamani siku moja niwe kama hawa.

Hebu tuambie ni watu gani umewahi kukutana nao wakati ukisughulikia post za kuweka kwenye blog yako?

Ni wengi sana kama unavyojua kazi yangu najkutana na watu wengi ingawa si kila ninayekutana naye ama ninapokwenda lazima niweke taarifa zao kwenye blog.

Je unafikiria kuwa unadaiwa na mtu akiacha comment/s kwenye blog yako?

Ndiyo kwa sababu kuna nyingine zinasaidia katika kuboresha.

Je kunadhamani kujibu comment iliyoachwa kwenye blog yako wakati ukijua kuwa huyo aliyeiandika labda hatarudi kusoma jibu lake tena?

Inategemeana na aina ya comment, ila nyingi huwa nazijibu kupoitia mails zao, pia najua ni lazima ataipitia sababu huwezi kutoa comment katika blog usiyoifuatilia.

Je, umewahi kufikiria kuacha kupost comment ambayo iko negative kwako na ukijua hamna mtu atakayejua?

Ndiyo nimeshafanya hivyo tena mara nyingi tu kwa sababu kuna nyingine zinakuwa si nzuri kwangu ama kwa watu ninaowaweka humu ndani ambao ni watu wanaotuzunguka katika jamii.

Je unazitreat tofauti au unafikiri watu wanaoacha comment kwenye blog yako na kuacha majina yao yaonekane wazi wanastaili comments zao kujibiwa au hata kuacknowledge kuwa umeona maoni yao?

Inategemeana na aina ya comment/s walizoacha.

Je, unafikiria ni makosa kucomment kwenye blog yako mwenyewe kwa kutumia jina lingine?

Hapana! Wakati mwingine inasaidia kuanzisha mjadala. Na kwa watu wanaochangia maoni yako kwa kuficha majina ya siwezi kusema kama ni kosa ama la kila mtu ana uhuru wa kuandika anavyojisikia, kwa wenye nia njema wanaweka majina lakini kwa wale wa malengo mwngine mara nyingi mwingine ni lazima wafiche majina yao.

Je unazichukulia comments zote sawa unazotumiwa kwenye blog yako bila kujali maoni uliachwa?

Inategemea.

Je, unaamini comments kwenye blog yako zilizoandikwa kwa urefu sana zinahitaji kuzawadiwa zaidi kuliko zile zilizoandikwa kwa ufupi tu?

Inategemea, kuna mtu anaweza akaandika ujumbe mfupi ukawa na maana na kuna mtu anaweza kuandika maneno mengi na yakawa pumba.

Je wewe ni mtu ambaye uko rahisi kukata tamaa?

Hapana, mimi ni mpambanaji wa hali ya juu ndiyo maana pamoja na kukumbana na misukosuko wakati ninaanza sikukata tamaa nimeendelea na mpaka kufikia hapa nilipo.Pamoja na kufika hapa bado kuna bloggers wengine baadhi wamekuwa hawataki kutoa ushirikiano na wenzao kitu ambacho si kizuri katika harakati za kusaka maendeleo katika tasnia hii.

Ikumbukwe kuwa kuna blogs nyingi zilianzishwa zimeshindwa kuendelea.

Je unaedit picha zako ili ziwavutie sana wasomaji?

Hapana mimi picha ninayoipata huwa naiweka hivyo hivyo ili mradi ikidhi maadili.

Je unaepuka kuweka post ambazo ziko very controversy kwasababu ya kuogopa watu hawatakubaliana na wewe au huna hizo post?

Hapana kitu ninachoweka humu ni kwenye blog yangu ni kile ambacho ninaamini haziwezi kuleta matatizo katika jamii. Huwa kutokana na kazi yangu ninazipata hizo controversial stories lakini kuziweka ama kutoweka ni maamuzi yangu.

Je unajisikia vizuri zaidi ukiweka post kwenye blog yako na ukapata maoni ya watu zaidi ya 20 au ukipata maoni ya mtu mmoja mashuhuri tu?

Ndiyo kwa sababu najua ujumbe umewagusa.

Je unasema blog yako kuwa inamafanikio iwapo unapata watu wengi wa kusoma au unapata watu wengi wakuacha comment kwenye blog yako?

Kikubwa ni kuona watu wanapata taarifa muhimu na zilizo na maana kwa jamii, si bora taarifa.

Je blog yako unatumia jina lako kamili au unablog kwa kutumia kivuli kingine na watu wanasoma na kuenjoy blog yako lakini hawajui wewe ni nani?

Kama nilivyoeleza hapo juu, Mamapipiro ni nickname yangu. Jina langu halisi ni Dina Ismail na ndilo lipo kwenye kichwa cha habari ya blog yangu.

Ni nini baadhi ya malengo yako ya mwaka huu kwa ajili ya blogu yako au unaonaje mwenyewe kwa kipindi cha mwaka mmoja ua mitano toka sasa hivi blog ya itakuaje?

Pamoja na kuhakikisha naleta changamoto katika tasnia hii, pia maboresho makubwa yanakuja kuanzia kimwonekano na hata uwingi wa taarifa nzuri na zenye maana.

Je upi ujumbe wako kwa wale watu wanaotaka kuanza kublog?

Waanzishe blog kwa maana wanayokusudia si kufuata mkumbo.

Je kwa maoni yako ni lengo gani kubwa kwa mwanablogger?

Kutimiza wajibu wako wa kuwapa kitu ulichokusudia wasomaji wako.

Watu wengi wanafikiria kublog kwa ajili ya kupata hela. Je ni nini baadhi ya vidokezo kwa watu wanaofikiria kufanya hivyo? Je, ni ukweli upi wa baadhi ya matarajio yanayohusina na nini kinaweza kufanywa na nini hakiwezi kufanywa wakati wa kublog?

Ndiyo kuna watu wanaochukulia kublog ni kwa ajili ya kupata hilo, kwangu mimi ni kinyume kwani natumia blog hii kama sehemu yangu ya kazi ya kujitolea. Ingawa kuna baadhi zinapata matangazo yanayolipiwa lakini hiyo ni kama bahati tu.

1 comment:

Anonymous said...

aisee nilikuwa ciijui blog hii lakini kupitia humu nimeisoma na kuona ni moja ya blogs makini, huyu dada huwa namsoma mambo yake katika magazeti ni mmoja ya waandishi mahiri wa habari za michezo, kila la heri nyuma yako