Week hii mwanablogger wetu ni Tryphone Chasama anayeishi Dodoma. Tryphone Chasama
ni mmiliki wa blog ya BongoNewz Blog. Blog yake inahusu habari,
burudani, habari za jamii na siasa kwa ujumla.
Ifuatayo ni historia fupi ya Tryphone na pitia blog yake BongoNewz Blog
kusupport na kufahamu mengi kuhusu blogger huyu:-
“Elimu yangu ni Shahada ya sayansi (BSc Education) na kwa
sasa ninaendelea na masomo ya shahada ya pili katika chuo kikuu cha UDOM. BLOG
yangu inaitwa BONGONEWZ BLOG, niliianzisha mwaka jana lakini sikupata muda
mwingi zaidi wa kuifanyia kazi mpaka mwezi Julai mwaka huu ambao ndio nilipata
muda zaidi wa kuishughulikia na mpaka sasa nina muda mwingi wa kuishughulikia.
Blog yangu kama nilivyosema inatumia kivuli
lakini jina langu lipo kwenye blog sehemu iliyoandikwa (about me) na hapo
nimejielezea vizuri mimi ni nani.
Nimekua nikiblog kwa muda wa mwaka sasa na kitu kilichonifanya nianzishe blog ni hali tu ya kuipenda hii kazi kwani ni kazi ambayo nilipanga nije kuifanya. Kwa sasa sina kazi nyingine zaidi ya kublog na ninaifanya hii pia kwa ubunifu wa hali ya juu kwani zaidi ya kuwa ni kazi yangu pia ni hobby vilevile.
Changamoto niliyonayo katika kublog ni kupata habari, pia vitendea kazi kama kamera ni changamoto kwangu. Wasomaji wa blog yangu ni watu wa rika zote kwani blog yangu ina habari zinazomhusu kila mtu.
Ili kufanya blog yangu ijulikane zaidi, natumia mitandao ya kijamii kama Facebook, twitter na mtandao wa Google plus. Mikakati niliyonayo kwa ajili ya blog ni kupata wasomaji wengi zaidi na blog yangu kuwa miongoni mwa blog maarufu hapa Tanzania na pia nje ya Tanzania.
Style ninayotumia kublog ni ile inayoambatana na picha za matukio husika au hata kama sina picha za matukio husika hua natafuta picha za wahusika kupitia mitandao mingine ili kufanya post ziwe na mvuto zaidi. Ninachoamini ni kwamba, picha zinahabarisha zaidi ya maneno, na zinaleta mvuto kwa msomaji pia kuendelea kusoma na kumfanya arudi tena kwa siku zingine.
Bloggers ambao wamekua kama dira kwangu na ambao natamani nipite katika njia walizopita ni Issa Michuzi, Magid Mjengwa, Haki Ngowi na John Bukuku. Nawapenda sana hawa Bloggers kwa sababu ya kazi wanazozifanya. Kublog imekua ni kazi kwao na wanaifanya kazi hii kwa umakini mkubwa.
Mtu akiacha comments kwenye blog sio lazima nimjibu ila itategemea na aina ya comment aliyoacha kwani kuna comments zingine zinahitaji majibu, na baadhi ya comments hua ni maoni tu ya mhusika kuhusu post iliyopo kwenye blog…Lakini comments zinazohitaji majibu hua nakuwa makini sana kumjibu kwa wakati kwani nahisi ni kama deni kwangu na hua najisikia vizuri sana kumjibu. Kujibu comments za wasomaji ni kitu cha thamani sana haijalishi kama atarudi kusoma au la, kitendo tu cha kujibu comments kitamfanya msomaji arudi tena na tena na awe na uhuru wa kucomment juu ya kitu chochote kile anachofikiria.
Kukata tamaa katika maisha yangu ni kitu ambacho naona ni kosa kubwa sana, siwi mwepesi kukata tamaa hata kama kazi ninayofanya inakua na changamoto nyingi sana. Malengo yangu kwa mwaka huu ni kuwa na wasomaji wengi zaidi, na kwa kipindi cha mwaka mwingine ujao blog hii itakuwa miongoni mwa blog zenye wasomaji wengi zaidi hapa Tanzania na hata nje ya nchi.
Ujumbe wangu kwa watu wanaotaka kublog ni kutosita kuanza kazi hii kwani ni kazi kama ilivyo kazi nyingine. Na wasikate tama pale wanapokutana na changamoto mbalimbali.
Lengo kubwa kwa mwanablogger yeyote ni kuwa na idadi kubwa ya wasomaji na blog yake kujulikana zaidi….na zaidi ya hapo ni kuifanya kazi ya kublog kuwa kazi inayomwingizia kipato.”

Tanzania
blog Awards inakutakia mafanikio mema katika masomo yako na blog yako kwa
ujumla.
3 comments:
Asanteni sana kwa msaada wenu na pia kwa kunitakia mafanikio...natambua mchango wenu mkubwa hasa katika fani hii ya kublog. Nawatakia pia mafanikio katika kazi zenu
Hongera sana Bongonews, tupo pamoja
Thanks Emu-three, pamoja sana
Post a Comment