Featured Blogger - Sweetbert Philemon

  
Kutana na mwana blogger wetu wa week hii kutoka The Lake Zone Link

1. Unaweza kutuambia kidogo kuhusu wewe na blog yako? 
 Naitwa Sweetbert Philemon toka Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha. Nimeanza kuwa Blogger mnamo Mei 2011, ambapo ndipo ilikuwa mara yangu ya kwanza kufungua blog wakati huo nikitumia Jina Best Bongo Music kama jina la Blog hiyo, lakini nilisitisha kutokana na kutokuwa na vifaa vya kutosha. Hadi mapema Mwaka huu ambao blog yangu nimeibadili kutoka This Is Habari hadi kuwa The Lake Zone Link kutokana na sehemu ambayo natokea. Nimekuwa nikijisikia furaha sana pale ninapohisi kuwa nab log na inafanya kazi. 

2. Je, wewe kazi yako ni kublog tu au hii ni kama kazi ya muda tu au hobby? 
 Kublog kwangu kumegawanyika katika aina tofauti, kwanza kwangu ni kama Hobby kutokana na kupenda sana masuala ya Information Technology, lakini pia kwangu naichukulia kama kazi yangu binafsi kutokana na kuwa nina Muda ambao nimeutenga kwa ajili ya kazi hii kama Kazi zingine nifanyazo. 

3. Jinsi gani unaanza kublog na kwa nini? 
Ili uweze kuanza kublog kwanza ni lazima uwe na akaunti ya barua pepe ya mtandao wa Gmail, baada ya hapo utajisajili vile vile kwa kutumia barua pepe katika mtandao wa Google ufahamikao kama www.blogger.com, ambapo baada ya kusajiliwa utaweza kuanzisha blog kwa ajili ya kazi hiyo. Unablog pale unapohisi unamuda wa kufanya hivyo na kuna mambo mbalimbali ambayo unahitaji kuijulisha jamii kwa namana nyingine ya kimtandao 

4. Nini changamoto unazozipata kwa kuwa na blog? 
Changamoto ninazopata kwa kuwa na blog kwanza ni Gharama za Uendeshaji kama pesa ya kuwa na vifaa mbalimbali vya kisasa zaidi kama Computer na Camera, Upatikana wa Mtandao(Network) hii ni moja ya changamoto kutokana na mazingira mengine kutokuwa na mtandao kabisa hivyo kushindwa kuifanya kazi, Upatikanaji wa Habari unakuwa mgumu kwani inabidi muda mwingine kutumia habari zilizokusanywa na wanablog wengine, Kufahamu mahitajio ya mashabiki, wakati mwingine inakuwa ngumu kufahamu ni nini wadau wako wanahitaji kutokana na kutoacha maoni yoyote katika sehemu ya maoni, hivyo kufanya kazi kwa kubuni, Mwisho ni muda inafikia kipindi inabidi kutumia muda wa shughuli nyingine katika kublog kutokana na Habari inahitaji kuandikwa muda gani. 

5. Ni miaka mingapi sasa umekua ukiblog? 
Ni Mwaka mmoja na Nusu tangu nimekuwa nikiblog 

6. Unafanya nini wakati ukiwa hushughulikii hii blog yako? 
Wakati si shughulikii blog hii nafanya majukumu mengine ya Kishule na Nyumbani pia ili kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa, bila kupoteza kimoja wapo. 

7. Ni mara ngapi unafikiri juu ya blog yako wakati uko mbali na kompyuta?
Inajirudia kwa mara nyingi kufikiria kuhusu blog yangu pale ninapokuwa niko mbali na Kompyunta hasa kuhusu Mwonekano wake, Habari zilizopo na Wadau wangu wa blog. 

8. Ni nani wasomaji wa blog yako? 
Asilimia kubwa ya wasomaji wangu ni Vijana kutokana na Habari za kiburudani ambazo zinakuwepo. 

9. Je ni mitandao gani mingine ambayo unatumi ili iweze kukusaidia kuitangaza blog yako ili iwafikie wasomaji walengwa wa blog yako? 
Mfani Twitter au Facebook Mitando migine ambayo natumia kuitangaza blog yangu ni pamoja na Google Plus, Alexa, Networkedblog pamoja na facebook na Twitter 

10. Nini hasa ni changamoto kubwa wakati unatengeneza post ya kuweka kwenye blog yako na kwanini? 
Changamoto wakati wa kutengeneza post ni pale unapokuwa unatumia post kutoka kwa wanablog wengine, kwani itakuchukua mrefu sana mpaka kuikamilisha post hiyo, Mfano kupata picha zinazoendana na post hiyo, kuweka sauti za muziki ambapo itabidi uingie katika mitandao mingine kutafuta vitu kama hivyo. 

11. Unafanya nini iwapo kuna wakati huna la kuandika kwenye blog yako? 
Wakati sina la kuandika katika blog yangu, huwa nafanya marejeo katika blog yangu kuangalia makosa ambayo yamejitokeza na pia kuangalia vitu vya kuongeza na kupunguza katika designing(Mwonekano) wa blog yangu ili iendelee kufana. 

12. Je ni nini mkakati wako na blog yako kwa ujumla? 
Mkakati mkubwa uliopo katika blog yangu, kwa ni kuifanya Website ili uwe ni mtandao mkubwa ambao utakuwa na kazi ya Kuhabarisha jamii mambo mbalimbali,Hadi kufikia hatua ya kuweza kaujili vijana wengine kushirikiana katika kazi hii, kama ilivyo mitandao ya Habari mingine mikubwa Duniani mfano ABC. 

13. Je ni bora kupata ukweli au uchunguzi wa jambo unalotaka kuliandika kwenye blog yako wewe mwenyewe au kupitia mtu mwingine? 
Ni bora kupata ukweli au uchunguzi wa jambo mwenyewe, hii itasaidia katika kuwa na uhakika na kile ambacho unakifanya, Lakini pale inapohitajika mtu mwingine kuwa na ukweli huo unaweza kuutumia labda kutoka na namna ya kukamilisha uchunguzi huo. 

14. Ni jambo gani bora blogger anaweza kutoa kwa wasomaji wake? 
Jambo bora ambalo blogger anaweza kulitoa kwa kwa wasomaji wake, ni jambo ambalo linawasaidia wasomaji na kuwapa uhakika wa jambo fulani ambalo walikuwa hawalijui au wana mashaka nalo, hivyo kuwafanya wapate uhakika huo, na kuweza kuwasaidia. 

15. Ni jinsi gani (mtu) anaweza kuelezea style ya yako unavyo blog? 
Mtu anaweza kuelezea style yangu ya kublog kwa namna tofauti tofauti kama, Uhabarishaji wa jamii, Kuburudisha jamii lakini pia anaweza sema ni kuonyesha uwezo wangu katika masuala ya mitanda 

16. Ni nini imekuwa mkakati wako kwa ajili ya kujenga kujulikana kwa mwenyewe na blog yako? 
Mkakati wa kwanza ni mimi mwenyewe kujitambulisha ndani ya blog ili watu kunifahamu pale wanapoitembelea, lakini pia mkakati wa pili ulikuwa nia Ukurasa wangu facebook ambao unanitambulisha kama mmiliki wa blog hiyo, pia twitter na mkakati mkubwa ni kupitia Tanzania blog Directory List ambapo blog yangu nimeitambulisha huko, Lakini pia ni katika mtandao wa Google na njia ya Jamaa zangu walio katika Media. 

17. Kila mtu ana post anayoipenda au anayoichukia. Je wew ni post ipi unaipenda sana na kwanini? Na ni post ipi unaichukia sana na kwanini? 
Napenda sana post ambayo imejaa uhalisia wa picha na video pamoja na maneno ambayo itatoa uhakika zaidi. Nachukia post iliyojaa maelezo pekee kwani msomaji hatapa kuhakiki kwa kutumia vithibitsho halisia. 

18. Je ni bloggers wapi ambao wewe unawaangalia na kufuata nyayo zao? Na kwanini?  
Bloggers ambao mie nawafuata ni pamoja na Dj Choka kutokana na namna anavyotoa mchango wake katika sanaa ya Muziki hapa nchini, lakini pia Millard Ayo kutokana na aina yake kuwahabarisha wasomaji kwa namna tofauti katika mtandao wake na kuwa update kwa kiasi kikubwa na Mx Carter wa Gonga Mix kutokana na namna ya mwonekano wa mtandao wake, hivyo kupitia kwao najifunza mambo mengi 

19. Hebu tuambie ni watu gani umewahi kukutana nao wakati ukisughulikia post za kuweka kwenye blog yako?
Nimekutana na Jamaa yangu Mtaki R Myenjwa pamoja na Norles Wales kipindi hicho nilikuwa nafuatilia post inayohusu ufunguzi wa Jiji la Arusha. 

20. Je unafikiria kuwa unadaiwa na mtu akiyeacha comment/s kwenye blog yako?
Ndiyo nitakuwa na daiwa kuijibu comment hiyo ili kuonesha ushirikiano wangu na wasomaji wangu 

21. Je kunadhamani kujibu comment iliyoachwa kwenye blog yako wakati ukijua kuwa huyo aliyeiandika labda hatarudi kusoma jibu lake tena? 
Thamani ipo kwani kuwepo kwa comment hiyo na kuijibu kutasaidia na wasomaji wengine wakuachie pale comment zao ambazo zitakusaidia katika maboresho mbalimbali ya blog yako na pia kutambua ni jinsi gani watu wanaitembelea. 

22. Je, umewahi kufikiria kuacha kupost comment ambayo iko negative kwako na ukijua hamna mtu atakayejua? 
Hapana sijawhi fikiria hilo kwani itafanya wasomaji wengine waone naruhusu upuuzi katika blog yangu. 

23. Je unazitreat tofauti au unafikiri watu wanaoacha comment kwenye blog yako na kuacha majina yao yaonekane wazi wanastaili comments zao kujibiwa au hata kuacknowledge kuwa umeona maoni yao? 
Kila kitu nisawa kwa yule aliyeacha au ambaye hajaacha jina , ikiwa tu comment zao zina maelezo yenye kuhitaji majibu. 

24. Je, unafikiria ni makosa kucomment kwenye blog yako kwa kutumia jina lingine? 
Sio makosa kwani ni kama njia yakuonyesha msomaji wako mpya nini atafanya katika eneo kama hilo katika blog. 

25. Je unazichukulia comments zote sawa unazotumiwa kwenye blog yako bila kujali maoni uliachwa?
Hapana Comment zote haziwezi kufanan kila moja itakuwa na ujumbe wake hivyo inabidi kujali zaidi maoni yaliyoachwa kufahamu utafanya nini. 

26. Je, unaamini comments kwenye blog yako zilizoandikwa kwa urefu sana zinahitaji kuzawadiwa zaidi kuliko zile zilizoandikwa kwa ufupi tu? 
Sio kweli urefu wa comment sio kwamba ndio imeendikwa kitu kikubwa ndani yake,bali hata comment fupi inaweza kuwa na ujumbe mzito kwako na wa kuufanyia kazi zaidi. 

27. Je wewe ni mtu ambaye uko rahisi kukata tamaa? 
Kwangu sio rahisi kukata tamaa, kutokana na mihangaiko ambayo nimeipata katika kublog, nitaendlea kuwepo. 

28. Je unaedit picha zako ili ziwavutie sana wasomaji?
 Hapana napenda zaidi picha iliyo na uhalisia kwa msomaji, lakini pale inapohitajika kufanya hivyo huwa na edit. 

29. Je unaepuka kuweka post ambazo ziko very controversy kwasababu ya kuogopa watu hawatakubaliana na wewe au huna hizo post? 
Naepuka kuafanya hivyo lakini inapofikia hatua ya kuzingatia maslahi ya jamii, inabidi kufanya hivyo. 

30. Je unajisikia vizuri zaidi ukiweka post kwenye blog yako na ukapata maoni ya watu zaidi ya 20 au ukipata maoni ya mtu mmoja mashuhuri tu. 
Najisikia faraja sana pale ninapopata comment hata moja tu lakini yenye maoni ya kunijenga zaidi katika blog yangu na siyo kujali wingi na umashuhuri wa mtu 

31. Je unasema blog yako kuwa inamafanikio iwapo unapata watu wengi wa kusoma au unapata watu wengi wakuacha comment kwenye blog yako? 
Blog itakuwa na mafanikio zaidi pale inapopata wasomaji wengi zaidi kwani itatangazika katika watu wengi na kufikia watu wengi zaidi, zaidi ya kuwa na comment za wasomaji wachache ambao hawataitangaza blog yako zaidi 

32. Je blog yako unatumia jina lako kamili au unablog kwa kutumia kivuli kingine na watu wanasoma na kuenjoy blog yako lakini hawajui wewe ni nani? 
Natumia jina la Kanda ya ziwa The Lake Zone Link, kutokana na sehemu ambayo natokea mkoa wa Mwanza na watu wanaenjoy kuona nawakirisha kanda hiyo. Wanatambua mimi ni nani kutokana na utambulisho ulio ndani ya blog. 


33. Ni nini baadhi ya malengo yako ya mwaka huu kwa ajili ya blogu yako au unaonaje mwenyeew kwa kipindi cha mwaka mmoja ua mitano toka sasa hivi blog ya itakuaje? 
Nina Malengo ya kufanya jitihada za kupata vifaa vipya vya kuendeshea blog hii kama Laptop/Kompyunta, Camera, Moderm na vitu vingine ambavyo vitahitajika,ili kuanzia mwaka huu na kuendelea blog hii iwe ni moja ya mitandao ya kijamii mikubwa nchini kwa watumiaji wa mitandao. 

34. Je upi ujumbe wako kwa wale watu wanaotaka kuanza kublog? 
Ujumbe ni kuwa kwanza wajiandae kikamilifu hasa kuwa na vifaa vya kuendeshea blog na wala sio mahudhurio ya internet cafe, itawagharimu pesa nyingi, ni heri kuwa na vifaa vyako mwenyewe. Na pia hizo blog zao wazisajili ili ziweze kutambulika Nchini. 

35. Je kwa maoni yako ni lengo gani kubwa kwa mwanablogger? 
Lengo kubwa kwa wanablogger tutumie nafasi hii kujitoa kwa sehemu ambazo tunaona zimefumbwa katika jamii zetu hivyo kuibua sauti zao, na kufikisha ujumbe wao, hasa katika kutetea haki za jamii nzima

36. Watu wengi wanafikiria kublog kwa ajili ya kupata hela. Je ni nini baadhi ya vidokezo kwa watu wanaofikiria kufanya hivyo? Je, ni ukweli upi wa baadhi ya matarajio yanayohusina na nini kinaweza kufanywa na nini hakiwezi kufanywa wakati wa kublog? 
Kublog si kwa ajili ya kupata pesa pekee kama watu wengine wanavyodhania zaidi, bali kublog ni namna ya kuisaidia jamii katika sekta mbalimbali kupata sauti itakayowafikia walengwa. Wakati wa kublog huwezi fanya mambo ambayo hayana interest na jamii.

Asante sana na tunakutakia mafanikio mema katika masomo yako na pia katika blog yako. 

4 comments:

emuthree said...

Nimeshukuru sana aina hii ya kuwatambulisha wanablo na blog zao, sijui kama inawezekana, kwani inahitaji utalaamu zaidi, ....wa kuwakutanisha wanablog `kimtandao' zaidi ya mmoja..huko ulaya inawezekana au? Ni wazo tu mpendwa

Sweetbert Philemon said...

Thanks Much. Tanzania Blog Award, mnatoa support kubwa sana kwa blogger, nawashauri na blogger wengine waingie katika directory hii ili waweze kutambulika zaidi na zaidi. Kazi njema.

Tanzanian Blog Awards Admin said...

Hi Emu three ijakuelewa swali lako. Uamaanisha kuwakutanisha wanablog online? I guess hapo ni watu wakipenda na kuanza kuzoeana....huwezi waambia watu wakutane kama hawajuani au hawana interest..but I know G+, meeting plus etc mnaweza kutana online watu kama saba mara kwa mara moja. Ila kwa tatizo la Tanzania ni cost za data ni nyingi...Skype au G+ sio cheap....kama sijakujibu swali lako hebu uniambie zadia...

emuthree said...

Nilikuwa na maana kuwa kila wiki unamtambulisha mwanablog wa wiki, au sio, huyo mwanablog akishajielezea hivyo kama ulivyomtahini, sasa wiki hiyo yake, anakuwa hewani, na anapata maswali toka kwa wanablog wenzake moja kwa moja.
Kiujumla umeshanijibu swali langu, ila nilikuwa naelezea ni nini nilikuwa nimekusudia.

Shukurani mpendwa.